Tuesday, November 17, 2009

Tangazo la vitabu online!

kwa taarifa tu ni kwamba, sasa nimechapa vitabu viwili online na cha tatu kinakuja.

kimoja kinaongelea juu wa namna kijana wa Africa anavyopaswa kufanya ili kujiletea maendeleo na bofya hapa kukiona

na cha pili kinaongela hazina ya kijana wa kizazi cha dotcom nacho bofya hapa kukipata


karibu mnunue, mjisomee, tuelimishane na kutunishiana mifuko na kuongezeana umaarufu.

kingine juu ya mauaji ya albino kipo njiani

6 comments:

John Mwaipopo said...

hongera kwa kuandika na kuchapisha. mie ntakutafuta uniuzie wewe mwenyewe kwa bei poa.

John Mwaipopo said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hongera sana Mulangira. Naahidi kuvinunua vyote na kuvisoma mara moja. Kazi nzuri!

masangu matondo nzuzullima said...

Kamala, nimeona hiki cha Kiingereza ni kurasa 12 tu lakini kinauzwa dola 17.60. Hapa kidogo mahesabu yanagongana. Ni kweli ni kurasa 12 tu au lulu.com wamekosea. Nijulishe.

Mbele said...

Ni mwanzo mzuri. Katika gazeti la KWANZA JAMII la wiki hii, ambayo niliiandika siku chache zilizopita, nimewahamasisha watu kwenda na wakati na kujichapishia vitabu wenyewe kwa kutumia tekinolojia hizi za kisasa. Kati ya mambo mengine, nimesema kuwa hii ni njia ya kujikomboa kutokana na kero za wachapishaji wengi wa jadi. Hongera sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@mwaipopo, nitafute, niko Bongo sasa.

@matondo, ni kweli ni kurasa 12 na ni chache sana kwani ilikuwa paper muhimu sana juu ya maendeleo ya Africa kwa vijana. ni kidogo lakini muhimu ila sema hao lulu ndio wanaopanga bei, sasa siui ila ukinunua kwa nia ya download, bei inapungua zaidi.

@Prof. mbele, kufanikisha uchapishaji wa vitau hivi kunatokana na juhudi zako wewe mwenyewe kwa kunifundisha bloguni na kwanza jamii