Monday, September 7, 2009

utamaduni wetu na dada zetu


japo twajidharau mpaka kuukana utamaduni wetu, wadhungu wanaufagilia na kutamani kuwa weuuuusi!! mcheki anavyosokotwa utadhani mzee wa DUH

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni jambo la kusikitisha kuona ni sisi wenyewe tunadharau utamaduni wetu. Hii nimeona pia katika mavazi tuanaacha kuvaa mavazi yetu ya heshima na ya kiutamaduni tunavaa vinguo visivyo na heshima. Mdhungu anataka kuwa mweuusi na mweusi anataka kuwa mdhungu. Kazi kwelikweli.

Chacha Wambura said...

ndivo wanavotuambia kimawazo na kifikra kupitia media

twaona mweupe ni bomba na tumeacha msemo ule wa blaka iz byute!!

Kuna stori moja ya ndugu zangu wakurya ambayo huwa naikumbuka sana. kuna mdada mmoja alikuwa nafanya kazi CARE. akapelekwa tarime kufanya monitoring and evaluation. aliitisha kikao kukawa na wababa na wamama wamekaa nyuma ya wababa (kama msikitini vile!!!!)

basi mdada wa watu akawa yeye kapendeza kinoma (alivaa jinzi na nywele zake katia kalikito). akanyosha mbabu mmoja akasema 'hibhi umetuita habha ghucha kufanya nini! hatuwesi kuzungumza na rimwanamke rimevaa suruari na rina nywere kana zimerambwana ri-mbwa'.

Mzee wa watu kajikalia kisha akabeba fimbo yake akatokomea. Wanaume wakamfuata nyuma kisha wavijana na baadaye wamama (hawangekaa katika kikao kwa sababu wataenda kupata kipondo kunyumba).

hii inaonesha kuwa wapo bado wazee wanaoshangaa kwa nini ubadili vitu fulani fulani kama nywele, ngosi ya mwili nk.

Aha!!!msije mkaanza kunishambulia kwani miye si ni mkurya?

chib said...

Dunia imebadilika sana, wazungu wanataka kuwa kama weusi ndio maana wanafanya tanning, na wakija afrika wanajianika juani ili wawe weusi kidogo, wakati weusi busy na kujibadili kuwa weupe. Nasikia soko la manyoya ya paka limeongezeka, watu wanatengeneza nywele kutokana na malighafi hiyo ili nwele zifanane na za wazungu

Chacha Wambura said...

na leo kwenye magazeti timesikia ati ndoa ya mh. waziri fulani iko matatani/mashakani kwa kile kilichoelezwa kuwa 'makalio a.k.a matako' ya mke wa waziri yamepinda baada ya kutumia madawa ya kuongeza makalio!!

hiyo nimeipenda!! kwa sababu imetokea kwa wakubwa pengine ufuatiliaji utakuwepo.

SIMON KITURURU said...

:-)