Tuesday, August 25, 2009

Musoma kwa ajili ya utambuzi.

mnyanchoka

tumefika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya utambuzi. sasa niko mjini musoma Katika ofisi za Foundation help itakapofanyikia semina ya utambuzi mchana huu.

niliwasili mjini msoma usiku wa kuamkia leo mida ya saa sita na nusu nikitokea jijini Dar kwa basi la Mohammed trans. kwakweli nashukuru sana oungozi wa basi hili kwani huduma zao ni nzuuri sana na magari yao yametulia. safari ilipendeza na tulifika salama.

ndani ya basi,karibu na nilipokaa, alikaa mmama ana watoto watatu. ilipokuwa jioni watoto wakataka kulala na mmoja ikabidi aje kwangu kwani nilipokaa kulikuwako na kiti kisichokuwa na mtu. basi katoto kalisinzia kwa shida kwani basi linaruka bumps, ilibidi nikapakate kalale vyema, nilifurahi kuwa mlezi.

mji wa musoma ni mwema, unapendeza. uko karibu na ziwa victoria una miinuko kibao na hali ya hewa n nzuri. ni furaha kumeditate ukiwa mjini hapa

chakula ni kizuri pia na haswa vegeterian diet. sukuru Mungu sijakutana na Wanyanchori wala Wanyanchoka isipokuwa Chacha Wambura marwa!! ambaye hatambei na panga, rungu wala Mkuki.

nawakaribisheni katika semina hii. Kesho itakuwa ni jijini Mwanza

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ninanukuu "ndani ya basi,karibu na nilipokaa, alikaa mmama ana watoto watatu. ilipokuwa jioni watoto wakataka kulala na mmoja ikabidi aje kwangu kwani nilipokaa kulikuwako na kiti kisichokuwa na mtu. basi katoto kalisinzia kwa shida kwani basi linaruka bumps, ilibidi nikapakate kalale vyema, nilifurahi kuwa mlezi." mwisho wa kunukuu. Nimefurahi sana usemi huu naamini kama hujawa baba basi utakuwa baba mwema. Na pia nakutakia muda mzuri huku Musoma na pia nashukukuru Mungu umesafiri salama. Upendo daima.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante saaaana dada Yasinta