Friday, October 23, 2009

mapenzi ya enzi na enzi

"nitakupenda mpaka ziwa victoria likauke, mpaka dagaa wakonde.

nilapo chakula nakuona kwenye beseni na kila nikioga nakuona kwenye bakuli.

wewe ndiye wangu kwa kweli nakupenda kuliko hata wazazi na sasa sijui nifanyeje kwa kukupenda ila tu jua ya kwamba nitakupenda mpaka basi"

duh!!!!!

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kumbe hizo enzi na enzi kulikuwa safi sana...LOL

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Umeiona hii wakati ukipitia makabrasha yako ya zamani nini? Safi sana! Nakumbuka kijijini kwetu kulikuwa na jamaa mmoja fundi sana wa kushusha hii mistari (naapa siyo mimi) kiasi kwamba vijana wote tulikuwa tunaenda kwake kuomba msaada wa kuandikiwa hizi tenzi.

Mambo yamebadilika sana. Enzi zile maneno matamu kama haya yalitosha kumlainisha "mwisiki" lakini siku hizi sidhani. Kama mfuko wako una matundu hata uwe bingwa wa "kupiga mistari" namna gani sidhani kama utaitikiwa...Siku hizi ni pesa na hadhi yako katika jamii - gari unaloendesha, nguo unazovaa (wenyewe wanaita pamba) na ...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Masangu Matondo Nzuzullima

bado wapo ila sio wa kudanganywa au sio?

yasita km umezipenda basi ndo gia (gear)

Chacha Wambura said...

Masanguu!!

Hapo tena ndoho tabhu...lol Kwani ukiapa kuwa ulikuwa weye utakwaje? ...lol

Pengine una uhakika kuwa hukufanya hivo kwa sababu hizo si gia za CHAGULAGA!....lol

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nadhani waisiki walikuwa wanajua kuwa wanadanganywa lakini meneno matamu yale yalikuwa yanapendeza sana. Japo yametiwa mubaalagha sana - cha ajabu ni kwamba yaliweza kuvuta usikivu wao. Sijui ni kwa nini mtu anajua kabisa kwamba anadanganywa lakini bado anakubali kusikiliza na...nyie watu wa utambuzi pengine mnajua.

Chacha - Chagulaga - we acha tu! Mabinti wa Kisukuma - ilikuwa kazi kweli kweli! Wakurya chagulaga yenu inaitwaje?