

wanakijiwe, baada ya kufika mjini bukoba na nikiendelea vyema na maandalizi ya kutoa mada za yutambuzi mjini hapa, naomba radhi kwamba sitakuwepo kijiweni hapa kwani naingia msituni kidogo kama zinavyoonyesha picha hapo juu.
ni miaka mingi sana sijafarrahia maisha ya kijijini lakini hata hivyo nimeamua kwenda bush wenyewe wanaseama kusafisha nyota. naenda kukaa migombani na ku-meditate kwa muda mrefu huku nikikaa na wazee wangu na washikaji wakule kwa muda usiojulikana lakini sio mrefu sana. nitaoga mtoni na nitazima mawasialiano yoote ili niipata fresh kule
kwakuwa mimi ndiye mtundika mada kijiweni hapa, msishangae mkiona kimya jamani. nitawaletea habari mpya kwani nitatoka huko nikiwa kiumbe kipya kabisa.
all the best na furahieni maisha.
4 Maoni::
Usisahau Rubisi huko kijijini. Mapumziko mema Mulangira!
Uwe na wakati mzuri Kamala
Omwami, usipotelee huko, sawa murah?
Mtondo, Lubisi sijafuatilia wala nini
am back now
Post a Comment