Monday, September 7, 2009

Jangwa la sahara kuwa kijani,

soma ndoto hiyo nimeitoa sehemu..........


Jangwa la Sahara kuwa kijani
Hayuma si tukifundishwa shule kuwa zamani duniani mabara (continents) zilikuwa yameungana, watu hata wanyama walikuwa wanazurura toka eneo moja kwenda kwingine. Yalipotengana mabara kutokana na erosion na mabadiliko ya hali ya hewa na maeneo mengine kubaki visiwa bahari nazo zikamegwa na kuwa na mikondo ya ukali wa aina tofauti.
Wanyama wa maeneo yalikuwa visiwa walibaki katika hali yao ya asili hawakuweza kuvuka maji na hawakuweza kuchanganyika. Na tunaambiwa kuna eneo kama serengeti USA kasoro wanyama. Hao waliobaki visiwani wanaonekana wa ajabu ya pembe ndefu, manundu ya ajabu au vipi kumbe ana jamaa yake katika bara kubwa. Hivyo ndege, kama kasuku, nyani, kobe, popo, nyumbu wa Kisiwani hasa wale wasioweza mfano kuruka angani akachanganyika kwa kuzaana na wa bara anakuwa wa ajabu kuliko wa bara. Hata Tembo wa zamani pembe yake ni mzigo mkubwa wa ajabu kuliko wa sasa aliyepitia mabadiliko makubwa ya hali ya hewa na adaptation. Naye kutokana na kung'olewa meno yake na majangili anaweza sasa akaanza kuzaa watoto wasio na meno (pembe) ikabidi abadili na hata mfumo wake wa kula na kuangusha miti akanza kukimbiza na kula watu. Hata ng'ombe mwitu ana jamii yake ambaye anafugwa. Si unajua pia tulianza kuchagua hata mazao na matunda tuliyoyapenda tukaanza kuyapanda na wanyama pori wapole waliokuwa wanatufuata wakati tukiwa hunters and gatherers tukawafuga ili tuwe nao karibu kwa nyama ndio tunao sasa. Na bado tunaendelea kuchanganya na kuwazalisha kwa mchanganyo kupata viumbe bora zahidi. Hata mimea sasa tunachanganya maabara kupata bora, ya muda mfupi inayozaa sana badala na mtama au mahindi ya kuzaa miezi 3; sasa tuazalisha mmea bora wa ndizi kwa chupa. Hata binadamu sasa technologia yake ya kusalisha imeendelea na hata kuzalisha kwa michanganyo ya mbegu tatu ili kuondoa maradhi ya kurithi. Na wale watu weusi tunaowaona mabara mengine ila wana nywele tofauti labda tulizaana nao huko karne bara lilipokuwa moja. Na ndi maana wakati wa baridi Ulaya baadhi ya ndege wa kuruka masafa marefu huja Tanzania katika baadhi ya mbuga zetu kuzaa huku na kurudi kwao na watoto wao baada ya baridi (winter) kuisha kwao.
Kwa kuchangia zaidi. Isimani Iringa inaonekana kulikuwa na Bwawa la maji kubwa zamani karne za miaka mingi iliopita na huwezi kuamini kama lilikuwepo na pamehifadhiwa kama mahala pa historia. Lakini Ishara ya bwawa hilo kubwa ni kuwepo kwa mifupa ya tembo, mamba, viboko (hippos) na silaha za mawe zilizokutwa hapo ikionyesha hunters & gatherers walikuwa wanafika hapo kuwinda nyama pori na kujichana samaki pia. Na tunaambiwa kuwa 'Bustani ya Eden' ambako adamu na hawa waliishi na kula matunda matamu kila kitu kilikuwepo na kulikuwa evergreen ili kuwa 'IRAQ' mbona sasa ni Jangwa, na Mfalme Nebukarnezer na masananu yake hakuwa huko? Na watu wakihama kukimbia ukame na jangwa bara la sasa la Afrika katika karne hizo wakiondoka toka Misri kuelekea kipande ingine. Na Misri wakagundua 'shaduf' ya kumwagia maji mashambani ili kupambana na ukame. Ninafikiri kuna masomo mengi ya sayansi shuleni yanayosaidia mtu kupanda hali ya ulimwengu huko nyuma ilikuwaje ni pamoja sayansi ya mawe, viumbe, hali ya hewa, Island Bio-geography etc wataalamu wanajua hayo na ndio maana mtu anatakiwa asome akiweka specialisation fulani. Hakuna mtu anayeweza kuwa mtaalamu wa sekta zote. sekta au field ambayo si yako inakuwa kama usiku wa giza katika mambo kama haya unayotuambia.


No comments: