Tuesday, November 17, 2009

Hppy birthday Mamaa Vaileth VM
Ametimiza Umri wa miaka kadhaa, ndio ni vaileth Valentine, katika maisha haya yamwili ni furaha tukizidi kusogelea kuacha miili. lakini kwa wale waliokwisha jichagulia maisha, hawana noma wala wasi wasi juu ya waendapo baada ya kuacha mwili kwani wamechagua sasa kwenda mahala wapajuapo hivyo kusogea kwa siku sio ishu kwao na hivyo huithamini miili yao.

maisha yangu yamebadilika kwa kiasi kikubwa tangu kuwa nawe na sasa nalijua vyema somo la kushirikishana, kushea na kuwasiliana. maisha ni mema na mazuri na Changamoto zake sasa zinakabiliwa sawa sawa kwani kuna mtu wa kunipa moyo. entare shaija eti lyange, enkazi eti likwatanisibwe. katika maisha ndivyo ilivyo, ni lazima upeane, tufarahie pamoja

umefikisha umri wa miaka kadhaa, sasa unaitwa 'mke wangu / wa mtu' na sio binti wala dada tena. muda si Muda, utaitwa mama na kukamilisha moja wapo ya kununi ya utegemezi ya kuhitajika kwa ndugu, rafiki, mpenzi au mtoto.
nakutakia maisha Chanya, yenye kufikiri vizuiri na kutenda vizuri, upendo na Heshima kwa kila kiumbe.
sachKhandi

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nadhani hakuna kuchelewa Hongera kwa siku ya kuzaliwa mamaa Vaileth VM. Nakutakia maisha marefu na pia uwe na wajukuu wengi sana. Hongera.

Masangu Matondo Nzuzullima said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima said...

MAMAA Vaileth VM - Hongera kwa kuoelwa na mtu wa utambuzi. Natumaini mtazamo wenu juu ya maisha ni tofauti!

Happy Birthday na endelea kutulindia huyo Mulangira wa taaluma ya utambuzi ili (kutumia msemo wa 50 Cent) asije akaji-self destruct. Muwe na ndoa njema na familia yenye furaha na amani. Nafurahi kusikia kwamba wewe ni "omukazi" mwema. Mbarikiwe daima!

Mzee wa Changamoto said...

Niongeze nini zaidi ya MAOMBI kwa uwepo na udumu wenu?
Hongera Dada Vaileth na nakutakia maisha mareefu yaliyo na furaha. Kuhusu u-mama nakuombea uje salama na mwana awe mfano kwa jamii
Kwa Kaka Kamala, nasema HONGERA kwa kuwa na huyu Vai ambaye sasa huoni shaka kumueleza hisia
Blessings

Nuru Shabani said...

Hongera sana Vai kwa kutimiza hiyo miaka kadhaa.
Kikubwa tunakumbea kila la kheri.

chib said...

Hongera mama V. Endelea kumtunza jamaa yetu ambaye siku zote anachangamsha vikorido vyetu

Anonymous said...

Vaileth, hongera sana. Mungu akupe maisha marefu. Najua unamipango mingi mizuri maishani mwako basi mungu akutangulie ktk kila jambo jema unalopitia.

Hongera kwa kila kitu, kwani sio wote wanaojaaliwa kuwa na vitu vyote hivyo, mume mtoto, hayo huwa ni majaaliwa tu. Nafurahi tumezaliwa mwezi mmoja japo tumetofautiana tarehe tu.

KILA LA HERI

mumyhery said...

Happy Birthday Mama Vaileth