Wednesday, August 12, 2009

maisha ya Dar ni kurudi nyuma nyuma tu

mwezi september nitakuwa nimekamilisha miaka mitano tangu nianze kuishi jijini dar na katika miaka hiyo nimeishi maeneo kadhaa na kutembelea kwa sana maeneo kadhaa. nimeishi mitaa ya Ukongo, Mwenge, mlalakuwa, Changanyikeni, Ubungo, Kibangu, Tegeta, MtoniMtongani, Posta (city centre), na magomeniKagera.

kwa miaka yote hiyo, masha ya Dar ni ya ajabu sana. kinachoniacho hoi ni reverse au kwenda kinyume nyume kwani kila kitu kinarudi nyuma na labda yangetengenezwa magari ya kurudi kinyume pekee,. ishu ni Muda wa kuwahi asubuhi.

nikiwa mwanachuo wa IFM, nililazimika angalau saamoja kamili niwe kituoni ili niweze kupata gari ya kuwahi mjini na kuwahi msongamano wa magari. baadaye ikawa saa kumi nambili na nusu, ikaja saa kumi nambili kamili na sasa ni saa kumi na moja na nusu.

kama unafanya kazi zako mjini na usafiri muhimu kwako ni dala dala, basi wewe wahi tu mapema yaani saa kumi na moja asubuhi uwe kituoni vinginevyo utapitia dirishani. ukitaka kupanda dala dala inabidi uwe na nguvu vinginevyo uruke dirishani. hata kama unagari binafsi foleni utakona nazo. ukimaliza zengwe la foleni basi parking ni ishu kwako. mjini hakuna parking na zikiwepo basi hazina usalama.

nyumbani nako vijumba vyetu vimebanana. vimejengwa bila parking kwa hiyo baada ya kufika nyumbani na gari lako, inabidi upige rivasi ya kuelekea kwenye parking ili ulaze gari lako vyema. yaani maisha ya Dar inabidi urudi nyuma nyuma ili mambo yaende. itafika wakati (nao sasa waja) ambao wakazi wa Dar watalazimika kuwa wanaamka saa tisa usiku ili kuwahi town.

yaani inauma. nipandapo dala dala huwa napanda na vitoto vya shule. hivi huwa vinachapa usingizi kama viko home vile kwani uamshwa kabla ya wakati uliopangwa kwao kulala kumalizika. ndoa hazina maana jijini dar na hivyo wanandoa hawajuani kwani muda woote mko safarini ya kwenda msikofika.

nyumbani na chumbani kila kitu inabidi mfanye fasta ili time isichelewe. kwa hiyo mnafanya mambo yenu kama vile mmeibana au mnaogopa kufumaniwa wakati nyie ni wanandoa halali. watoto wanalelewa na mahosegel na hawawajui wazazi wao vyema. si huja wamelala na huondoka wameamka?

ni maisha ya Dar, ni ya kinyume nyume tu yaani reverse. tumechagua kuishia barabarani na tuendako tukifika tunagundua hatujafika bali inabidi tuendelee tu kwenda na kwendaa. labda tutafika!

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Bongo Darisalama, ndo taabu ya kuishi Dar. Lakini pamoja na hayo watu kibao washatua mabegi wanasema hawatoki.
Wote wapo Dar es Salaam.

chib said...

...Na wengine wanaendelea kuja kila kukicha

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labda mimi nihame nini maana!!

Foundation said...

KL mbona huhami sasa? nakusubiri huku vijijini kwetu kwa wanaynchori na wanyanchoka!