Wednesday, August 26, 2009

wahubiri wetu na siku za mwisho

"Siku za mwisho zimekaribia. wenye dhambi tubuni, na watakatifu jiandaeni kunyakuliwa na bwana, maana atakuja kama upepo au radi, tutaenda mbinguni, wenye dhambi watabakia wanalia na kujuta na kusaga meno"

hayo ni maneno yanayosikika kwenye Nyumba za ibada. mchungaji mmoja aliwahi kunipiga huo mkwara, aliponitambulisha kwa mke wake, yule mama ailikuwa na mimba. sasa kama ni siku za mwisho kwa nini anampachika mke wake mimba? siaache twafa? au

kwanini anawasemea wale anaodhani wanatenda dhambi?

eti watalia na kusaga meno, wasio na meno je watasaga nini?

wewe kama bado unawaamini hawa majamaaa, du!!!

15 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala, Kamala Duh!

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!
Kwani dhambi ni nini na yapimwaje?

Chacha Wambura said...

jamani mbona mwanichanganya?


Tunaambiwa kuwa 'itakuwa kulia na kusaga meno'. Twaambiwa kuwa ukikufa unaacha mwili hapa na inakwenda 'LOHO' yako kwenye kiti za uzima kwa ajili ya hukumu. Sasa utaliaje na kusaga meno ilhali huna mwili? hayo meno yatatokapi wakti roho ni kibogoyo?

KL, twambie..ukikufa na ukakutana na Sir 'god' je unajiumba tena na kuwa mwili kama ulivo sasa?

Cheers!!!

Masangu Matondo Nzuzullima said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima said...

Biblia imejaa lugha ya taswira na mara nyingi kisemwacho sicho. Yesu mwenyewe alipenda sana kuzungumza kwa kutumia taswira na mifano ambayo iliendana na mazingira ya wakati ule - mifano ambayo kwa wakati wa sasa yaweza ikatatanisha. Ndiyo maana vitabu kama vya Danieli na Ufunuo vinatatanisha mno hata kwa wanathiolojia wa leo na kila mmoja ana tafsiri yake - Waroma wana tafsiri yao, Wasabato, Wapentekoste n.k. Kwa hivyo isome Biblia kwa mtazamo huo.

Nimekuwa nikifuatilia vipindi vya kiugunduzi vinavyorushwa na History Channel na Discovery Channel hapa Marekani kuhusu ukweli wa Biblia, Yesu mwenyewe hasa kama binadamu alikuwa nani n.k. Vipindi hivi vimekusanya wataalamu mbalimbali - Wanaanthropolojia, Wanasosholojia,Wanahistoria, wanasayansi na kila aina ya taaluma (siyo watu wa dini). Mijadala na uchambuzi wao si wa kidini na nimejifunza mengi kuhusu Biblia, Ukristo na mabadiliko yake uliyoyapitia. Nitaweza kuandika zaidi mjadala ukiendelea.

Kulia na kusaga meno mimi nadhani ni sitiari (metaphor) tu kuonyesha jinsi huzuni na uchungu utakavyokuwa siku ile. Mtu anayelia na kusaga meno bila shaka yumo katika majonzi mazito mno; na hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku ya mwisho. Yule ambaye hana meno pengine ndiyo yumo kwenye hatari zaidi kwani huyu atasaga fizi zake na kujitoa nyama na damu.

Haya ni mambo ya imani; na ukiamini inakuwa. Nimeshashuhudia wanawake wagumba wakitambika katika miti na makaburi ya wahenga na kupata watoto. Kijijini kwetu (Busheni) wakati ule tukikua wanakijiji walikuwa wakichangishana pesa na kwenda kutafuta "ngemiombula" (mleta mvua) wakati wa ukame ambaye alifanya matambiko pale kijijini na mara kwa mara kweli mvua zilinyesha. Imani!

