Monday, August 17, 2009

semina ya utambuzi jijini Mwanza!

tangazo hili linatoka kwa Afisa program wa familia ya jitambue.........kutakuwepo na semina ya utambuzi jijini mwanza kwa muda wa karibia juma zima kuanzia siku ya jumanee tarehe 24/8/2009. semina itakuwa iikifanyika mida tofauti kufuatana na upatikanaji wa nafasi wa washiriki na mahali pa kufanyika semina hiiyo patajulishwa baadaye.

yatakayojadiliwa ni pamoja na:


Namna ya kupata utajiri pamoja na mafanikio katika biashara, kiuchumi, kazini na shuleni; namna ya kujenga mahusiano mema kazini na upendo wa kweli katika ndoa, suluhu ya tendo la ndoa; namna ya kujiamini; kuondoa msongo wa mawazo, chuki, kijicho na hasira za ziada; kinga ya uchawi; namna ya kupata chochote utakacho maishani; kuondoa tabia sugu kama ulevi, uvutaji sigara n.k., kuondoa hofu na aibu, kupata afya nzuri kimwili kwa njia ya tiba mbadala, kufikiri vizuri, n.k.

wale wote watakaoweza kushiriki semina hii wawasiliane kwa kupiga simu namba, 0754 771 601, email; utambuzi1@yahoo.com au utambuzi1@gmail.com

hakuna kiingilio maalumu japo inaruhusiwa kutuoa mchango kwa watakaojisikia.

ahasanteni sana na karibuni wakazi wote wa Mwanza na vitongoji vyake.
Ahsanteni.

imetolewa na afisa program,

FAMILIA YA JITAMBUE (FAJI)

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mada nzuri. Usichoke kuwa unatumegea mara moja moja hapa bloguni. Kama hiyo mada ya kinga ya uchawi itawafaa sana Wasukuma kwani kwa kuamini uchawi na kucharangana mapanga wakishutumiana kurogana ndiyo wenyewe.

chib said...

Michango muhimu bwana, lazima upigie kadebe watu wachangie

Chacha Wambura said...

mie ntataka kujifunza uchawi...sio namna ya kujikinga bali namna ya kuwaloga wanyanchori na wananchoka waache kucharangana mapanga huko tarime.

halafu nikishaweza niwaloge wanawake wa kikurya waache maneno/mawazo yao ya kuwa mwanamke kupigwa ni sunna na kwamba wasipom-kong'oli basi hapendwi!!!!

Sijui Da Koero na Yasintha wanawezaje kuliongelea hilo labaadhi ya wamama kupenda kukong'oliwa!!!!