Wednesday, October 21, 2009

Bukoba ni mvua za kufa mtu

nikiwa ukingoni kabisza mwa safari yaangu ya Mkoa kagera iliyoambatana na mikakati kibao, nimeshangazwa saana na hali ya hewa hya mkoa huu wa kagera.

mikoa yoote ya nchi hii imekauka, ni ukame na ninjaa lakini mkoa wa kagera mvua zinanyesha na mazao yanaendelea kukua shambani na yanayovunwa basi huuzwa nchi jirani ya Uganda wakati mikoa iliyobaki ikiwa na njaa za kutosha na vyakula bei juu.

inashangaza ni kwa nini vyakula vielekee uganda na sio mikoa baki ya tanzania. labda ishu ni bara bara na njia za usafirishaji kwani ni rahisi saana kusafirisha bidhaa yoyote kuelekea uganda kuliko Tanzania

anyway haka ni kanchi ka ahadi ndio maana vyakula na mvua vya kufa mtu na labda ni hamie huku bongo

napiga hodi kwa Wanyanchoka na wanyanchori eti naenda kuwapiga utambuzi wakati wana mishale, mikuki na ni wataalamu wa kurusha mawe wakila Nyama na kunywa damu mbichi inayowatia unyama. je nitaweza kuwapatia utambuzi bila kula jiwe? mkiona kimya mjue washanitenda wale.

najiamini

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Safi kama unajiamini na uendelee kujiamini Kamala.