Friday, November 27, 2009

kuna Nykakati choo cha uswahilini huwa bora kuliko hoteli

Samahani naomba kutoka nje ya mada leo. kumbuka kijiwe chetu kimekuwa kikijadili juu ya ndoa, sasa leo kidoogo tuone juu ya haraka za kwenda chooni kuliko jikoni, au chumbani nahata kwingineko, ni ugonjwa wa kuharisha aka mdogo wake kipindua pindua.

siku Moja miaka ya 2004 nikitokea Posta kwenda Nyumbani Mwenge, nilisikia tumbo linaleta za kuleta mitaa ya Moroko. nikavumilia na kumbuka silijui jiji, nikafikiri ntafika home. hali ikawa mbaya, nikashuka kituo cha Nyirenda A.k.a ITV na kukatiza mitaa ili niwahi kilipo choo. nikielekea nyumbani, nikaona no, hali ni mbaya siwezi kumwahi raifiki yangu mpendwa i.e choo. nikageuza na kuifukuzia baa ya Meryland iliyioko kituoni ili niende chooni. hapa natembea kwa kasi na kwa stairi za ajabu ajabu nikikata mauno. nikazuga kama naenda kaunta na kuelekea choooni.

ni soo, kuna mtu kajifungia mule, duh, nikasubili nikiwa nimesimama kama ile nina mguu mmoja ili kubana injini isishuke ghafra. jamaa akatoka na kunisalimia 'za sahizi' sssalama! nikamjibu nakuingia ndani. moyo uliburudika na nilifurahi saaana kukiona choo kile kichafu, nikakifanyizia na kubakiza zigo la nyumbani, si ni ugonjwa wa ghafra!

basi mdogo wangu EK ananipahabari yalivyowahi kumkuta mitaa ya mabibo na akaamua kuivamia nyumba asiyoijua ili aonyeshwe choo kilipo. anabisha hakuna mfunguaji, kilikuwepo choo cha nje, akajisevia na kukifurahia choo kile. alipomaliza hakuona mtu na kujiondokea zake.

sasa kali ni jamaa mmoja, kitu kimebana na injini inataka kutoka kwa njia ya kuharisha. jamaa kaona nyumba mbele yake asiyoifahamu, akaamua kuingia, alikatiza kwenye korido mpaka huani na kuwakuta wamama wanapika pika na kusukana pale, hakuuliza wala kusalimia, alikimbia nduki mpaka chooni.

alipokwishamaliza kukifurahia choo kile, akaanza kujishangaa jinsi alivyokatiza mpaka uani na kujua choo kilipo na soo ikawa ni atatoka vp mle, ila akatoka tu nakuwasalimia wale wamama ambao mwanzoni aliwapita bila kuaona na kuwaomba samahani kwa kuwainngilia, nao wakamuelewa na kumcheka, akafurahia kukifurahia choo.

somo; kuna nyakati choo huwa muhimu kuliko chakula. ukimuona mtu anakula chakula kitamu, fikiria masaa machache baadaye itakuwa ni uchafu, divi linukalo

3 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

ayaaaa!

lakini kweli...lol

chib said...

Aibu ya nini, hata kama ukibiga baruti huko chooni, ukitoka unasema ukweli, jamani uharo hauna brake kali. Kila mtu atakuelewa, kuliko kukaa kimya hadi ukatota.

mumyhery said...

mmhu!!