Thursday, October 15, 2009

nimejifunza mengi kule bushi kwetu

Daima nikifikaga kijijini kwetu huwa sipendi kuongea saana na wazee na mara nyingi huwa nakuwa mkimya na msikilizaji kwani pamoja na upungufu wa wazee wetu wa kujitia wanjua saana kutuma laana na kutaka kutukuzwa, wapo wengi wenye busara, hekima na mitizamo lukuki juu ya maisha yetu na jamii yetu

nilienda kupumzika na sikuenda kutembea tembea lakini nilikutana na mzee mmoja mwalimu mstaafu maarufu kama mwl Mushumbusi ladislausi, ni mkatoliki mzuuuri ambaye kaamua kumpeleka mwanae wa mwisho Lwejuna almachius kusomea taaluma ya kutoa kibubusa (dogma) namaanisha uongozi wa kuchunga kondoo wanaosimama kwa miguu miwili, namaanisha watu na hivyo kaenda kusomea upadre

basi aliniambia kuwa kijana wake anasomea falsafa. akaanza kuniambia juu ya umuhimu wa kusomea falsafa na kwamba ni somo muhimu kwetu kama kweli tunataka mambo yanyooke vizuri kwetu katika ngazi za kijamii na hasa 'si-hasa' namaanisha politiks

mzee Mushuimbusi anasema wanasiasa woote makini wanaojenga hoja na kutetea maslahi ya wengi wamesoma falsafa. anasema Nyerere ni mwanafalsafa, Slaa, Zito Kabwe na wengineo. je ni kweli tunahitaji wanasiasa wa kifalsafa-falsafa kama anavyodai ndg Mushumbusi? je we mtizamo wako ni upi? kuna ushahidi mwingine juu ya hili?
kitururu je?

7 comments:

SIMON KITURURU said...

Falsafa zangu zaweza kumfanya Mwanakondoo ajinyonge!:-(

Na kwa bahati mbaya falsafa zangu hazikusomewa popote!:-(

Na kwa kawaida naamini kuna Wanafalsa ambao they are too AIDIALISTIK kiasi kwamba naamini inategemea nchi ikokatika hatua gani iliwawe na manufaa.

Kwa mfano naamini Tanzania sasa hivi haihitaji MAAIDIALISTI kama akina mfu Nyerere. Inahitaji watu kama Putin wa Russia kwamba akisema tunaibwenga Georgia basi Russia inaibwenga kweli Gorgea.AU tu kama Rais wa China ambaye akiamua kuwa Kibaha iwe bwawa, basi mtake msitake watu wa Kibaha hata mlieje mtatimuliwa na itageuzwa bwawa.

Nachojaribu kusema nahisi tunahitaji zaidi watendaji wa ambayo tayari tunajua ukitenda kitu kinatokea na sio sana falsafa Mpya.

Kwa mfao kama Kikwete angekuwa anaweza kutekeleza aliyosema wakati anagombea pamoja na kuwa Maisha bora kwa Mtanzania yasingekuwa yametekelezwa, lakini angalau tungefikia sehemu kusema kweli kazi kaifanya bila kuigeuza mitazamo yake wala Falsafa.

Kitu kingine naamini kuwa karibu Watanzania wote ni wanafalsafa ukiwasikiliza wakati wanatongoza.Ila afanikishaye uasherati baada ya mtongozo , huyo kavuka falsafa na sasa anafanya ngono.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala ulikuwa unamissiwa. Nashukuru kama umerudi salama na pia umerudi na nguvu mpya.

Chacha Wambura said...

Mtakavitu Simon, nakukubalia na nakukatalia kwa wakati mmoja. Nakukubalia kama huyo umsemaye atakuwa na mawazo chanya lakini nakukatalia kama huyo mutu itakuwana mawazo hasi ya kutuchanganya. Na yule ambaye ana mchanganyiko wa hasi na chanya ndo maweeee...lol

pia falsafa zinatofautiana, unaweza ukamsoma makiaveli ukamwelewa tofauti na padre anavomsoma hivyo tinahitaji kufikiria saidi juu ya wana-FA tunaowahitaji.

cheers

SIMON KITURURU said...

@Kadinali Chacha Wambura:

Nami nakukubalia kwa ulicho nikatalia.

Kunauwezekano mkubwa nimerahisisha jibu la swala gumu kwa kutogusia zaidi aukuindia kiundani zaidi katika pande zote za tako katika hili swala.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kitururru juu ya kusoma nakubaliana na wewe. sisi sote ni wanafalsafa kwakweli na lilie ulisemalo nimeliona vijijini kwetu. watu wasiosoma, wanashikilia falsafa fulani na kuzisimamia na kuleta mabadiliko chanya.

ila katika ulimwengu unaoongozwa na mfumo wa elimu uliojaaa ubinafsi na nini sijui, kuna haja ya kumfanya mtu kureje falsafa yake binafsi kwa kumpitishia kwenye falsafa za mizoga aka wafua kama nyerere, makieveli na wengine, hii itasaidia kwao kurejea nyuma na kujirekebisha, au sio?

Chacha Wambura said...

Mt Simon, aksante kwa kukubali kutofautiana.

kwa kweli hatuhitaji viongozi philosopers (wana-FAs) bali viongozi Reformers. Na hawa reformers siyo wa ku-reform mafisadi bali watakaoji-reform wao wenyewe ili kwa kuwatazama wao tuweze pia kuwa reformed...Nadhani dhana hii ndo inafananafanana na ile Omwami KL aliiongelea ktk mojawapo ya posts zake za nyuma ambapo alisema kuwa tunahitaji viongozi walojitambua...I stand to be corrected.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Chacha, ukitaka kubadili ulimwengu, unafuata kanuni ya st Baljit singh ya; "change yourself so that you can cange the world"

ukitaka kuubadili ulimwengu jibadili wewe kwanza