Friday, October 2, 2009

ukikutana na mpenzi wako wa zamani

Jmosi ya tarehe 4 Oct naanza safari ya pili katika kufanikisha adhma yangu ya kuhama jiji la dar na kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa. niliwahi kusema kilicho nileta dar miaka mitano iliyopita na sasa ni wakati wa kuondoka zangu kabla mwaka haujatokomea kusikojulikana.

sasa sababu iliyionileta Dar ni kusoma japo nilipaswa kwenda Arusha, nikasingizia kutokupata chuo kumbe nilitaka kuwa karibu na aliyekuwa mpenzi wangu NW. hata hivyo alinipiga chini sikuwa naye wala nini

juzi tu nimekutana naye, bint yuleee niliyempenda na kuongea naye kama vile sina haja naye ya kimapenzi tena wala nini. NW aliponiangalia jichoni, nilirejea mwaka 2003 tulipokuwa wapenzi, duh, inakuna mpaka moyoni lakini ndo hivyo, nshajisalimisha kwingine

niliongeanaye kwa muda na kuuliza kulikoni lakini maisha yanaendelea. sikutaka kujua saana kama yuko kwenye uhusiano mwingine kwani hayao ni maisha yake binafsi na siyo yangu. aliniambia anavyofanya kazi katika benki moja ya jijini Dar, nikampongeza na aliniambia anaishi maeneo ya Kinondoni.

sikutaka kupajua anapoishi na wala sikutaka namb a yake ya simu na bahati nzuri mimi sio mteja wa benki anayofanyia kazi. ni maajabu kuwa alilnisabishia kuhamia hapa na sasa ninapojiandaa kuondokanakutana naye tuna.

ni maisha ila ukikutana na mpenzi wako wa siku zote ndugu yangu, ambaya uliwahi kumpenda kiukweli ukweli, hata ujifanye vipi lazima kuna hisia fulanilakini kumbe mambo yalipaswa kuwa kama yalivyo na ndio maana sio wako tena

wakazi wa Musoma, mwanza, kahama na Bukoba, maarifa ya utambuzi yanakuja octoba hii hii, kaa mkao wa kujitambua

8 comments:

Chacha Wambura said...

Karibu mwitongo KL. Huku utakuwa salama bla kukutana na huyo mai nanihii wako alokutosa.

kama huna haja naye niunganishie basi si unajua tena mie mkurya ambaye ni ruksa kuwa na wengi?...lol!

Nyegera waitu,...lol

Mwanasosholojia said...

Hakika ulikuwa na wakati mgumu Kamala, hata hivyo ulishaamua kusonga mbele, kurudi nyuma inakuwa ngumu

Yasinta Ngonyani said...

Nakupongeza kwa kuwa na msimamo. Inaonyesha umeamua nini ufanye.

Mzee wa Changamoto said...

Unapokutana na yeyote unakuwa na HISIA. Linalofuata ni UJAZO ambao hisia za mtu huyo zinakutawala. Na mara zote inategemea alikuwa na uzito gani mawazoni na maishani mwako. Kuna wanaopata HISIA wakikutana na wale waliowaokoa kaika majanga mbalimbali kuliko wanapokutana na wapenzi wao.
Kwa HABARI yako ni kweli kuwa ulistahili kuwa na hisia ulizokuwa nazo. Kumbuka huyu (kwa mujibu wako) alikufanya uje Dar. Umesema ukasingizia ulivyosingizia ili uwe Dar. Haukuwa uamuzi wa siku moja. Uliwaza na kuwazua na kupima faida na hasara (kwa akili za wakati huo) na kisha ukaona ni vema kuwa naye.
Kwa hiyo ni kweli kuwa kwa mtu wa thamani yake kwako, unastahili kujihisi uluvyojihisi. Lakini pia nakusifu na kukupongeza kwa MSIMAMO uliokuwa nao kwa kutoomba namba, kutopenda kujua maisha yake binafsi na hata kutojua aishiko kwani NJIA PEKEE YA KUEPUKA MATATIZO NI KUTOYAPA MATATIZO MWANZO WA KUWA NAWE. Ungeanza kwa namba, kisha ukaongea kidogo, lakini kidogo hiyo ikawa ni miadi na miadi hiyo ikawa ni penzi "kiduchu' na penzi hilo lingetibua kila ambacho umejijengea tangu ulipogundua kuwa hauko naye na unahitaji maisha mapya.
Basi ni vema kumshukuru Mungu kuwa umeweza kuonana, kuongea na kufurahia muda na huyo aliyekuwa "barafu wa moyo wako" kwani wapo ambao wakionana na waliokuwa wapenzi wao hawapiti tena mtaa huo.

Nami hufurahia kukutana na kila aliyewahi kuwa sehemu ya maisha yangu na nathamini kila mchango wao.
Safiri salama na mafanikio mema katika mafundisho yako ya kitambuzi kwani WENGI WANA UHITAJI WA UTAMBUZI.
Blessings

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

maisha haya jamani. basi nikakutana tena na rafiki yake tunayefahamiana, akaanza kunipa salam zake na kuniambia alivyonimiss.

alitaka kunipa namba yake nikajifanya simsikii vizuri lakini akamalizia kuwa atampatia namba yangu kisha atanitumia SMS. nilijifanya sijui kitu na sitaki kujua kinachoendela na najua hawezi kuja mbele yangu kwani utamaduni wa bongo unamnyima binti nafasi ya kujisemea.

kama movie.

Tandasi said...

Nakutakia kila la heri brother lakini vp tamasha la wanablog utakuwepo, hiro richacha rinataka kukubebesha rawama tu mwitongo wasichana wamekwisha. zaidi nakutakia heri MUNGU akutangamainshe na mema na akuepushe na mabaya-UDUMU UMOJA

Chacha Wambura said...

KL, unakumbuka ka-wimbo ka Bushoke ka 'Nimepata Barua toka kwa mupenzi wangu wa zamani?' ama ka wimbo ka 20% ka 'Ningekusamehe?'

Basi usije ukaingia katika mtego wa kupata sms na kuijibu. Ukipata nijulishe nkuelekeze namna ya kui-block na hata simu zake...lol

ameshapigika huyo hana lolote hivo...anatafuta kimbilio wakati tayari ushapata mai waifu wako ambaye ni kila kitu...lol

Chacha Wambura said...

Tandasi, nilikuwa tu nataka kumsaidia kubeba mzigo huo naona hataki sijui kaona wivu...lol