Saturday, November 7, 2009

Tunaendelea na ndoa.

Ni baada ya harusi na ujinga mwingine wowote ule. Sasa mishawasha na kujionyesha kumeisha kwa siku ya harusi na kumtambulisha yule mliyeoana na sasa maisha yanaanza kama kawaida yake na kawaida iliyokuu ni kwamba ili maisha yetu yawe na maana ni lazima changamoto ziweepo na bila hizo, maisha na ndoa zetu hazina maana na labda hazihitajiki.

Tulipotegemea raha tunaanza kutatizwa. Na badala ya kusimama kwenye nafasi zetu, tunakaa pembeni na kuwaita wengine ili waje kumaliza matatizo yetu utadhani ni yao na wao wakija kazi kubwa ni kusimamia upande wao na kuuponda mwingine kwamba kama ulienda kwa ndugu wa Mume, basi watavutia upande wao na wakike hivyo hivyo. Hata hivyo tuyaitayo matatizo sio matatizo bali ni changamoto tu

Kwa mfano; baba yangu alioa wake wawili kwa nyakati tofauti na hakuweza kuisha na mke hata mmoja. Baba alimwoa mama wa kambo au mke wake wa kwanza na kuzaa naye watoto watatu, baadaye mambo hayakwenda sawa, wakafukuzana na kumwoa mama ambaye pia niliambiwa kuwa walifukuzana nikiwabado mtoto mdogo na wa mwisho nikiwa nina siku chache hapa duniani kama mwaka au pungufu.

Nilijaribu kufuatilia kilichompelekea baba kushindwa kuisha na mama au mama wa kambo na kwa bahati mbaya baba aliisha kufa na hivyo sikuweza kusikua hilo kutoka kwake. Nikiwa nimelelewa katika familia ya upande wa baba niliweza kumsikia mama yake baba (bibi yangu) akiwalalamikia wale wake zake baba kuwa walikuwa watu wa ajabu wasiofaa kuolewa na baba. Mashangazi pia walilalamika, unashindwa kujua nani alioa baba, bibi au nduguze?

Pamoja na kwamba mama alitoka kijiji jirani sana na pale nyumbani, sikuwahi kuambiwa kuwa kuna mama na kuna shangazi niliyedhani ndiye mama. Nilipokuwa mkubwa na kuanza kuongea na watu wa nje, ndo nikaaza kuambiwa habari za mama yangu. Baadhi ya watu walilia machozi kuona simfahamu mama na nduguze

Daima bibi na mashangazi zangu walinisimulia ubaya wa wake za baba akiwemo mama utadhani sio mama yangu na waliniambia mpaka matusi makubwa na sijui lengo nini na nikijaribu kuamini kuwa labda mama ni mbaya japo alinizaa. Niliona kasoro moja ambayo ilikuwa ni kunizuia kumwona mama au nduguze na nikajiuliza ni kwanini wasiache nijionee huo ubaya??

Kama mtoto nilikuwa ‘victim’ wa maamuzi yao kiasi kwamba nilikuwa najiuliza mama ni yupi kati ya wanawake wote niliokuwa nakutana nao njiani. Ukafika wakati nikaweza kumwona mama wa kambo na baadaye mama. Wote kwa pamoja waliwalalamikia bibi na mashangazi zangu (mawafi) juu ya ndoa na sio baba! Nikashangaa.

Nikienda huku naambiwa hivi na huku hivi. Bahati mbaya baba alikwisha kufa ila nikashangaa wake zake baba wanawalalamikia mawifi na mama mkwe na sio mume. Nikajumuisha maongezi na kugundua tatizo kwamba baba aliwaamini sana nduguze na kuwaeleza kila kitu na kuwaomba wasaidie kusulushisha au aliacha maisha yake binafsi na ndoa yake mikononi mwa watu wengine

Hilo ni sehemu ya tatizo la ndoa. Kutokuwa sisi na kuona changamoto kama matatizo makubwa na kuwaomba wengine waje kusuruhisha. Kufanya hivyo ni kuigawa ndoa na kujiletea matatizo kwani katika jamii zetu hizi za kiafrika au kama binadamu wenye uhai, ni lazima kutakuwepo upendeleo na ubaguzi wa kumwona auliyenaye kuwa ni mtu mbaya kwani sio ndugu yako.

Hii ni hatari na wanawake ndio waathirika wakuu. Inafika hatua mwanandoa wako haonekani kama mtu na wewe unamdharau kwa ubadguzi na kuona mabaya yake kuliko mazuri utadhani unaweza kuishi na ndugu zako wakawa kama yeye. Hii ni hatari sana kwa ndoa.

Upatapo matatizo katika ndoa, jambo la kwanza ni kwa kusuruhisha na mwanandoa mwenzio. Jinsi ya kusuruhisha ni kukaa kwa muda na kuongelea tatizo kwa kusikiliza kwa makini. Ikiwezekana mwondoke nyumbani na kwenda mahala patulivu na kuongea vizuri.

