Friday, October 23, 2009

MISOSI YA BUKOBA EMAIL KUTOKA KWA MWANAKIWE WA BUKOBA
HII NDIYO BUKOBA YENYE NEEMA.
Kwa miaka kadhaa sasa nimekuwa mkazi wa mji wa Bukoba Kata ya Hamugembe, Mtaa wa Omukishenye(eneo lenye mchanga). Nimeanza kuishi Bukoba bila ajira wakati huo nilikuwa nachukua kozi ya Hotel Management na kwa bahati mbaya shule hiyo haikuwa nabweni hivyo tulilazimika kuishi street na kujitegemea wenyewe. Niliemea chakula, mkaa namahitaji mengine then nikawa nawajibika kuandaa mwenyewe.
Ninachotaka kuongelea ni maisha ya Bukoba yalivyo cheap kwa upande wa chakula ukilinganisha na miji mingine size ya Bk. Kwa Bk chakula kikuu huwa ni Ndizi (Ebitoke), na hii ni kwa makabila yote yanayoishi Bukoba asijeakakudanganya mtu eti ni chakula maalumu kwa wahaya tu, HAPANA.
Simnajua kuwa chakula kikisha kuwa na unafuu mambo yote yana…. Kama unavyoona picha za magari yenye chakula , hiyo mizigo wala haiendi soko kuu ila inaenda kwenye ka soko kadogo ka mtaa wa Omukishenye. Ndani ya ka soko hako huwa yanaingizwa magari yaliyosheheni kama unayoyaona pichani manne kwa siku za Jumanne na Ijumaa(Hizo ni shehena za ndizi, kabeji, palachichi, nanasi , nyanya, nyanya chungu , mihogo, magimbi pamoja na mengine kibao. Pamoja na shehena hiyo kuingia mtaani kwetu sasa neema unakutana nayo katika bei. mie huwa najisikia kumpa sifa Mungu hasa nikiona unapata mfungu wa magimbi kwa shilingi mia tano tu. Mimi sina familia kwa hiyo huwa sijishughulishi na mambo ya kupika, ila nilibahatika kuonea na rafiki yangu mwenye familia(mme, mke, mfanyakazi na mtoto) yeye aliniambia magimbi ya shilingi mia tano tu ni mlo tosha kwa familia yake tena wakati mwingine kunakuwa na ziada, na vyakula vingine kama mihogo na ndizi hali inakuwa ni hiyohiyo. Kwa nanasi huwa ni shilingi 200 – 500.Mji wa Bk huwa unategemea sana kupata vyakula kutoka Wilaya za Muleba, Bkb vijijini-IZIMBYA na Karagwe kwa % kubwa. Hapa nimeongelea tu kwa mtaa wa Omukishenye lakini panapo majaliwa nitakuonyesheni hata Soko kuu ili uone mwenyewe.
Mungu ibariki Bukoba

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hizo ndizi hizo umeniumiza kweli ROHO. Kamala tubadilisha uje huku na nami nije huko....LOLAmen!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

acha hizo Yasinta. mimi nakuja huko ukiwepo na sio vinginevyo na hata hivyo niliishapanga kuwa nakuja kukaa miezi mitatu tu na kurudi bongo. siwezi kukaa ugenini hata kidogo km nyie huko

PASSION4FASHION.TZ said...

Kaka Kamala nakuunga mkono kwa asilimia 100,Tanzania tuna kila sababu ya kumshukuru sana mungu,mengi katujalia na kama tungekuwa wenye shukrani tulipaswa tuseme "mungu katupendelea"Katupa bahari,maziwa,mito,milima,mabonde na mabwawa ardhi nzuri iliyojaa rutuba,mifugo ya kila aina lakini bado unakuta kuna watu maeno mengine bado wanalala na njaa,hawana maji safi ya kunywa.

Jana nilikuwa naangalia BBC NEWS saa 6Pm sikuamini macho yangu na maskio yangu kwa nilichokisikia na kukiona kwenye TV,jirani zetu Kenya wanakufa kwa njaa,kuna ukame huko haujawahi kutokea,mifugo inakufaa,binadamu wanakufaa kwa njaa na kukosa maji,watoto ukiwaangalia kama huna roho ngumu lazima utatokwa na machozi,niliumia sana nikakumbuka kwetu Tz vyakula vinaozea sokoni,vinaharibika vina mwagwa,badala ya kuwatafutia masoko ya kuuza nje wakulima wetu,siwangefaidika na nchi jirani tu hapo kama Kenya jamani?tena na uhakika vyakula vingewafikia vikiwa fresh,kuliko kuacha watu wanakufa na njaa na upande wa pili vyakula havina masoko mazuri vinashia kuharibika na kumwagwa.
mungu endelea kuibariki Tz.na watu wake iko siku labda itapata viongozi wa kweli.

Born 2 Suffer said...

Ni mtori kwa utumbo hapo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

passion4passion, umenena. nazunguka sana mikoani na ninayaona haya unayoyasema juu ya tz na kwa baraka za tz ulizotaja ni kidogo ili uzzitaje zote unahitaji kukaa na kutulia vinginevyo huwezi kuzimaliza, ni lukuki.

Anonymous said...

NIMETAMANI KWELI HIZO NDIZI BUKOBA.KAMALA NIRUSHIE PICHA ZA HUKO KWETU KAYANGA BASI (IRENE) JAMHURI STREET

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

irene siko tena kayanga nimeshahamia mikoa mingine picha nitarusha zilizomo kwenye faili zingine mpaka wakati mwingine

kasinge mawe

Anonymous said...

KAKA YANGU KAMALA HUYO IRENE ASIHOFU IPO SIKU ATAZIPATA PICHA ZA KWAO KAYANGA, LA MSINGI ATUOMBEE UZIMA.
NI KAWAMALA ALEX (MWANAKIJIWE WA BUKOBA)

Tandasi said...

kamala upo juu!

Anonymous said...

mimi mwenyewe nilizaliwa omukishenye na nimekulia hapo hapo, nimefurahi sana kuona picha za omukishenye na mto kanoni,nilikuwa napitia kishenge kwenda shule,tuwekee na picha za omukishenye tuone mabadiliko maana miaka mingi nimeondoka,watu wengi sana nawakumbumkuka mfano kina ta nestori alibaliwo na wengine wengi.