Thursday, October 1, 2009

BAADHI TA TUMISEMO TUMEBORESHWA

RAHA YA DAFU, UKISHAKUNYWA YALE MAJI, SHARTI DAU LICHOKOLEWE

RAHA YA CHUNGWA, UMENYEWE, KISHA UKATIWE".


RAHA YA NANGA BAHARINI, MTONI ITASHIKWA NA TOPE."

UTAMU WA NDIZI UKO NDANI YA "NGUO" ZAKE.

VUA NIKUPE VITAMU KAMA UTAWEZA KUVUMILIA VIGUMU PIA

Ingawa vingine ingawa hunoga ukivivua lakini waweza pia kuvifunua tu halafu kwa mrija ufyonze juisi ya ndani ya embe iliyobinywabinywa embe sindano.

KULA NANASI KUNAHITAJI NAFASI.......

mwalimu alizoea kusema wavulana juu wasichana chini akiimanisha hosteli za wasichana zilizokuwa sehemu yenye mwinuko na sisi tulikuwa pande nyingine.

mtaka cha uvunguni, sharti ainue kitanda.

aliyekojuu, mfuate huko huko maana hashuki na anazidi kupenda.

asiyesikia la mkuu, masikio yake hayasikii vizuri au hasikilizi.

mwenye macho, anaona vizuri.

akili ninywere, kwa sababu ziko kichwani

7 comments:

chib said...

Bahati nzuri watoto wanajiandaa na mitihani ya kiswahili hawaisomi habari hii, vinginevyo, wameanguka katika mtihani! :-)

Yasinta Ngonyani said...

Kamala:-( Kazi kwelikweli

SIMON KITURURU said...

DUH!:-)

Chacha Wambura said...

ngja nikatafute mawe zaidi...lol

Tandasi said...

kiswahili na changamoto zake je wakenya wanajua tunavyokikimbia kiswahili

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Lugha ni sehemu ya jamii nayo huakisi mabadiliko yanayotokea katika jamii. Methali, misemo na ukopaji wa maneno ni baadhi ya vipengele vichache tu ambavyo huakisi mabadiliko haya kwa uwazi zaidi. Nadhani wengi mtakubali kwamba katika hali ya kawaida methali na misemo kama polepole ndiyo mwendo, haraka haraka haina baraka, aliye juu mngoje chini, vijana ni taifa la kesho na mingineyo imeshapitwa na wakati.

Na misemo ambayo Kamala ameiweka hapa inaakisi vyema falsafa ya sasa katika jamii na kama alivyosema Mzee wa Changamoto tunaweza tusiwe na tafsiri moja. Hebu tusome tena maoni mwanana ya Mzee wa Changamoto hapa: https://www.blogger.com/comment.g?blogID=7953064069616248417&postID=1759176434190041809&isPopup=true

Mzee wa Changamoto said...

Kwanza NIKIRI kuwa kuna wakati nashinda kutoa maoni kwa kuwa nakuwa sina uwezo wa kueleza namna ninavyofurahia uhusiano nilio nao nanyi. Kaka Chib, Da Yasinta, Kaka wa Mkodo, Mtani Chacha, Kaka wa Ndotoyangu Tandasi na Profesa Matondo (kati ya wana-blog wengi) nawaheshimu, nawathamini na najivunia kila wakati niwaonapo.
Kaka Kamala asante kwa "kusanyiko" la haya maneno. Imenifanya nirejee kwa Da Mdogo wangu K na kusoma maoni ya wachangiaji na kisha nimepata meengi ambayo niliyakosa niliposoma mara kadhaa zilizopita.
Tupo PAMOJA na kwa pamoja TUTAFIKA