Kama huamini katika Yesu na Ukristo ni sawa lakini waruhusu wanaoamini waamini! Bila shaka hata wao hawatakubaliana na kile unachokiamini wewe (kama kipo). Na ushukuru unazungumzia Ukristo kwani sidhani kama unaweza kuwa huru namna hii katika kuzungumzia Uislamu! Unaikumbuka adhabu aliyopewa Salman Rushdie?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mzee wa C.Moto hata mimi sijui dhambi ninini.

Chacha, usipokutana na sirGod kabla ya kufa ni vigumu sana kukutana naye baada ya kufa.

matondo umenifurahisha kwani ulianza vizuuuri sana lakini ukaishia kuwa padri, mchungaji, mjuakweli pekee, mwoga a moto, nk.

mwisho wa comment yako unaonyesha kama vile umechukia na unakemea fulani hivi na kunitaka niwaache wanaoaminishwa waendelee kuaminishwa. hata mimi niliwahikuaminishwa lakini kwa kuitafuta kweli, nikawa huru na sasa siaminishwi bali nafanya na kuona.

wale watambikaji hawakuamini bali walitenda na ikawa.

kulia na kusaga meno ni mikwara tu yakijinga ndio maana nikasema kuna wasio na meno ya kusaga!
mbona hujibu swali langu juu ya kwanini wahubiri mjihusishe namaisha ya watenda zambi? unafikiri bila watenda dhambi kuna mahubiri?

niwaache wanaomwamini Yesu, una uhakika gani kama simwamini? mbona nameditate wakati na yesu alikuwa meditator mzuri? mbona siri vyakula vizuiwavyo na bible?

sijui kama ssimwamini au kumkubali yesu wakati labda nadhani siwaamini wahubiri, na dini. si unajua kuna tofauti kubwa kati ya dini na Yesu? si unajua alizichukia sana dini?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mulangira Kamala;

"...mwisho wa comment yako unaonyesha kama vile umechukia na unakemea fulani hivi na kunitaka niwaache wanaoaminishwa waendelee kuaminishwa..."

Sijachukia na wala sikemei cho chote. Kama kuna kitu nakithamini ni uhuru wa kuendesha mijadala huru bila chuki, matusi wala bugudha. Tazama nilivyolalamika kuhusu jambo hili hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/08/ati-hatuwezi-kujadili-jambo-bila.html. Kama nimesikika kama nimechukia au nakemea basi samahani. Hata sijui jinsi ya kukemea kwani hiyo ni fani ya walokole na mimi si mmoja wao.

Nadhani nilichotaka kusema ni kwamba mambo ya imani ni magumu sana kwani ni IMANI ya mtu, na mijadala mingi ya imani ambayo nimeshawahi kuiona/kushiriki huwa haifiki popote kwani hakuna mtu anayekubali kulegeza kamba kwa sababu ni IMANI yake. Wapo watu ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya imani zao.

Yawezekana "kulia na kusaga meno ni mikwara ya kijinga tu" lakini kwa mtu ambaye hiyo ndiyo IMANI yake kabisa kabisa haionekani hivyo. Kwake yeye sitiari hiyo inachoma, kumwogofya na kumtetemesha. Kwake ni ukweli dhahiri!

Kamala, mimi sina sifa hata moja kati ya hizi ulizonipa. Mimi si "padri, mchungaji, mjua kweli pekee, mwoga wa moto, nk." na sijui umetumia vigezo gani kunipa vyeo vyote hivi. Duh, hapa umenichekesha kweli! Kama nafsi, hulka ma misimamo yangu haijajionyesha katika blogu yangu basi pengine itajionyesha zaidi siku za mbele. Mimi hata sijakifia kilele cha utu na kujitambua kama ulivyo wewe na naamini kwamba daima nitakuwa mwanafunzi hapa duniani. Ndiyo maana natembelea blogu yako kila siku ili kujifunza. Mimi pia si mlokole, mtakatifu, padri wala nani. Mimi ni mimi na nakuomba unielewe hivyo. Siku nikija Bongo nitakutafuta unifundishe ku-meditate. Nitafurahi sana nami nikijitambua kama wewe!

