Sunday, September 20, 2009

Ulimi ndo mbaya au?

nilipokuwa bado nanenda na mkumbo katika masuala ya kiroho, nilikuwa naimba kwaya kwani napenda kuimba na mpaka sasa huwa naimba imba. basi tuliimba hivi juu ya ulimi....

ulimi kitu kidogo saana
lakini chafanya maajabu.
ulimi wamtukana muumba
natena unamtukuza.

ulimi unavunja unyumba
ulimi watenganisha watu
ulimi wafanana na moto
moto mdogo huunguza pori
ni hatari mwenzangu.

mtu huyo asiyekosa
katika huo usemi wake
basi huyo ndiye mtu mweema
alindaye ulimi wake

ofcoures ulimi ndo unaokula, kunywa maji na kutema makoozi. lakini je ni waajabu labda kuliko viungo vingine kama vile viitwavyo Nyeti a.k.a sehemu za huli (siri)? unaamini kuwa watu wote ni matokeo ya ngono? kipi cha ajabu ulimi au?

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmmmhhhh ulimi Kazi kwelikweli:-)

Chacha Wambura said...

kwani ni ilimi ama ni wewe?

Ni wakati gani unajitenganisha na ulimi na viungo vingine?

kuna kakitabu kamoja nalikuwa nakasoma kanasema ukitaka kufanya biashara ya upendo inabidi ukate kichwa umpelekee sir god kama sawadi a.k.a. sadaka kwani sasa ni moyo a.k.a. loho ndo itakuwa ina-present sawadi na siyo kichwa!!!!

Hivyo upendo utakaotoka kwa moyo ni ule wa agape na siyo wenye kuathiriwa na mawazo ya mukichwa na viungo vingine kama majicho, pua, ulimi, sikio, mustachi, kidakatonge na mudomo!!!!

chib said...

Mimi badi sijaelewa vizuri ujumbe, ngoja nikanywe mlamba kwanza ili nipate akili nzuri ya kuchangia

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

weweeee chib, umenikumbusha mulamba

mumyhery said...

mimi ngoja nikanywe mshana kwanza hahaha!!!!

mumyhery said...

lakini wahenga walisema bora kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mumphrey labda ni hivyo