Monday, September 14, 2009

ni miaka mitano jijini Dar sasa. bado wakujaehe?


Mwezi kama huu katikati mwaka 2004 ndipo nilipoamia rasimi jiji Dar es salaam.

Mara yangu ya kwanza kabisa kufika jijini humu ilikuwa ni mwaka juni, 2001 nikiwa bado mkristo au mfuasi wa Maltin Luther mzuuri nilitoka kwetu bukoba na kusafiri hadi jijini morrogoro kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa waluteri maarufu kama ”national conference” ambapo tuliimba, kupigwa mikwara juu ya maisha yetu ya baadaye na kufundishwa juu ya ngono (urafiki uchumba na ndoa)

Nikiwa jijini morogoro ambako nilifika kwa treni (ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuiona treni live na kuisafiria nikiwa daraja la tatu – kukaa) niliamua kufanya mchongo na binamu yangu mmoja aliyeko dar ili nifike jijni humo kwani morooro kulilkuwa na mbu wa kutosha. Basi bwana, kimya kimya bila kijulisha familia, nikajitupa jijini. Nakumbuka ilikuwa siku ya jpili.

Kabla ya kufika jijini humu nilidhani jiji hili lilikuwa la-nguvu sana kutokana na madoido na malingo na mikogo waliokuja nayo mikoani wale jamaa waliotoka hapa. Kwanza walijifunza kuongea kama wazaramo harafu kuisifia Dar kama mlokole asifiavyo mbinguni na nilidhani labda Yesu alijichimbia huku!!!

Nilishangaa kuona jiji likiwa limezagaa kila aina ya uchaafu, halitamaniki, mitalo imeziba, limejaa maji machafu na linanuka kila aina ya uozo. Nikadhania labda bado niko Dar vijijiji, akafika jamaa yangu kunipokea, tukaelekea kule home, duh, nikashangaa kumbe Dar watu wanakanyaga udongo! Ile mikogo ya wale jamaa nilidhani huku kuna lami mpaka ndani.

Labda sijafika mujini, tukaenda posta, dah! Sisiemi sana japo niliona maghorofa marefu zaidi. Mkoa wa kagera nilikotokea haunaga matatizo ya umeme kwani umeme unatokaga Uganda. Basi majamaa waliotoka dar wakaja kagera, kila umeme ulipojaribu kukatika, basi ilikuwa gumzo la wiki nzima jinsi mikonai kulivyo hovyo na dar hamna tabu zile, kufika dar nikashangaa mgawo kwa kwenda mbele na hamna umeme mchana mzima. Swali likawa je, yale madoido yako wapi?

Basi bwana, likizo yangu ikamalizika vyema na nikarudi mkoani kwa mbinde. Mwaka 2003 baada ya masomo yangu kule chuoni, nikaja tena Dar, mambo yakawa mazuri kwani nilikutana na msichana N. W, niliyempenda toka Bk akiwa mwanafuzi wa Makongo, basi tukaanza uhusiano raasmi na uongo kibaaao wa nakuota wewe, mara siri, sirari na ahadi za ndoa.

Nikaondoka na kwenda kuanza kazi Bukoba. Wacha nikaasema lazima nikasomee Dar, karibu na N.W mke mtarajiwa, na hivyo kulazimika kuishi nisikukopenda (Dar) kwa sababu kuna ninayedanganya naye kuwa tunapendana (N.W) na kuachana na mpango wangu wa kusomea chuo cha Arusha.

Ulikuwa ni mwanzo wa matatizo kwani nilipokuja mwaka 2004, nilikuta N.W haikubuki tena hata sura yangu wala bangi zangu za kumuoa, kumuota nk, shukuru Mugu sikunywa sumu, vinginevyo usingenisoma hapa leo hii. Dah, yakaisha, nikaanza masomo, nkatamani kwenda Arusha ila kumbuka niliiisha kutelekeza kule kwa ajili ya NW, nikavumilia shida za misongamono ya magari, majumba na hata wingi wa watu chumba kimoja nyumbani, ni maisha tu ya da na joto lake.

Anyway, nilifurahia sana kwani niliishia kujitambua na kuwa ’enlightened’ kupitia initiation ya Santmat meditation. Mpaka sasa nasepa, life is better, tunaendelea kuishi na kusavaivu, badala ya NW nikawapata lukuki, wa mujini, siwawezi nikawa ’singo’ na sasa naendelea vyema

Imepita miaka mitano sasa. Maisha ya hapa ni ya kukimbizana na usiyemuona ya hofu, wasi wasi na misongamano ya kila kitu. Kuna baa nyingi za kujidunga lakini pia kuna maarifa kibao ukiamua kuyatafuta. Makanisa na ulokole ni kabao, na vijiwe pia. Utapeli na uhuni ni wa kutosha lakini michongo pia ni kibao. Nimefahamu mengi hapa ila kuna maisha mengi ya feki na ya kufoji.

