Sunday, August 23, 2009

ni semina za Utambuzi kanda ya ziwa

Ile semina ya utambuzi inayopaswa kufanyika jijini Mwanza kama kiwakilishi cha kanda ya ziwa sasa itafanyika Musoma, Geita na shinyanga pia.

jumaane ya tarehe 25/08/2009 kuanzia saa kumi jioni semina ya jitambue itafanyika kati kati ya mji wa Musoma, mahala atakapopanga Chacha Wambura.

kwa wanaopanga kuhudhuria Semina hiyo wawasiliane na Bwana Wambura kwa simu namba; 0713 235146 au 0787 945414 ili kujiandikisha na kujua mahala itakapofanyika semina hiyo.

na Jijini Mwanza tutakuwepo siku ya Jumatano tarehe 26/8/2009. Siku itakayofuata yaani Alhamis, tutakutana katika hotel ya Impala na kujaadili juu ya Mungu na Santmat meditation wakati siku ya ijumaa tutaendelea semina ya utambuzi.

kwa walioko mwanza pia wasiliana na Chacha Wambura kwa namba hizo pale juu au piga 0754 771 601 wale wasioweza kuhudhuria kwa muda uliopangwa waweza kukutana kwa muda maalumu kwa kupanga na watoa mada.

Geita na Shinyanga, tuwasiliane kwani maandalizi ya huko bado yapo jikoni

karibuni tujifuze, karibuni tukue

........ kwaniaba ya familia ya jitambue (FAJI)
Dar es salaam

4 comments:

SIMON KITURURU said...

Hapa ndio najilaumu kwa nini sina utaalamu wa kupaa na ungo maana nisingekosa kuhudhuria hizi semina:-(

Chacha Wambura said...

Mtakatifu saana Simon (sina hakika na hilo kwani yawezekana ni Mtakavitu!!), kwani na wewe ni wa kanda ya ziwa? kama ndiyo tukutumie ungo, si unajua tena mambo fulani ya kanda ya ziwa?

huku ndo kule ukifika kama umetundika ugimbi wako macho yashabadilika na kuwa mekundu basi ushaingia katika list ya kucharangwa mapanga!!!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana Kamala kwa kutujuza hili. Ni kweli bahati mbaya wengine tupo mbali.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

inapendeza. mzee kitururu kazi ipo.

Yasinta, siku inakuja ambayo mafundisho haya yatakuwa yakipatikana hata kwenye internet na haitakuwa lazima kuja hapa.