Wednesday, September 23, 2009

from rwanda with lessons part I

nimeipenda post hii na kuikopy kama ilivyo kutoka kwa michuzi na kuileta hapa ili wengi tuipitie labda katika siasa kuna cha kujifunza
Wiki chache zilizopita niliahidi ku-share na blog hii ya jamii mambo machache niliyoyaona Rwanda. Nilimepata msukumo zaidi kutokana na historia ya Rwanda, kwani mwaka 1994 mauaji ya kimbari yalisababisha mauaji ya watu wengi sana, inakisiwa zaidi ya watu 500,000.
Matokeo ya mauaji ya kimbari yaliongeza chuki zaidi kati ya Wahutu na Watutsi. Katika hali ya kawaida, wengi tungetegemea Rwanda ingesuasua na ingedidimia zaidi. Lakini ukienda Rwanda utaona maendeleo makubwa mno; wafanyakazi kuanza kazi saa moja asubuhi, ujenzi, barabara nzuri nk.
Badala ya kuona na kukaa kimya au kuanza kulalamika nimeonelea ni busara kuandika na kushare huku nikitarajia tutaweza kujifunza kwa majirani, ambao kasi yao wengine wanasema wameshatuacha au watatuacha mbali.Haya ni machache; Uongozi bora, Uthubutu wa Wanyarwanda, Usafi na utii wa Sheria, Nyumbani ni Nyumbani na Mipango miji.
Uongozi bora:
Uongozi bora wa Rais Paul Kagame umechangia kwa kiasi kikubwa sana kuifikisha Rwanda hapa ilipo. Wiki iliyopita Rwanda imetajwa na ripoti ya Benki ya dunia kama nchi iliyoboresha zaidi mazingira ya uwekezaji. Tofauti kubwa na nchi nyingi za kiafrika, Mawaziri wanaendesha magari na tena sio mashangingi kama TZ.
Tulishuhudia Rais Kagame mwenyewe akiendesha gari !. Ikiwa Rais anaonyesha mfano mara nyingi viongozi wengine watafata. Kagame amesimamia utawala bora, ukiwa Rwanda na ukafanya kosa hakuna cha wewe nani, jamaa hawapokei rushwa!. Jarida la TIME lilimtaja Rais Paul Kagame kati ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Najua kwa kutambua uwezo wa Kagame, Tony Blair hakusita kuwa mshauri wake binafsi!.
Uthubutu wa Wanyarwanda:
Tukifuata historia Wanyarwanda huzungumza kinyarwanda na kifaransa. Hili sasa limebadilika Wanyarwanda wanazungumza kiingereza na Kiswahili vizuri!. Kwa wale wafuatiliaji wa BBC idhaa ya kiwahili, siku chache zilizopita ilizungumzia uanzishwaji wa ufundishaji wa Kichina kwenye chuo kikuu cha Kigali!.  Tayari wanafunzi wengi wanasoma na wanaongea Kichina, hii ni ishara tosha ya uthubutu wa Wanyarwanda, wanatambua umuhimu wa kujifunza lugha nyingine muhimu. Jambo kuu zaidi ni Warwanda kuyapa kisogo yaliyotokea na kuangalia mbele. Dereva wa texi aliyeniendesha alipoteza wanafamilia wote kwenye mauaji yale, lakini anaangalia mbele.


Usafi na Utii wa sheria:
Jambo la kwanza kugundua ufikapo Rwanda ni usafi wa hali ya juu wa jiji la Kigali. Hairuhusiwi kutupa takataka ovyo bali sehemu maalum zilizotengwa. Kusisitiza suala la usafi kila Jumamosi ya mwisho ya mwenzi ni siku ya usafi kila mtu anashiriki katika kufanya kazi za usafi, hili pamoja na sheria zimefanya tabia ya usafi ijengeke. Sheria za usalama barabarani ni msumeno, kila anaendesha pikipiki ni lazima avae kofia pamoja na abiria. Waendesha pikipiki za kukodi wana namba na mavazi maalum ya kazi, hili linafanya kutambulika kwa rahisi. Usalama wa Rwanda ni jambo jingine ambalo ni thahiri, hapa napata swali lisilo na jibu; polisi huwianisha uhalifu wa silaha na nchi zenye au zilizokuwa na machafuko. Iweje Rwanda iliyotoka kwenye machafuko, iko jiranio zaidi na nchi zenye machafuko hadi leo za Burundi na Congo iwe salama hadi mabenki yanafungwa saa nne usiku!.