Miaka mitano ipitapo ni wakat kuamu kwani nilikuja hapa nikiwa na malengo ya kuishi miaka mitano tu, na sasa ndo hiyooooooooooo imechanganya miguu na kukata kiuno ikitokomea kusikojulikana. Je sasa ni wakati wa kuamia wapi? Mikoa ya kusini, kasikazini au kanda ya ziwa? Kati je? Mashariki je? Au usukumani?

Ua na mimi niende states kwa matondo na kijana wa changamoto nini? No. Au niende Rwanda kwa CHIB? Hapana, kumbuka mpango ni kwenda kwa Yasinta Sweden na kukaa miezi mitatu tu ili nile na kulala bure harafu nirudi huku.

Kwa maoni yako wewe unayeishi mujini na ugenini, unaona ni busara kwanu kurudi kijijini kwetu na kulima na kusaidiana na jamii ya pale au nikae town au niende uzaramoni? Kwa wanyanchoka je? Nafagiia musoma lakini duh, kuna chacha wambura na anajiwwe mfukoni muda wote! Aha ukiangalia negativuz utakuwa sio mwanaume.

Sijui kama niende maulaya na kuanza kikimbizana na Muda ili muda uwe bosi wangu huku nikihaha kupata kilichombali au nisichoweza kukipata na hata nikikipata hakinipi ridhiko na naendelea kukimbiza kingine? Muhimu: ni wakatai wa kuondoka Dar, sijui niende wapi bado, nichgulieni

13 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala, Kamala! Mimi nakuchagulia njoo Sweden na unaweza kukaa hapa hata miaka mitano sio miezi mitatu tu. Swali kwa nini unataka kuhama hama?

Yasinta Ngonyani said...
This comment has been removed by the author.
Yasinta Ngonyani said...

Oh! Kamala naona umebadili picha: Umependeza....LOL

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yeeeeeep yasintaaaaaaaaa. ombi langu naona linachungulia jibu. basi kesho naenda ubalozini kutafuta viza weweeeeeeeeeeeeee

taksomike!

punkt

weeeeeeeeeeeeeeee

Ysinta kuhama hama ni kawaida sana ya binadamu. kwani wewe nilikilikutoa kwenu ukaenda Songea mujini na ukaenda sweden? nini kilikutoa sweden mwaka huu ukaenda Ruhuwiko na kurudi tena Sweden?

nipe jibu nami nitakupa jibu!!!!!!!

sijabadili picha pekee, angalia vyema mabadiliko ni mengi

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Kuna mafunzo kuliko ninavyoweza kushauri.

Yasinta Ngonyani said...

Mmmh! Kamala weeee njoo tu nategemea utapata hiyo visa. Na Kamalaaaa nimekuelewa kukaa sehemu moja si vizuri. Haya mabadiliko mengine sijayaona zaidi ya picha mpya. Naona umeshaanza kujifunza na kiswidi pia safiii sana .Tack så mycket.

Chacha Wambura said...

Swala hapa nadhani si wapi unataka kwenda bali kokote utakakokuwa utafanya nini. kama huna cha kufanya basi uatishia kuwa na bosi aitwae MUDA.

Sina hakika kama ukienda usukumani utakutana na bosi 'muda' au Namala matondo anasemaje? Muda si umiujua huko ughaibuni?

Hivo ng'wanawane, kaza buti zungumza na my wife wako mjue mnahamia wapi. Si mbaya ukanunua manati kama unataka kuhamia Musoma kwa babu yako nyerere!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yTackso mickey, vilcomen, olvidsjar

Marwaaa!! ukurani sijitaki nini???

haya bwana

Chacha Wambura said...

KL, kama waogopa kuja musoma basi kokote utakakokwenda ni nzugwe tu manaka naona kama unakimbia matatizo ya Dar kama foleni, ubize nk

shaurilo!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha una maana gani ukisema NZUGWE? u ndo ki nyanchoka?

Chacha Wambura said...

yaani taabu tupu

ni kiswahili cha kwenu hukooo bongo daslaam

Koero Mkundi said...

dada yasinta ujiandae na matoke huyo ni muhaya akija kwako ukumbuke na mlo na Heniken...lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koerooo. sinywe henken mimi