Wednesday, September 16, 2009

unaaminishwa maisha ni magumu?


mazingira yetu ya jamii tuishimo zinatuaminisha siku zote kuwa maisha ni magumu na sisi tunakubali kwa kiasi kikuuubwa sana.

shule tunaambiwa ni ngumu na siku za mitihani ni vitiisho kwa kwenda mbele. tunashuku uwezo wetu, maongezi na matendo yetu. tunatishiwa juu ya kifo kama vile ukimwi, ajali nk. maisha ni magumu ati.

tunaambiwa hajtujaendelea na uchumi wetu ni mbaya sana nasi tunaamini na kuhangaika. tunaambiwa kuishi karibu na wenye hele ndio kuendelea na ndiyo maana waTZ hujibana DSM na waafrika huzamia na kwenda ulaya na marekani.

tunaambiwa tusipokuwa makini mambo ni mabaya na yanatisha. sasa kuna mporomoko uchumi nao unatutisha utadhani tulishiriki kuujenga. maisha yamekuwa ni ya pesa tu utadhani tulizaliwa na pesa mkononi au bila pesa hakuna maisha.

imetufanya tukaanza kuishi kesho. tunawasiwasi saana na maisha yajayo zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

mbaya zaidi tunaenda kwenye nyumba za ibada na kutishiwa juu ya dhambi zetu, Mungu na siku za mwisho eti hizi ndo za mwisho na zikiisha, basi uwezekano wetu wa kuchomwa moto ni mkuu zaidi. inapendeza pale mmoja kati ya waupigao mkwara huu anapokutana na masahibu makuu kuliko yale wakambiayo wewe uyatendeye kuwa ni dhambi. basi wanamaliza soo kiaina kwa kukudanganya kuwa alipitiwa na shetani kumjaribu kama YETHU alivyjaribiwa porini. unaendelea kuwa na hope mkuu.

Anyway, tusipigane mikwara wala huwa na hofu juu ya hili wala lile. kumbuka hatukuomba kuzaliwa bali sis ni matokea ya michezo fulani ya watu wengine na hivyo hivyo maisha ndivyo yalivyo. simpo, ni mchezo mchezo tu wa kupokea kila jambo kam linavyokuja badala ya wasi wasi na hofu za nitakufa lini au ntakula nini. wewe ishi tu kama nikifo kinakuja kivyake huko na kama hakija achana nacho. jamaa yako anakuonaje sio ishu kwani si ulizaliwa peke yako?

usiende misibani kuzika ili nawewe ukifa wakuzike. kumbuka ukishatoka kwenye mwili (kufa) mwili unakuwa ni taka taka ambayo lazima izikiliwe mbali vingevyo ni harafu kali tu. usijali utaziukwa wapi kwani mwili unakuwa sio wako tena na unastahiri kutupwa popote.

dont fear, take it easy dear

6 comments:

chib said...

Umebomoa au umejenga ukweli wa mambo. Big up kwa uchambuzi

Chacha Wambura said...

yep! n magumu kama huna mapesa

au vipi?

Yasinta Ngonyani said...

Inategema utaona maisha magumu vipi kwani maisha sio mapesa tu. Ukipanga vizuri unaweza ukawa na maisha mazuri tu. Ni mawazo yangu kumbuka.

Chacha Wambura said...

Yasintha, utapangaje vizuri bila mapeni?

ngumu hiyo!!!!!!!

Koero Mkundi said...

KAMA MAISHA NI MAGUMU RUDI BK...LOL

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

koero nini tena? BK = British Kingdom?