Friday, August 14, 2009

maisha bora yashafika hamyaoni?wengi mlikuwa mkisubilia wanasiasa waje na maisha bora kwa kila mbongo kama walivyoahidi. sasa huu ndio wakati wenyewe sasa. nauli za mabasi ya mikoni zimeshuka na zinaendelea kushuka kwa kisingizio kuwa bei ya mafuta nayo imeshuka. inasemekana nauli za dala dala nazo zitapungua kati ya Sh 50 mpaka 100.

si mafuta yameshashuka bei?
wakuu wa mikoa wamebadirishwa ili kuondoa sura za kamatakamata ile mamantilie machinga nk. kubwa zaidi mkuu wa mkoa wa Dar, Willy Lukuvi, ameisha tangaza kuwazuia wale Mugambo wote waliokuwa wakiwapiga akina mama na kuwavua nguo machingazi.

amewapiga marufuku kwamba kazi ya
o sio njema na kuipaka matope kibao kiasi kwamba ukiwashitaki wanaweza kufungwa maisha au kama vile serikali ilikuwa nje ya nchi wakati wanafanya unyama ule! nakwambia mambo ni mazuri sasa kwani bidhaa zitapungua bei zaidi na zaidi.

machinga wanarudi mitaani. nilikuwa Bukoba, wale jamaa wanaosafirisha kwa piki piki (maarufa kama Asekido / boda boda) wamesheheni mitaani na wanafanya kazi bila wasi wasi wala bugdha. mambo mazuri hayo.
bila shaka bei za mazao zitapanda na mkulima atakuwa hurukuuza apendako. kama unataka kujiunga na elimu ya juu huu ndio weakati kwani nakuhakikishia kuwa watakaodahiriwa mwaka huu watalipiwa gharama zote na wale wa mwaka kesho (full sponsord) kwani wakati wa kampeni zilizopita nilikuwa mwanachuo na sikuwa na sifa za kupata mkopo lakini tulipata sote na ni full! Jiunge mzee. kama unataka kuanzisha biashara huu ndio wakati kwani hata usipofuata kanuni sawatu na twende mbele. ni wakati wa kuvuna matunda ya uongozi na ni wakati wa kuyaona maisha booooora kwa kila Mdanganyika.

mzee wa changamoto huwa haelewi inakuwaje wanasiasa, sasa hili ndilo jibu. kabla ya januari mwakani, utakuwa na kila sababu ya kuendelea kuichagua sisiem na viongozi wake. mbuzi wa kafara walee mahakamani. nakuhaikikishia wengi watafungwa japo waweza usiwaone tena.

mramba, Yona, Mgonja, Liyumba, Zombe, Richmonduli, nk. ni wakati wa kuonja joto ya jiwe kwa makosa yao japo mwisho wao ni vigumu kwako kuusikia. mambo ya politikisi hayo nisiyopenda saana kuyaongelea. ila huu ni wakati wa neema na wakati wa dili. ile ahadi ya mabasi yaendayo kasi kwa Dar!!!!!

tutaanza kukabana tena koo kwa kutimuana na kusaini mikataba ya Hovyo mwanzoni mwa 2011. politiks

10 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Ahaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! Sasa ona wanasiasa wetu wasivyo na aibu. Watatenda haya haya ambayo umesema. Hii inaonesha ni jinsi gani wanavyojitahidi kutengeneza kima Martin Luther wengi tunaoweza kuja na I HAVE A DREAM zetu ambazo wala hazihitai akili za ziada. Yaani kwa kuangalia nchi inavyoongozwa na siasa zilizo "disposable" ndani ya miaka mitano, huna haja ya kuwa Shgeikh Yahya kujua kitachofuata,m kitakachobadilika na kitakachomdanganya mwananchi ili "kumuwekezesha" Mbunge ama rais. Ndio maana nilisema chaguzi zibadilishwe. Tuwa na ule wa katikati ya muhula wa kumchagua Mbunge ili kama tutaona Rais anavurunda basi tumchgagulie wabunge walio na mwamasho ama kama wabunge wanamwangusha Rais, basi tumpe watakaomsaidia kufanya atendayo kwa jamii. Lakini swali ni kuwa hata tukifanya katikati ya muhula, watachaguliwa wenye kujua kazi ama ambao wanahonga kiasi kikubwa?
Kaka, tuendelee kuelimisha kwqani siku yaja kwa wananchi kuyakumbuka haya.
Nuff RTespect
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima said...

You can fool some of the people all of the time and all of the people some of the time but you can't fool all of the people all of the time

Wakati utafika!

Chacha Wambura said...

Ayaaa!!! mbona mimi nshaganganyika tayari? sasa nami naanza biashara ya kuchuuza wasomi! nani ataniona?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

karibuni

MatteJerry said...

Maandalizi ya Uchaguzi, Safiri ijayo inabidi kufafanuliwa maisha bora kwa kila mtanzania maana yake ni nini?

I wonder what will be CCM slogan in the next election.

chib said...

Si mchezo!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaazi kwelikweli hapa.

Fadhy Mtanga said...

Ze mwakani, they call it twenty ten.

Mambo yake itakuwa ni kama sinema. Barabara zalimwa, shule zakumbukwa vitabu. Mwaka hutosikia migomo vyuo vikuu maana matatizo yatashughulikiwa kwa spidi ya mwanga.

Kila kitu.

Kila kitu.

Mwakani.

Lakini mwaka huo twenti teni,

Wengi watafulia. Halafu watakosa maji ya kusuuzia.

Ramadhani Msangi said...

Taaanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo woteeee, nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana.

Kamala, weka beat hapo, na mwingine gitaa, wengine wachagize kwa miluzi, huku tumekunja nne tunatikisa tikisa mguu ulio juu.....maisha ni burudani kwakweli ndani ya Tanzania.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matejerry, dont worry, slagan itakuja tu. kwani ile ya ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya si uliisikkia enzi za uchaguzi? kaa mkao wa kula. ila labda tutalijadili hilo pia.