Wednesday, September 9, 2009

kuongeza Nywere na makalio, wazdhungu kuota jua


katika post moja wapo hapa kijiweni, tulizungumzia juu ya wadhungu kupenda uafrika na waafrika kupenda udhungu. chib aliongelea juu ya wadhungu kujianika juani wawe kama weusi, na weusi kujiharibu ili wawe kama wadhungu na kutumia manyoya ya paka ili nywere zao ´zidhunguke´

Chacha wambura akaongelea mikongóto ya wanawake watakaomsikiliza yule dada mwenye Suruali mbanano na Yasinta akasikitishwa na utamaduni wetu kufa. anyway tukasikia magazetini kuwa mke wa kigogo mmmoja yuko hatarini kwa matako yake a.k.a makalio kupinda pinda hovyo.

yote kwa yote. sijui niite nini. ni ile ile kijana wa changamoto aitayo kujipoteza katika kujitafuta. wadhungu wanapojaribu kufanana na waafrika hawajipotezi, bali wanajipata vizuri tu. wanasuka nywere na kumbuka kusuka hakuna soo yoyote ile zaidi ya kuuwaepusha na makemikali vichwani mwao.

kujianika juani ni faida kwa kila afanyaye hivyo japo wengine huwa tunalikimbia na kuliona linatutia nuksi. niliwahi kuandika makala juu ya uhusiano wa karibu kati ya jua naMungu a.k.a muumbaji a.k.a nguvu kuu. wadhungu kule kwao hawalioni jua. na labda baridi ndio inayowafanya kuwa weupe vile. kuupata weusi ni dili kwani ni rahisi tu, ni kwa kujianika juani. lakini weupe sio dili kwani lazima hujiaribu na kujiingiza matatizoni ili uupate weupe.

na labda ngozi nyeusi ndio dili kwani inajidhihirisha jinsirangi hii isivyobadilika kufuatana na hali ya hewa bali iko vile vile, kwa kiingereza ni constant. lakini nyeupe inabadilika usiku, asubuhi, mchana nk.

kuhusu wadhungu kujianika juani, kumbuka jua ni kani (force) kuu ya asili (great force of nature) kwa wanaojitafuta na kujigundua katika tahajudi (meditation) wanaweza kutwambia nguvu waipatayo kwa kuliangalia jua au kutahajudi wakiwa juani. mchunguze mdhungu au mtu yeyote mwenye tabia za kujianika juani, utaugumdua faida lukuki. hana msongo wa mawazo wala visasi vya hapa na pale. anafuruha na anafanya kazi kwa bidii kwani akili yake huwa freshi. hatulitumii jua ipasavyo kwani hatujui umuhimu wake!

kwa hiyo basi, wajinga na wasiojijua ndo hutumia vitu vya ajabu ili waonekane namna gani vipi. wanapenda udhungu, ni noma wanavaa mawigi na manyoya ya waliokufa. wanakula sumu ili wanenepesha matako yao. sijui kama wanamkosoa muumba ua vipi.

mbaya zaidi ni kwamba hawajifunzi kutoka kwa waliowatangulia. jijini dar kuwa mfano, kuna wamama kibao wameungua nyuso na ngozi. ukiwaangalia ni kama wamechanganyikiwa au akili zao hazifanyi kazi vizuri. wengine wamezaa watoto vilema, zombie nk kwa sababu ya kemikali hizo.

wanajipoteza katika kujitafuta, wanatafuta uzuri, wanashindwa kujua kuwa uzuri wao umo ndani mwao na sio kemikali. uzuri wa Afrika ni kuishi juani miezi kuminambili na kuwa na rangi nzuuuri ya weusi na sio kujipodoa na kujichubua na ujinga mwingine.

ni hayo tu

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala, kwanza nasema nimecheka kweli. Watu sijui kwa nini hawaridhiki na hali waliyoumbwa afadhali hata hizo pesa wangewapa watoto yatima kuliko kupeteza kuongeza "uzuri" Na sijui kama ni "uzuri" au ni mzigo. Dunia imeharibika ninahisi ni ule mwisho wa dunia sasa unakaribia maana watu wanaongeza kila kitu sasa na wengine wanapunguza. Kwa nini tusiridhika kama tulivyoumbwa? na rangi zetu?

Chacha Wambura said...

YN, habari ndo hiyo

mwisho wa dunia ni kule manda!!! Kuna mtoto mmoja aliulizwa mwisho wa dunia ni wapi akajibu 'ni Manda' sababu ukingalia mwisho wa mawingu si ndo mwisho wa dunia?

hiyo yote ni kwa sababu, mh! (nachelea kuibua mjadala) mama na wadada wetu hawajiamini ndo thababu wanataka kumuulisa sir god kwa nini umeinfanza hivi.

kuna kawimbo kamoja ka dini ya katoliki kanasema...imefikia pahala mkono ama uso ama makalio yanamuuliza sir god kwa nini umeniumba hivi

sijui kama tutafika!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Mimi naamini tutafika kama tutakuwa sisi ni sisi sio kuwa watu wengine. Kuwa na tako kubwa au ndogo au kuwa mnene au mwembamba hivyo ndivyo ulivyoumbwa ya nini kujipasua na kuweka vitu visivyo na maana. Ni kujitafutia kifo tu. Mikorogo, ya nini jamani. kazi kwelikweli.. Nasema tena ni mwisho wa dunia sasa Chaha Wamburu amini sio Manda tu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Yasinta usiogopeshwe saana na siku za mwisho bwana. bado sana. zingekuwa za mwisho usingezaa ili dunia iishe. si tusipozaliana twafa?

Chacha Wambura said...

labda ukiwa na titi, hipsi na tako kubwa unazaa watoto wengi wazuuuuri!!!

kama sivo wanakimbilia nini huko?

Chacha Wambura said...

nesi ama daktari alioko mtandaoni kama kuna ukweli kuhusu hilo

Chacha Wambura said...

na madaktari wamesema kuwa wanaweza kurekebisha matako ya mke wa waziri yalopinda!!!!

ila wanasema operesheni hiyo itakuwa aghali sana, dah!

hapo imefika patamu saaaaanaa!!

chib said...

Swali, Kwa nini mnavaa nguo wakati mlipoumbwa na kuzaliwa mlitoka bilabila!

Chacha Wambura said...

Chib, ni kwa sababu tunaficha sehemu sehemu ambazo tumeziita 'za siri'

sina hakika na huo usiri kwani ninajua kila mwanamke na mbaba ana nini sasa sijui usiri uko wapi.

Mt. simon a.k.a. petro baryoona kitururu anaweza kutudadavulia kuhusu hilo.