"...mbona hujibu swali langu juu ya kwa nini wahubiri mjihusishe na maisha ya watenda zambi? unafikiri bila watenda dhambi kuna mahubiri?"

Mimi si mhubiri lakini nitawasaidia wahubiri hapa. Sababu ile ile inayokufanya wewe uhahe huko na huko kueneza mawazo yako ya kujitambua, mara leo kanda ya ziwa, mara wapi - ndiyo sababu hiyo hiyo inayowafanya wahubiri wahangaike kuwaambia watu kuhusu siku ya kulia na kusaga meno. Kwa sababu ni IMANI yao na wanaamini kwamba huo ni wajibu wao. Wao wameagizwa hivi "...nendeni mkaitangaze na kuieneza injili kwa mataifa yote, mkiwafundisha na kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wangu..." Kama wewe unavyoamini kwamba elimu ya kujitambua ndiyo suluhisho na ufunguo wa mambo yote, wao pia wanaamini kwamba Yesu wanayemhubiri ndiye ufunguo na suluhisho la mambo yote. Sijui kama mambo ya Utambuzi na Yesu vinapingana au ni mafunzo yenye misingi ile ile.

"...niwaache wanaomwamini Yesu, una uhakika gani kama simwamini? mbona nameditate wakati na yesu alikuwa meditator mzuri? mbona siri vyakula vizuiwavyo na bible?"

Sidhani kama mtu anayemwamini Yesu anaweza kusema kwamba "...kulia na kusaga meno ni mikwara tu ya kijinga" na sababu ulizozitoa hapa sidhani kama zina uhusiano wo wote na kumwamini Yesu. Nijualo ni kwamba kumwamini Yesu ni swala la kibinafsi na mimi sina haki, wajibu wala uwezo wa kujua jambo hili.

Napenda nimalizie kwa KUOMBA MSAMAHA kama nilisikika vibaya katika comment yangu ya kwanza na natumaini ufafanuzi huu umesaidia. Na napenda nirudie kauli yangu niliyoanza nayo hapa. MASUALA YA IMANI NI MAGUMU. IMANI - Imani inayomfanya mtu ajifunge mabomu na kwenda kujiripua akiamini kwamba kwa kufanya hivyo anakwenda kwenye raha, imani inayomfanya mtu auze kila kitu alichonacho na kumpa Askofu Kakobe, Imani inayomfanya mtu apone kansa ambayo madaktari walikuwa wameikatia tamaa, IMANI...

Wigwa Mwanawane?

Chacha Wambura said...

Masangu, Nene najaga mashimbe mpaka mjadala uishe, au vipi?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Chacha;
Wajaga mashimbe? Tunakuhitaji katika majadala. Tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwenu watu wa utambuzi. Shokaga wanguwangu!

chib said...

vibogoyo watasaga fizi zao!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

makande, Nzuzu,bitondo tondo,bibalabala. ginehe, nahena, molahadhuhu, wabeja, gukaya....

naandika komenti hii nikiwa kwenu katikati ya jiji niikishuhudia ziwa na meli za kwenda kwetu.

duh sijui nianzie wapi maana hizisafari unazozihita 'kuhaha' zina starehe yake na changamtoto pia. kama mimi nahaha huku ukuryani na usukumani sijui walioko utumwani 'misiri ya mbali' tuseme wanafanya nini!!!
unawatetea walokole wakemeao harafu unasema hujui na huna fani ya kukemea??

maswala ya imani hayajawahi kuwa magumu tatizo lenu mnayaangalia kwa kutumia akili huku mkichokozeka kihisia badala ya kuyaona kiroho ili muuone ukweli mpana badala ya vitu vidogo

juu ya kusaga meno chib kakujibu. wewe utasagaje meno? kwanini Mungu anasagisha watu meno? huyo siye Mungu ni kichaa mwenye roho mbaya. Mungu anapenda tu wala hasagishi meno kwa nini tuwatishie watu juu ya Mungu? kwa nini mkitoa sadaka mnamtolea Mungu wakati mkispendi ni za kwenu?