Msipoelewana basi tafuta mshauri. Mshauri awe ni yule unayemwamini na asiyekuwa na upendeleo, atakayewasikiliza na kutunza siri, ni vyema asiwe na uhusiano (hasa wa damu) na familia ya mke au mume. Ndugu zako na wazazi wako (wa mke/mume) wanaouhuru wa kutoa maoni lakini usiwape sana nafasi kwani wanaweza kuja na upendeleo au hata wivu.

Matatizo ya kindoa huathiri zaidi watoto wasiohusika kama mimi nilivyoathiriwa kiasi chake. Lakini uhai wa ndoa umo ndani mwako.

Ni hayo kwa leo, barikiwa na mjadala unaendelea

9 comments:

Chacha o'Wambura said...

mh! ndoa ndoano...lol

naona kama maigizo vile! Mt Simon wathemaje vile?...lol

pengine nina-maanisha 'MPENZI nahisi inabidi NIKUOE na nalazimika KUKUPENDA kwa kuwa nimpendaye kikweli SIWEZI KUMPATA!:-(" ...lol

Mzee wa Changamoto said...

Dah!
Ni kweli kaka. Kinachosahaulika hapa ni kuwa NDOA inahusisha KUONGEZA NA KUPUNGUZA MENGI KUHUSU MAISHA YAKO. Kama ulikuwa ukiishi hivi, itabidi upoteze angalau nusu ya UHURU wa konakuungana na wa mwingine ambaye naye anastahili kupoteza nusu yake ili nyote muunge nusu zenu kuwa kamili. Ndio maana ndoa za wale ambao hawataki kubadilika baada ya kuoa hazidumu. Wale wanaotaka kuendelea kuwa na marafiki wote waliokuwa nao, kuwa na muda kiasi kilekile na familia zao, kuwa na mitoko ileile na kuwa na maisha kabla ya ndoa. HAIWEZEKANI kwa kuwa sasa si wewe, bali ni ninyi.
Nashukuru kuwa NIMEJIFUNZA MENGI hapa na MJADALA UENDELEE
Blessings

Nuru Shabani said...

Duh!Pole sana.
Ndoa nyingi sana zimekuwa zinaendeshwa kwa "remote".Kuanzia watu wanapotafuta wenzi wa maisha yao jamii huwa imeweka vigezo ambavyo sio halisi mume mzuri ana sifa kadha wa kadha halikadhalika na mke.Baada ya ndo kinachotokea ni kulazimisha kuishi kwa kufuata vigezo vya jamii kitu ambacho wanandoa wengi huwa hawawezi kwani hapo ndipo kuna maisha halisi.Mi ninadhani kuna haja ya watu kusimama sisi kama sisi bila kusikiliza jamii inasemaje.

Mzee wa Changamoto said...

Jingine nililogundua kuhusu ndoa ni kuwa watu wanapokuwa hawajaingia kwenye maisha ya ndoa, huwa wanaifikiria mpaka siku ya harusi. Pengine mpaka Honemoon na mawazoni mwao ni ile taswira ya UFAHARI NA SHAMRASHAMRA inayokuwepo. Taswira za vikao vya harusi na kutembelewa kujua maendeleo. Taswira za shopping ya harusi na namna ambavyo kila mmoja anajitahidi kuonesha anajali katika kuwasaidia kutengeneza harusi yenu.
Kutokuwa na TASWIRA ya nini kinaweza kufuata baada ya siku ya ndoa na honeymoon ndio tatizo kwa wengi na ndio maana wenye ndoa za kifahari saaana ambao hawakutazama "kitakachofuata baada ya sherehe" huingia kwenye misukosuko muda mfupi baada ya hapo kwa kudhani wametengwa na kutothaminiwa na kuanza kutafuta ushauri wa kila kitu mahala pasipostahili.
Pengine wanaofunza kuhusu ndoa wangewekeza kwenye MAISHA BAADA YA SHAMRASHAMRA ZA NDOA maana yaonesha ndilo likosekanalo.
Blessings

Anonymous said...

I found this site using [url=http://google.com]google.com[/url] And i want to thank you for your work. You have done really very good site. Great work, great site! Thank you!

Sorry for offtopic

Anonymous said...

KAMA NI MAFUNDISHO TUMEYAPOKEA NA NI MAZURI SANA,TATIZO WATU TUNAOPATA MUDA WA KUPEKUA KWENYE BLOG NA KUJISOMEA NI WACHACHE MNO.
KAKA KAZA BUTI

Tandasi said...

haya mabo hayo! mjadala huu una mashiko, lakini nyie wajuzi mna ndoa imara nyie?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Tandasi, sijui nikujibuje. lakini nayaishi yale ninayoaandika na siyatoi kwingine bali najaribu kuangalia ndoa nilizowahi ona au ishi karibu nazo na vile nifanyavyo, na mawazo ya wanakijiwe

SIMON KITURURU said...

@Kadinali Chacha: :-)