Tuesday, September 29, 2009

Mambo ya Bungeni bajameni.


picha hii ni moja kati ya zilizopigwa katika bunge kivuli lililofanyika juma lililopiata pale karimjee. nimejifunza mengi zaidi ni jinsi ya kuendesha shughuli za Bunge na changaoto zake lakini kubwa zaidi nimeona umuhimu wa kuwa na wabunge vijana wenye changamoto lukuki na wenye vichwa motomoto.

kama picha hiyo inavyoonyesha, kuna wakati inabidi mkuu, utoe jicho kwa hasira na huruma lakini uvumilie na kulinda ulimi sijefyatuka kama bloguni. nimejaribu kuweka video lakini inagoma. mngejionea juu ya changamoto za kambi tawala na kambi pinzani na ni kwanini tunahitaji wapinzani wengi bungeni.

kuna mahala spikianalazimika kuliburuza bunge na akizubaa wabunge wa upinzani watamburuza yeye lakini kuna maamuzi mengine ni ya kidiktata kwa sababu za kisiasa au inabidi iwe hivyo. miongozo ya spika ilikuwa kibao. kwakweli ni changamoto na natamani video ikubali.

baada ya hapo tutasema nini kinafuata. nitasafiri kwenda mikoa mitatu ya kanda ya ziwa ikiwemo Shinyanga, Musoma na kagera na baada ya hapo nitatoa msimamo wangu juu ya kile alichokisema mjengwa au matondo.

tunahitaji damu mpya bungeni jamani au sio?

15 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza nasema picha nzuri umependeza:-) na pia napenda kukupongeza kwa kazi uifanyayo na uwe na moyo huo huo Kamala. Kazi nzuri. Ila bahati mbaya hiyo video imagoma nasi tungefaidi kuona.

chib said...

Mkuu, hongera

Mzee wa Changamoto said...

Naangalia picha hizo mbili zilivyo mkabala na najiuliza kuna tofauti gani ya kinachoendelea akilini mwako??? Moja unacheka na moja unahuzunika. Wewe ndiwe wajua. Lakini nimefurahi kujua kuwa umekwenda kujionea bunge.
Ninalosubiri ni CHANGAMOTO TUSIZOZIJUA TOKA BUNGENI.
Blessings

Chacha Wambura said...

twambie ulikwa kambi gani kati ya hizo mbili?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep. picha zilikuwa zikipigwa kwa kasi. hapa mezani kwangu kuna nyaraka nyingi sana zikiwemo zile za mawasilisho ya mawaziri, katiba, kanuni za bunge na rejea kibao.

unahitajika kuwa makini sana muda wote wa bunge kwani inabidi umsikilize mbunge anayechangia mada. maelekezo ya spika na wewe uwe tayari kulistua bnge pale kinaposemwa ndicho sicho.

kuna mwongozo wa spika zikosewapo kanuni au usomwapo uongo. kwa kweli bunge si mchezo, ni mkiki mkiki. unakuwa na mayaraka kibao na muda wote uko bize na labda ndio maana wazee husinzia wakati mwingine. tunahitaji watu wenye nguvu sana bungeni jamani.

Ofcourse nilikuwa Kambi inayowafaa watu wanaopenda kuhoji na kuhakiki hoja

SIMON KITURURU said...

Hongera Mkuu!
Ila usitie sana huruma mafisadi wasije kudhani weye mnyonge!:-)

chib said...

Nina imani kubwa na Kamala, mafisadi hawatafurukuta

Tandasi said...

Damu changa inahitajika lakini je damu hiyo changa imeenda kutafuta nini humo bungeni, je kwenda kupata umaarufu kama Mh. mawasha, au? JE UNAENDA KUFANYA NINI BUNGENI? hilo ndio swali lenye kubaini weledi na shabaha ya mtu.HONGERA KWA HATUA HIYO MPYA unayoanza kupiga.Tunakuombea.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"Kama picha hiyo inavyoonyesha, kuna wakati inabidi mkuu, utoe jicho kwa hasira na huruma lakini uvumilie na kulinda ulimi sijefyatuka kama bloguni"

Hapa "umeniangusha" Kamala. Kwa nini ulinde ulimi? Je, uwezekano wako wewe kugombea ubunge wa kwelikweli ukoje? Naamini wanablogu watakuwa tayari kuchangishana. Hebu moto huo wa vuguvugu la kutetea wanyonge uendelee kuwaka moyoni mwako!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijatoa tamko rasmi kama naenda au siendi. wakati ukifika nitalifanya hilo.

matondo kuchuga ulimi ni muhimu na hapa usitegemee kuangushwa. unahitaji kusikiliza kwa makini ili ujenge hoja badala ya kuja kujikuta unafyatuka na kutoa kauli tata au ngumu au matusi kwa sababu kuna vitu vinavyoongelewa kisiasa na watu wanavipitisha na kuvipatia muda utadhani vyahitajika.

kwa hiyo inabidi ulinde ulimi ili uweze kujenga hoja kwani uchungu wawezakukufanya utamke hata maneno yale yaitwayo matusi au kufanya kama kule kenya -- yaani kumfuata jamaa aliko na kumpatia mawenzi na ngumi kadhaa

ili kwa utambuzi unaweza tu

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"matondo kuchuga ulimi ni muhimu na hapa usitegemee kuangushwa..."

Kamala nawe bwana, yaani katika typo zote ukaona ufanyie typo kwenye neno KUCHUGA ULIMI. Haya shauri yako lakini Kihaya changu nilichojifunza Kahororo kinaniambia kwamba KUCHUGA ni...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

achani na biashara za kuchuga badala ya kuchunga wewe, rudi kwenye hoja!

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaa.........
Hii kali kuliko Profesa.

Bwaya said...

(Huku nikipiga makofi...)Mzee safi sana.

Anonymous said...

Duh, kweli maisha magumu bongo jamani tuacheni utani. Picha hiyo imenitisha!