Monday, November 2, 2009

Maisha ya ndoa na ndoa yenyewe.Hivi ni kwanini watu wanaoana? Ni swali gumu. Wengi watakwambia wanatarajia kupata furaha,amani, upendo na ridhiko kutoka kwa wamuoaye, wengine watasema umri wa kuoa umefika na wengine watasingizia dini kuwa Mungu aliagiza kuwa tuoane.

Hata hivyo karibia 90% ya ndoa hazina amani, hazina upendo wala ridhiko na hazifai na zimebakia kuwa ndoano. Ni kamba au mnyororo wa kuwafunga na kuwalazimisha na kuwavutilia matatizoni.

Blog hii sasa imeamua kuanza kujadili juu ya ndoa. Huko Nyuma tulijadili juu ya tendo la ngono (wengine waliliita tendo la ndoa) na kujikuta kuwa tumesahau swala muhimu ambalo ni ndoa. Ukimuuliza mtu aliyejitambua kuwa ni kwanini kaoa au olewa atakwambia kuwa ni kwa sababu labda ya kupenda ngono au kampani au kuzaa au nini sijui na nakumbuka nilipomuuliza yule wangu aliniambia kuwa anapenda hicho kitamu zaidi.

Kwa nini ndoa ni ngumu na nini kifanyike ili zisiwe ngumu, ziwe nzuri, tamu na nyepesi? Waliojitoa kwenye ndoa na kuamua kwenda nje ya ndoa wamekuta kuwa hawawezi, walio waacha wenzi wao na kuwaoa wengine, wamekuta ubaya kuliko walikotoka na ni bora warudi kule.

Sasa ishu iko wapi na ninini kifanyike?

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ndoa ni kuvumiliana, kupendana,kuaminiana na kusikilizana. Huu ni mtazamo wangu!!

chib said...

Ndoa ni heshima ya mtu katika jamii akiwa katika mtiririko mzima wa kuhakikisha kiumbe binadamu anaendelea kuwepo kwenye sura ya dunia. Mambo mengine ni matokeo ambayo unaweza kuyaongeza au kuyaepuka. Ukiwa na ndoa kwa malengo mengine, basi hiyo si ndoa bali ni doa, maana umeshaondoa kiunganishi.
Ukiweza kusoma sentensi yote bila kupumua, basi ujue ya kwamba tafsiri yangu umeielewa. Sina zaidi

nyahbingi worrior. said...

hili swala labda walio ndani ya ndoa wajibu kwanza,sisi ambao bado tuvute muda kwanza.

Chacha Wambura said...

Nyabhingi, mimi ambaye niko ktk ndoa siwezi kujibu pia sasa si utaona kuwa hatutakuwa tunajitendea haki wenyewe?

nadhani mada imeletwa kwa waliomo na wasokuwemo...lol

uelewa wangu unanielekeza kuamini kuwa walio wengi ktk ndoa (mimi pia nikiwemo) tunaingia katika asasi/taasisi ya ndoa bila kujua nini tunakwenda kufanya/ku-contribute ama hata kujua ndoa ni nini...lol

na hapo ndo sarakasi inapoanzia...lol

Chacha O'Wambura said...

Yasinta, kupendana maana yake ni nini?

Yasinta Ngonyani said...

Chacha Wambura! Kupenda/kupendana sio jinsi unavyojisikia, kupenda/kupendana ni maono, hisia/kioja pia shani;mhemko.