Monday, November 30, 2009

Kijiwe Chafikisha miaka Mitatu-epibisidei


Jamani kijiwe Chetu kimefikisha umri wa miaka mitatu tangu kiwe hewani. mara ya kwanza kabisa kuona blogu ilikuwa ni kupitia kwa majidi mjengwa aliyekuwa akiandika kwenye gazeti nililolipenda na kuacha anwani ya blogu yake, nilipata shida kuifungua kwani niliandika sport badala ya spot.

nilipofanikiwa kuifungua na kuitembelea, nilitembelea na nyinginezo nyingi kama vile Michuzi nakadhalika. nilifanya utundu na ikizingatiwa kuwa wakati huo (2006) nilikuwa mwanafunzi wa masuala ya Teknohama mpaka nikatengeneza blogu yangu mwenyewe. blogu ya kwanza kutengenezwa na mimimi ilikuwa ni Mushanage.blogspot.com amabayo baadaye nilisahau paswed yake na kuitelekeza na ilikuwa ni octoba 2006

nilitengeneza blogu nyingine kadhaa mpaka hii. mwanzoni iliitwa ijawebonere.blogspot.com na niliamua kuibadilisha jina baada ya kuona ni gumu kulitamka kwa wapenzi wengi wa blogu hii. niliamua kukiita kijiwe kwamba ni mahala pa watu kujisemea tu hii ilikuwa ni bifu baada ya kuona mjengwa anabania baadhi ya comments kwenye blogu yake na hasa za vijana.

baadaye nikaaza kuwatengenezea watu blogs, nilimtengenezea kijana mike dalali (nkwabi.blogspot.com) mike mahenge na wengineo kama vile kaluse (utambuzi na kujitambua).

blogu au kijiwe hiki kilianza kikitoa zaidi habari za kawaida zilizotokana na makala zangu kwenye magazeti, na baadaye picha na makala huku lengo likiwa ni kufanya picha. aliponitembelea bwana kaluse kwa lengo la kutaka kufunguliwa blogu, na akaanza kuandika juu ya utambuzi, ndipo nilipogundua kuwa kumbe maarifa ya utambuzi ni muhimu kushea bloguni. ndipo nikaanza kutundika mambo yanayofanana na hayo.

kublogu kumenifundisha mengi nakumenikutanisha na wengi. sikuwahi kufikiria saana juu ya kutengeneza faida lakini ninafaida lukuki zikiwemo zile za kujamiiana (socialization). sasa nafahamiana na watu wengi kila kona ya dunia. wengine tumetokea kuwa ndugu kwa sababu tu ya kublogu.

nimegundua kuwa blogu hizi husomwa na watu wengi na wengi wao hushindwa au hawapendi kuacha maoni. ukiwa mitaani unaona wengine wanaeleza ni kwa kiasi gani wanafarijika kwa kusoma blogu. hata hivyo muda wa kublogu wakati mwingine huwa mdogo au hukosekana kabisa na hapo ndipo hupita siku kibao bila kutundika jipya lakini muda wote huwa unawafikiria wasomaji wako au wankijiwe.

Leo hii blogu hii imefikisha miaka mitatu kamili tangu mtundiko wa kwanza uingie hapa na nawashukuruni sana wote kwa kunifanya niendelee kuwepo. huwa nafarijika na maoni ya kila mmoja na ninaaminitunaweza kujenge jamii bora kwa kupitia blogu zetu hizi pia.

Blogu pia upunguza urasimu wa vyombo vya habari na hutoa taarifa mbali mbali nampya. kuna watu (na hasa familia) wanaojifanya kutokutembelea blogu hii lakini katika maongezi hujikuta wameongelea yaliyomo humu.

najiuliza ikitokea nikaacha mwili ghafra blogu hii itakuwaje kwani ni mimi pekee mwenye pasword pia mwandishi na mhariri!

OMUKAMA ABABELE

16 comments:

EDWIN NDAKI said...

Hongera sana Kamala kublog sio kazi ndogo..

Nafarijika kuona una moyo wa kublog miaka nenda rudi.Bado nakumbuka sana kipindi tukikutana kwenye kibara za cha Majid Mjengwa.

Nakutakia kila jema katika mchakato wa kublog..tupo pamoja.

Tutafika tu

Yasinta Ngonyani said...

Duh! kumbe miaka mirefuuuu mitatu. Pongezi nyiiingiii sana Kamala. Sisi wengine wachanga kabisaaaa.EPIBESIDEI KIJIWE HIKI.

