Tuesday, August 11, 2009

shairi la Mtanga


nimeamua kulitundika ili tulipitie tena.....
Nashika kalamu yangu, salamu nazituma,Kwenu marafiki zangu, natumai mu wazima,Nawaombea kwa Mungu, mjaliwe yalo mema, Salamu wanablog.Simon Kitururu, huzamia MAWAZONI,Fikra zake ni huru, pia zina burudani,Nasi tunamshukuru, hachoki tangu zamani,Salamu wanablog.Yupo dadetu Yasinta, yeye hupenda MAISHA,Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,Sifa tele azipata, maana huelimisha,Salamu wanablog.Christian Bwaya yupo, hutaka tuJIELEWE,Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,Ukweli daima upo, muhimu ujadiliwe,Salamu wanablog.Mubelwa Bandio pia, MZEE WA CHANGAMOTO,Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,Muziki hutupatia, yenye midundo mizito,Salamu wanablog.Subi dada yetu sote, wa NUKTA SABA SABA,Ili mengi tuyapate, blog yake yashiba,Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,Salamu wanablog.Chib naye ni rafiki, hutumia HADUBINI,Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,Magharibi mashariki, hutujuza kulikoni,Salamu wanablog.MWANAMALENGA Kissima, hutuonesha MWANGAZA,Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,Kwa ushairi ni vema, tungo zake zapendeza,Salamu wanablog.Serina Serina huyo, ana UPANDE MWINGINE,Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,Salamu wanablog.Koero Mkundi pia, hutuambia VUKANI,Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,Daima hukumbushia, tutoke usingizini,Salamu wanablog.Ndugu yetu Mumyhery, kabobea kwa MAVAZI,Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,Salamu wanablog.Kamala tunamjua, wa nyegerage KIJIWENI,Fikra apambanua, ili tutoke kizani,Sote tukajitambua, tujijue kina nani,Salamu wanablog.Masangu wa Nzunzullima, CHAKULA chake KITAMU,Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,Salamu wanablog.Markus Mpangala, KARIBUNI sana NYASA,Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,Salamu wanablog.Lumadede mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,Salamu wanablog.Na MWANASOSHOLOJIA, siachi kumsifia,Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,Salamu wanablog.Nami MWANANCHI MIMI, wa DIWANI YA FADHILI,Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,Salamu wanablog.Ambao sijawataja, lipo shairi jingine,Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,Salamu wanablog.

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana kaka.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante pia bwana mtanga. shairi hili linazaa tafakuri nyingi mno na linaifikirisha sana.

samahani kwa kulitundika kienyeji mno