Monday, October 19, 2009

nimepokea barua juu ya uchafuzi wa mto kanoni


picha na email ni ujumbe na malalamiko ya mwanakijiwe mwenzetu akaaye na kufanya kazi zake mjini bukoba. ni mwanaharakati wa mazingira na mpenzi na mfuatiliaji wa kijiwe chetu hiki. nimeona ni vyema niutundike ujumbe wake na picha kijweni kama unavyosomeka.........

Pole na majukumu, nimetuma ujumbe huu nikijua kuwa uko bush ila ukija mjini tu utaupata.
Kila ninapo jaribu kutoa comments zangu kwenye mada zako nashindwa, labda ni kwa vile hii technology kwangu haijapanda, but i hope utanielekeza vizuri tu pindi tukionana au waweza kunielekeza hata kwa njia ya maandishi.
Maoni naweza kutoa au nisitoe kitu cha muhimu kwangu ni kupata muda wa kusoma zile mada zako na kuzitafakari.
Bila shaka wewe ni mtu unayeifahamu vizuri Bukoba, hapa huwa kuna ka mto kanoni kale ambako kanamwaga maji yake ziwa V. Mimi huwa nakapenda kwa jinsi kalivyo kaakaa ila nimekuja kusikitishwa na kitu kimoja kinachoitwa uchafuzi wa mazingira/kanoni. kitu ambacho sikukielewa ni pale tu maeneo ya Hamgembe inayopakana na Migera lakini inatenganishwa na mto kanoni kuna vituo zaidi ya 10 ambavyo vinaendesha shughuri za kibinadamu. Mfano: kufua, kuosha vyombo, kuosha pikipiki, kuoga na mengine mengi ambayo kwa kweli yanatia kinyaa hata wewe ukiona.
Hivi kweli najiuliza kwa staili hii tutawezaje kutunza mazingira? nimebahatika kupiga picha moja ya shughuli zilizo kuwa zikiendeshwa pale, KWA KUJIFICHA LAKINI
kwa taarifa au nyongeza tu ni kwamba katika mji wa bukuoba, mto kanoni una sababisha uwepo wa madaraja takribani matano kama sio sita na hulisha ngombe na mifugo mingine na pia watu hulima mazao lukuki ya biashara karibu na mto huo

1 comment:

chib said...

Watu hatuna ufahamu wa kutosha kuhusu kutunza mazingira na usafi wa maliasili.