Thursday, September 3, 2009

nimeulizwa swali juu ya uwepo wetu

swali hili limetoka kwa msomaji anayenisoma kupitia magazeti ninayoandikia makala kadha wa kadha na amejitambulisha kama Peter Shirima Mkazi wa shinyanga mjini........


bro, habari za leo, hivi kwa nini tupo hapa duniani? au tupo bila sababu? yaani sisi kama sisitunanufaika vipi na uwepo wetu hapa duniani na kama tupo sio kwa faida yetu, tupokwa faida ya nani?na kama ni kwa faida yetu ni ipi? na kama sio kwa faida yetu ni kwa faida ya akini nani? na nikwanini kwa ajili ya hao wengine kama tupo ajili yao? nimesindwa kujua kwa sababu baada ya mwanadamu kuucha mwili (kufa) sijui ananufaika nini na uwepo wake hapa duniani.

na sms nyingine ni....

uwepo wetu hapa duniani maanake ni nini?, faida ni kwa ajili y a nani? ni kwa ajili mwili? na je faaida hiyo ni ipi?

sms ya mwisho ilikuwa.......


hatujui sababu hasa ya uwepo wetu? sisi kuwepo tupo kwa sababu tumetakiwa kuwepo tu na maumbile?


wewe msomaji sijui kama unajiuliza maswali kama haya au una majibu walau kidoogo kwa ajili ya mwenzetu huyu. karibuni kuchangia.

9 comments:

Chacha Wambura said...

nionavo mie, ni kuwa sababu ya kuwa hapa ni kufurahia maisha (makulaji, ugimbi kwa sana, kuwa na watoto wengi, kuwa na wake wengi)-kumbuka mie ni mkurya, sasa unaguna nini ebo?

hata hivo nimeumbwa si ili nikate ku kwa ugimbi ama totoz ila hivo vitu vimeumbwa kwa ajili yangu!! (eating/drinking to live and not living to eat/drink)

kinachonitatiza ni kuwa sijui ni kwa nini tunateseka hapa duniani kama huyo aliotuumba alitaka tuishi maisha pooowa!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Wambura marwa, and totoz unazichukua ili uishi au ili iweje, umeumbwa kwa ajili ya totoz au totoz kwa ajili yako?

sasa umeleta maswali mengine kwamba tunateseka, ili iweje? kwani wewe unateseka kweli?

Chacha Wambura said...

Naona zimeumbwa ili nizichukuwe!!!! Si ziko nyingi kuliko sisi?

nijuavo mimi, mateso ni kila kitu kisichokuwa katika mpangilio wa kumpa mtu faraja ama raha kama ugonjwa nk. Sasa kama Nyamhanga a.k.a mulungu a.k.a seba a.k.a god alituumba ili tuishi poowa kwa nini kuna magonjwa?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Marwaaaaaaaa. haya we zichukue. nakushauri usome kitabu cha receptivity cha sant kirpal Singh uone anaseamje juu ya totoz.

nan kasema kuugua ni kubaya? kwa nani? kwa mfanyakazianayepata off na kupumzika nyumbani ua kwa daktari anayejihakikishia kipato kutokana na kuugua kwako au wife wako atakayepata ahueni ya usumbufu wako kwani huna nguvu au kwako wewe utakayekaa na kutulia na kufayiwa kila kitu, si unaumwa?, sio kubaya bwana

Chacha Wambura said...

nitumie kitabu hicho mkuu...

kwa maana hiyo kuugua ni kuzuri?

je ndiyo sababu ukienda hosp ukamuuliza mtu hata kama yuko kwenye machela mahtuti juu ya hali yake atasema kuwa ni nzuri?

nahisi kuchanganyikiwaga kiasi fulani, ne!

SIMON KITURURU said...

Upo ukijisikia upo.

Unasababu za kuwepo akili ikikutuma kujiuliza kwanini upo na ukapata sababu za kuwepo.

Kama huna sababu zakuwepo labda jiue tu kwa kuwa kama huna sababu hata yakuishi labda hustahili kuwepo

Kama hukumbuki ya kabla hujazaliwa basi kabla ya kuzaliwa haukuwepo.

Ukizani utakuwepo baada ya kufariki, hakuna mwenye vigezo vya kukubishia kwa hiyo farijika au tishika kivyako kama unaamini baada ya kufa utakuwepo.

Na kama ubongo wako haukukumbushi ulivyokuwa unajisikia jana, ACHILIAMBALI MWAKA JANA kama saa hizi, kuwepo kwako jana , leo au hata fikira za kesho ni michezo tu ya ubongo. Na ukiua ubongo na ukiozesha mwili wako ugeuke udongo, hata tukukumbuke kama Nyerere na UJAMAA WAKE labda bado uwepo wako kama mabilioni ya watu waliotangulia KUFA AMBAO HATUWAKUMBUKI ni sawasawa na haukuwepo.

Na umuhimu waliotangulia kufa unaweza ukawa na maana kama umechangia kuwepo kwa kama unaamini uwepo wako unamaana [Hapa achilia mbali michango yao ya makeup ya genes zako au MICHANGO ya AKINA NYERERE na akina HITLER ambayo labda umaana wake kwa vyovyote vile si wakudumu kama tu AZIMIO LA ARUSHA]


NIMEACHA!

Anonymous said...

Swali hili halina jibu maalumu! Ni wajibu wa kila mtu kujiuliza na kupata jibu na ukiweza kupata jibu hapo ndipo utakapoona maana ya maisha. Ingawaeje pia haitaleta tofauti yoyote katika maisha yako!Fumbo!

Anonymous said...

It's the question that won't go away, because the answer reveals that we are here to wake up, to discover our true nature – our gifts, talents and capacities – and to express them.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, one thing u left behind is also to know ourselves and to realize God