Thursday, September 17, 2009

Maisha yetu ni kutanga tanga, mpaka lini?

Asubuhi y a leo nikiwa naelekea kwenye michakariko ya kila siku, nimekutana na binti rafiki yangu wa muda mrefu akielekea job. Binti huyo ambaye imepita miaka kama mitatu tangu tuonane, alikuwa akielekea kazini. Nimeongea naye kwa kifupi, tukasalimiana na kumkumbusha enzi zileeeee tulipokuwa wanafunzi na tuliyoyafanya bila kusahau tuliyo nuia kuyafanya pia. Ni maisha yaliyopita. Historia utunza mambo mengi kwa kweli.

Basi binti alikuwa mitaa ya posta akielekea kazini. Nikaona pia mkanganyiko wa kimaisha ya kila siku. Anaelekea nitokako kama kazini kwake wakati mimi pia naelekeo atokako kuwa ni kazini. Ni maisha. Siwezi kuwa yeye ili niwe karibu na kazi wala kinyume chake.

Kanielezea anavyofanya kazi fulani ya kuingiza takwimu kwenye kompyuta. Ni kazi ya muda mfupi japo inampatia kiasi kikuubwa sana cha pesa. Binti huyo ambaye ni muhitimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam kanistua juu ya wasi wasi na hofu ya wanadamu waliowengi ya kukimbiza kilichokuwa mbali nao wakidhania kitawapa furaha kumbe ni noma.

Kanielezea anavyofanya kazi ile lakini anaweza kuachana nayo muda wowote akipata kazi nyingine kwani haina ¨future¨, eti ni ¨temporary¨ n ikaangalia na kushangaa juu ya kawaida yetu ya kuishi kesho badala ya leo na sasa. Anatafuta kazi ya kesho wakati kesho yenyewe hajaiona badala afanye kwanza hii ya sasa. Hajui kama kesho yake inategemea sasa. Ana hofu, ana wasiwasi na majuto

hajui kama kazi ile itamuhakikishia ¨future¨. Ni msomi ni mhitimu wa university of Dar es salaam ana shahada ya BCOM, nzuri tu. Mtu kama huyo hawezi kufanya kazi kwa ufanisi wala kwa moyo kwa kuwa anaitafuta nyingine, si ameishaifikia kesho? Anadhani akipata yenye future itamsaidia sana. Hajui kuwa kuishi kesho wakati bado uko leo ni kujichanganya akili bure.

Msomi huyo wakike na wanawake wanasemekana kuwa noma, eti ukimsomesha mmama basi umesomesha kijiji kizima kuliko libaba levi, zinzi liishilo na mmama huyo huyo. Hajatulia. Anatafuta maisha ya kesho sio ya leo. Hii ndio noma yenyewe. Hana mpango wowote, yeye ni mwanasayansi wa aina yake, anayetaka kuigundua kesho wakati hajamaliza kuiishi sasa (leo)

ndio maana ukimtongoza mdada, mdanganye utamuoa, si anataka maisha ya kesho? Wakati wewe unaitaka sasa! Ndio maana maofisi yetu hayatulii, hayana watu wanaoweza kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa sababu wanaitafuta kesho. Wanataka kujua bosi anasemaje juu ya kesho, hafukuzi mtu kweli? Mshahala upo je?

Muhasibu anataka awe meneja wa fedha. Mfanya kazi wa kawaida wa wizarani anataka kuwa naibu katibu mkuu, katibu mkuu anatamani kuwa naibu waziri, na waziri anatamani kuwa Waziri mkuu / raisi. Mwishowe ni kutambika ili wawe mawaziri badala ya kufanya kazi kwa bidii na moyo, wanatamani kesho yao.

Ufanisi wa kazi hamna kabisa. Ni ubabaishaji na hofu juu ya kesho au majuto juu ya jana. Ndoa nazo ndo hivyo. Una hofu kama mwezio hashuguliki na wa nje, utadhani wataondoka naye / nayo. Ni maisha ya hofu saana. Una hofu na kulazimika kuwa mnafiki wa kuishi ili ukifa uende mbinguni na sio kwenda mbinguni kabla ya kufa, si unahofu?

Hao ndio wasomi wetu. Eti wanaitafuta ¨future¨ wakati wanahitajika sasa na sio kesho. Malengo yetu ni kupata vyeo na kula hela na kujilimbikizia mali badala ya kutumika na kufanya kazi kwa malengo kwa faida ya jamii pana. Nikisema ntarudi kijijini kuwa mkulima naonekana chizi. Si mjini ndo kuna mihela?

3 comments:

Chacha Wambura said...

sawa lakini na my wife wako ulimwambia utamuwowa ama unamupenda?

aksante kwa kipisi hicho murah!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

marah, leta mawe

Chacha Wambura said...

maweeee!!!

ndiko tulikofika kwa sababu ambazo ziko wazi. Tunatafuta kitu nje ya sisi, duh!