From Rwanda with lessons – Part II itafuata.
Mdau IK.

5 comments:

Chacha Wambura said...

Sasa washangaa nini? Tatizo si unalijua?

Ni kweli kuna mafunzo mengi katika masuala yaliyojionesha hapo kwenye hiyo post. Kuhusu ulinzi, mtakumbuka kuwa siku si nyingi tulikuwa na mfumo mzuuri sana ambao ulitusaidia kabisa kuhimili matatizo haya ya ujambazi. Mtu alikuwa akihama ama kusafiri anasafiri na barua ya kumtambulisha ambayo huiwakilisha kwa viongozi wa kijamii wakati ule siasa haijaingiwa na unyang'au na ilijulikana huyo mgeni anakaa muda gani na ni sababu gani zimemleta hapo. na kama alihitaji makazi barua ilimtambulisha juu ya tabia yake.

siku hizi ng'wanawane, ni pesa yako tu unapata shamba na ardhi kedekede bila kujali hiyo pesa umeipata kwa kuuwa albino huko kahama (kama hujapatwa na mkono wa sheria kama hawa wa leo hii walohukumiwa KIFO).

Mimi nadhani ni kuwa hatujathubutu kwa kutumia kafalsafa ka kijinga ka babu yake KL kuwa 'SABABU, NIA NA UWEZO' upo wa kuweza kutekeleza hayo yote mloyataja katika hiyo post.

nimeangalia kipindi cha UCHUMI ktk TBC1 ambapo mpewa heshima maria nagu alikuwa na-justify kwa nini tunahitaji FDI nkabaki mdomo wazi(siyo kwamba nili-salivate, no!). Nika-refer kwa report ya Global Gold (www.gold.org) kwamba dhahabu imeleta uahuweni wa maisha kwa jamii zinazozunguka migodi, toba!!!

presha ikaanza kupanda na kushuka!!!

Bandugu bapendwa, nimechoka kwani nami nilijionea hayo alojionea huyo mjamii nilipotembelea huko miaka miwili ilopita.

urakozya...senkyuuuu!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Makala nzuri. Tunayo mengi ya kujifunza na kusema kweli kwa nchi kama Tanzania ambayo ina kila kitu - HATUNA KISINGIZIO cha kutopiga hatua kimaendeleo. Rafiki yangu pia alinieleza tofauti aliyoiona kule Botswana - kanchi kadogo kaliko jangwani kanakotegemea almasi na ng'ombe. Sijui kama viongozi wetu wanasoma makala hizi, na wanapotembelea nchi kama Rwanda na Botswana hawapatwi na ule wivu mzuri wa kimaendeleo?

By the way Kamala - umetembelea hapa - http://matondo.blogspot.com/2009/09/kumekucha-kamala-lutanisibwa.html?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep. tunahitaji utafiti mpya bwana Wambura katika hili.

matondo ndio nimepatembelea

Chacha Wambura said...

KL, hatuhitaji utafiti bali vitendo na nyie mnaoona mambo hayendi ama yanaenda ndivo sivo ingieni katika vyombo vya maamuzi kama bunge na halmashauri. Kamala ukigombea udiwani mimi ntakuwa campaign manager wako ila kama huna mlungula tutapikika chungu kiloja.

Koero Mkundi said...

Ni kweli kaka Chacha Wambura kinachohitajika ni vitendo, tukisema tufanye utafiti, mafisadi watatumia fursa hiyo kujichotea mabilioni ya fedha kwa kisingizio cha gharama za utafiti....

Kaka Matondo na wewe nakubaliana na rai yako.