tatizo la kukana vyeo hivyo ni kwa sababu hujavisomea lakini ukiaza kutoa 'dogma' basi ndo mmoja wao. swala la kujifunza utambuzi ni sawa. lakini kumbuka maarifa ya utambuzi yalianzia India na kusambaa sana marekani na mkondo nilioupitia ulitokea marekani. nakushauri utafiti na kujua huko huko. fungua osho.com, eckharttolle.com nk uanzie hapo. ukitoka marekani na kuja kufundishwa, nitakuchaji hela tena nyingi makusudi kwa sababu umeacha bahari ukaja kuogelea kwenye dimbwi

juu ya wetenda dhambi labda utufafanulie dhambi nini na mtenda dhambi anafananaje na kwanini wewe sio mtenda dhambi!

nikujuze tu kuwa mimi 'sihahi' kueneza mawazo ya utambuzi kwani kwanza utambuzi sio mawazo yangu bali ni uhalisia. pia niko kwenye kazi zangu nyingine na utambuzi unafanyika tu na sio lengo kuu la safari zangu ndugu. ukitaka kujua nafanya nini uliza uambiwe.

mimi kamwe siamini na hili nimelisema nashangaa kwa nini unaniaminisha utambuzi. mimi nautenda utambuzi wala siuamini!!!

ndio, kulia na kusaga meno ni mikwara ya kijinga kwani mateso yoote yesu aliyshayateseka kwaajili yenu na aliwaonyesha kuwa sisi ni zaidi ya mwili na kusema usimwogope auaye mwili na kusema kuwa sisi ni zaidi ya mwili na hatuwezi kuteseka wala kufa na ndio maana akawashangaa na kuwaombea huruma waliodhani wanamtesa na kumuua kwani sisi ni zaidi ya mwili hatuwezi kuteswa wala kuuwawa japo twaweza kuuacha mwili na kuvaa mwinngine au ku-merge into an ocean of life

tatizom la wasomi nikunukuu kwa kuwa nimesema kusaga meni ni mkwara. kwangu mimi naweza kukushauri usizingatie saana ninachokisema bali ninachokitenda na sio kama msemavyo kanisani!!!!

hujasikika vibaya kwani ndivyo uongeavyo na mimi siamini katiak ubaya.

ni vigumu kuendeleza mijadala kama hii kwani nasafiri na kufanya kazi za nje ya ofisi. inapendeza lakini pia muache kujadili kibubusa zaidi.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mulangira Kamala;

Nimekupata. Nakutakia safari njema. Wape salamu zao huko uliko. Natamani sana siku moja kurudi Bukoba na kupaona tena Kahororo. Ukirudi tunaweza kuendeleza tena mjadala huu wa "kibubusa". Asante

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

haya mukunurwa Omulangira waKisukuma

Anonymous said...

Nyie mnaojaribu kufanya discussion na Kamala mnapoteza muda wenu bure. Huwezi kufanya discussion na mtu asiyejali ideas na ideals za wengine. He doesn't care about your views, life experiences, life philosophy etc. As long as hujui hii DOGMA yake ya kujitambua basi utaishia kutukanwa, kubezwa na kudharauliwa. Angalia comments zake anywhere on the blog world. It is all about this stupidity thing called kujitambua (the same thing that is preached by the SCIENTOLOGY cult), "teaching" people how to be rich while himself is poor (although he will claim that in kujitambua sense he is rich). Hata utoe points na hoja namna gani as long as siyo mtu wa kujitambua you will be treated as a stupid person. So people don't waste your time trying to argue with a person who thinks he knows everything (in essence a STUPID person) because you may also end up looking even more stupid! Tchao!

chib said...

Anony, Duh!!