Mzee wa Changamoto said...

Nakumbuka nilivyoingia hapa kama ajali vile. Sijui nilikuwa nasaka nini katika internet kisha katika kusaka taswira hizo nikaonapost kwa Mjengwa nilipo-click ikafunguka blog yake na baada ya kumaliza kusoma nilichokuwa nataka nikaendela kusoma chini zaidi ndipo nilipokutana na kibandiko chake kuhusu Kamala kuamua kurejea kwenye kutoa maoni. Niliposoma maoni nikaona "thumbnail" kwenye jina lako na nilipo-click nikafunguliwa profile kisha nikaingia ukumbini.
Anyway. Sababu uliyokuwa nayo wewe kuanzisha blog ndio\yo iliyopelekea mimim kuanzisha yangu. Nilikuwa natuma habari na maoni lakini ama yalikuwa yakikatwa saana ama hayakuwa yakiwekwa. Niliposoma kwako na kujua ulichukua uamuzi huo kwa sababu kama yangu, nami nikaanza kujiandaa kuanzisha yangu na sasa ni mwaka na nusu tangu niingie hewani.
Kwa ujumla CHANGAMOTO YETU ni ZAO la kijiwe hiki
KILA LA KHERI KATIKA KILA JEMA UTENDALO

Bennet said...

Hongera mkubwa, kaza buti tuletee mambo zaidi

nyahbingi worrior. said...

mtazamo wangu,sio tu blogu itimize miakaa kadha bali ujumbe katika blogu imewafikia wasomaji?na je wasomaji wamekubaliana kutokukubaliana na yaliyomo katika mada tofauti?

Hongera tu haitoshi.

Amani.Selassi I.

Mija Shija Sayi said...

Ubarikiwe.

Shabani Kaluse said...

NI KWELI KAKA UMENIKUMBUSHA SIKU ILE TULIPOKUTANA PALE JENGO LA MKAPA POSTA TUAKAIANZISHA BLOG YA UTAMBUZI NA KUJITAMBUA, NAKUMBUKA ILE PICHA YA MTOTO MDOGOMULIYOITUNDIKA KWA MARA YA KWANZA AKILA BISKUTI KAMA POST YA KWANZA.........UNA KILA SABABU YA KUJIVUNIA KAKA

John Mwaipopo said...

'ongela' mtoto wa nyumbani kwetu

mumyhery said...

Hongera sana Mkuu Shukran kwa yote yaliyojiri na tunasubiri kwa hamu yatakayojiri

Candy1 said...

Quoting "najiuliza ikitokea nikaacha mwili ghafra blogu hii itakuwaje kwani ni mimi pekee mwenye pasword pia mwandishi na mhariri!"

Kumbe sio peke yangu niliyekua najiuliza hivi. Happy 3rd Birthday kamalaluta.blogspot.com :-)

Kweli wengine tunasoma hapa then tunajificha lakini ujue you are an inspiration to starters like us. :-)

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

cheers!

na picha ya hao ulo nao ni akina nani? samahani kwa kuuliza....lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep, inapendea kujua kuwa kunawalifuata nyayo na kwakweli blog ni kitu cha ajabu.

ujumbe kufika au kutokufika sijui sana ila naona kama kazi yangu kubwa ni kutoa kile nilicho nacho kwa njia niwezayo ambayo ni blog the mengine yatafuata.

Chacha hao jamaa niwatatu kama blogu ilivyo na miaka mitatu!

chib said...

Umebobea katika kublog.

hongera sana

Mbele said...

Hongera kwa kudumu kwa miaka mitatu. Wahenga wanasema, kuishi kwingi ni kuona mengi. Ni wazi umejifunza mengi. Kila la heri.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Uwazi wako na kutokuogopa kusema ukisemacho ni mojawapo ya sifa zinazokupambanua na kukupa upekee. Nimejifunza kitu kikubwa sana na hasa jinsi ya kuendesha mijadala na kuvumiliana - kuendesha hoja kali na wakati mwingine kwa lugha kali isiyobembeleza - lakini mwisho mkakubaliana (kutokubaliana) na kuendelea kucheka na kuwa marafiki.

Hongera kwa kutimiza miaka mitatu na naamini kwamba hutachoka!

Tandasi said...

MUNGU ambariki kamala ampe mtoto amabaye atampa password ya hii blog kama mrithi in case kamala anaishi miaka mingi ijayo MUNGU mbariki kamala MUNGU wabariki wanablogu