Wednesday, August 19, 2009

Tunahitaji viongozi waliojitambua.

Ni wakati mwingine sasa unaokaribia wa kuchagua viongozi wapya wa kutuongoza kisiasa. Mengi yamekuwa yakisemwa na yakijadiliwa juu ya sifa za kiongozi na uongozi kwa ujumla. Wapo wanaolalamikia viongozi na baadhi ya walalamikaji wakipata nafasi za kuongoza wakati mwingine hufanya manyanga labda kuliko yale ya waliokuwa wakiwalalamikia.

Wakati huo tunapoelekea na kujiandaa kuchagua viongozi wapya wa karibia ngazi zote, ni vyema tukaangalia, tukatafiti na kujiuliza tunahitaji kuongozwa na mtu wa namna gani na aina gani. Tunahitaji kuongozwa na watu waliojitambua kwa ungozi endeleva na wenye tija na sio kuongozwa tu kwa sababu kuna nafasi za kuongozwa na wala sio kuwa na wagombea eti kwa sababu kuna nafasi za kugombea kama ilivyo kuwaida yetu sasa.

Ni wakati wa mabadiliko, ni wakati wa kujitafiti kwanza kabla ya kusimama na kutaka kuongoza wengine. Je, ni kweli sisi tunaoogombea nafasi za uongozi, tuna sifa hizo kweli za kuwaongoza wengine? Kwa nini tunataka kuongoza? Je sisi tunaowania nafasi hizo, tunaweza kujiongoza sisi wenyewe kwa ufasaha makini?

Kujitambua na kuongozwa na viongozi waliojitambua ni jambo muhimu sana . Tunahitaji kiongozi anayetambua kuwa yeye kama binadamu, hapa duniani anapita tu na muda wa kukaa hapa ni mfupi na hivyo tunahitwa kutenda mema sio kujilimbikizia mali . Tunahaitaji kiongozi anayejitambua na kujua mazingira yake. Kiongozi ni lazima ajidhibiti kimwili, kiakili, kihisia na hivyo kukua kiroho.

Tunahitaji kiongozi atakayeweza kuona umoja wetu kama binadamu na sio kubaguana kwa misingi ya ukabila, rangi wala taifa. Tunahitaji kuwa na kiongozi aliyekua (evolve) ni hivyo kuwa juu ya dini ili azimiliki na kuzitawala zote badala ya kiongozi anayetawaliwa kwa kudhibitiwa na dini moja tu ili aone ukweli mpana kuwa lengo la dini zote ni moja.

Tunahaitaji kiongozi mwenye upendo anayetambua umuhimu wa kuwapenda watanzania wote na kusimamia ugawanaji wa rasilimali zote kwa ajili ya wote badala ya kujilimbikiza yeye na familia yake. Ni kiongozi atakayeona utu, umoja na amani kuwa muhimu kuliko vinginevyo vyote. Ni kiongozi atakayeweza kusisitiza na kupanga mikakati yenye lengo la kunufaisha wananchi waliowengi badala ya kujitengenezea tenipasenti yake.

Kiongozi bora ni yule anayekula chakula bora kwa ajili ya afya bora badala ya yule anayekula kwa hisia za kusaka radha ya mdomoni idumuyo kwa sekunde mbili huku akijaza tumbo na kulipa kazi ngumu ya kubeba mzigo usiohitajika na kulemewa huku akikabiliwa na afya mbovu itaanayo na kula hovyo.

Tunahitaji kiongozi atakayeona utumwa uliomo katika kuongoza watu badala ya ukuu usiokuwa ukuu wa maana. Kiongozi mwenye kuingia katika uongozi akiwa amebeba malengo ya kwelli ambayo kwa nia na moyo waka anaamua kuyatetea, kuyaamini na kuyafanyia kazi na sio kiongozi wa kuandaa propaganda za kudanganya wapiga kura ili wampatia ulaji. Kiongozi anayeishi miongoni mwa jamii anayoiongozi na sio mkazi wa ‘mujini’

Je! Kiongozi huyo atatoka wapi?

Bila shaka ni miongoni mwa jamii yetu. Jamii ya wapigakura wetu inapaswa kujitambua, kuwa na malengo na kumtambua yule atakayeweza kweli kuwafikisha katika malengo yao . Jamii hiyo ya wapigakura haitasubili hata siku moja waje wale wajanja wa kujua kuchonga maneno na kujifanya wanajua shida na mahitaji ya wananchi hivyo wawachague ili waishi kwa ahadi na ndoto za mchana, bali jamii hii itawatafuta wale inaoamini kuwa ni bora na kuwaomba kwa njia yoyote hata kama hawataki kuwa wawe viongozi wao.

Jamii itatambua kuwa viongozi wa kweli huwa hawapendi kuongoza na hivyo itajua umuhimu wa kuwaomba na kuwasihi wafanye kazi hiyo. Jamii iliyojitambua kiasi cha kuweza kuwa pamoja na kujua nani wa kuwaongoza, haitakuja tu, bali itatokana na vyombo vya habari makini. Si vyombo vya habari vya kuandika habari za kushutusha kutishiana bali vinavyoandika habari kwa lengo la kaelimisha, kuhamasisha na kuwaonesha wananchi umuhimu na nafasi yao katika kutatua yanayoitatiza.

Mwisho wa siku tutapata uongozi wa maana, wa kueleweka, uliowa kwetu na wakutufaa. Vinginevyo tutaendelea kuwapigia kura watalii katika majimbo yetu na nchi yetu, watakaokuwa wanasimamia na kutunga sera za elimu huku wakisomesha watoto wao ughaibuni, tutaendelea kuwachagua wachoyo wasiojua wanacho kihitaji na hivyo kujikusanyia kila wakionacho machoni pao. Tutaendelea kuwachagua wanafiki wanaoona makosa ya wenzao huku wao wakipata nafaasi hushindwa kuyaona yale waliyoyaona walipokuwa nje ya uongozi


3 comments:

Chacha Wambura said...

KL, aksante kwa manifesto hii. Nadhani ntaitumia kugombea urais mwakani japo sijajua wapi itapata pesa ya takrima ya kuwapa 'wenzetu'.

hii ni nzuri kuzidi ya waraka wa wakatoliki, au sivo?

halafu hicho chakula ukisemacho ni chakula gani, cha uzima?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

cha ufu

Chacha Wambura said...

halafu wewe ushajitambua. unaonaje ukichukua fomu ya kugombea?