Friday, November 20, 2009

Tutafute pazuri katika ndoa zetu.

Tumeona juu ya migogoro katika ndoa na visa na mikasa vya kukaribisha sijui nani ili asuruhishe huku wakiwa na upendeleo na hivyo kuharibu zaidi. Kumbuka pia migogoro na kuvujika kwa ndoa huathiri watoto zaidi wasiohusika na migogoro ile kama nilivyojitolea mfano mimi mwenyewe.

Basi ukifuatilia vile visa na vikwazo katika ndoa, huletwa zaidi na kufikiri kwetu kubaya, kutazama pabaya zaidi badala ya pazuri. Kufikiri huku huanzia mbali, huanza tukiwa wadogo, wakati wa uchumba na mara nyingine siku ya ndoa yenyewe. Tukiwa wadogo huwa tunaonywa juu ya uwezekano wa kupata wenza wabaya au kuwafanyia ubaya kama vile kuwapiga, kuwasaliti nakadhalika.

Shamra shamra za ndoa huambatana na maonyo juu ya uwezekano wetu wa kuwapiga wenza. Kwa mfano siku ya harusi, mwanaume huambiwa maneno kama, usimpige, na mwanamke huambiwa asimzarau na kumuuliza ni mwanaume gain wewe. Basi hakuna neon hata moja la kusameheana, kupendana na kutendeana wema. Na sisi huendelea kuangalia mikanda yetu ya ndoa na kurudia rudia jumbe hizi na kuwa kweli

Katika ndoa zetu tunafikiria mabay ya wenzetu na kuyapa kipaumbele na kuanza kuona kama hawafai na hawana msaada wowote kwetu na kwa hiyo tunapaswa kuwatendea ubaya. Hii ni hatari kwa ndoa zetu. Hata kama mwenzetu anamakosa namna gani, kumbuka bado ni mwenzetu, tujkiagalia upende mzuri, tutaona ni kwa kiasi gani ni mzuri na muhimu kwetu. Vinginevyo tutakuja kujutia matokeo yetu ya kuangalia upande mbaya.

Mitandao ya kupigania haki za wanawake, hupendekeza wanawake waachane na waome wakorofi badala ya kuwasaidia kubadilika. Wengi wa wanawake walioacha nyumba zao walikuja kujutia baadaye na wanaume kuteseka wakati mambo sio rahisi kuyarudisha nyuma

Tukumbuke pia kwamba kama tunaona ubaya kwa mwenzetu basi sisi tunaweza kuwa sehemu ya ubaya huo. Kuangalia upande chanya wa wenza wetu ndio mkombozi wetu. Tuwe huru katika hili bila kufungwa na jamii wakiwemo wazazi na ndugu zetu. Tunapodhani wenza wetu wana ubaya, basi suruhu ni kushirikiana nao ili kuushinda huo ubaya. Tusipofanya hivyo, basin a sisi tunakuwa sehemu ya huo ubaya na kuukuza na wakati mwingine sisi ndio chanzo cha huo ubaya tunaouona kwa wengine.

Kumbuka ndoa ni lazima iwe na changamoto na dawa ya changamoto ni kuzipokea na kuzikubali ili kuzikabili salama. Vinginevyo ni kushindwa na kuishia kubaya. Sisi ndio msingi ya mafanikio ya ndoa zetu. Furaha, amani na ridhiko katika ndoa zetu, vimo ndani mwetu na sio nje yetu.

Swali, mada ijayo tuongelee nini kati ya tendo la ngono katika ndoa na kuasidiana majukumu ya kila siku ya nyumbani?

2 comments:

chib said...

Inabidi utunge kitabu kwa faida ya wale wasiosoma blogu, au unasemaje. :-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Chib, labda nitafanya hivyo. inafuatana zaidi na wasomaji mnasomaje, pia nimechapisha vitabu online, umeshanunua kimojawapo?