Monday, November 16, 2009

wewe kamala, Umefunga ndoa??

katika maisha yangu ya kila siku na siku zangu hizi za mwisho mwisho katika jiji hili la Dar es salaam huwa napenda kupitia katika eneo la kanisa moja na kupata chai na yule ninayejiaminisha kumpenda.

basi kuna rafiki yangu wa siku nyingi na huyu sio rafiki bali ni 'wanyumbani' yaani ni kama jirani kule kijijini na kamwoa binti jirani kule kwetu. tunaishi maeneo yale yale hapa Dar. sasa leo asubuhi kama vile alijua kijiwe hiki kinaongelea juu ya ndoa, akaniomba samahani na kuniita pembeni mimi na yule nimpendaye kwa kutuomba radhi kwa muda wetu.

basi akaanza kuninonogoneza, hivi wewe kamala una mpango gani na mwenzio huyu? mumefunga ndoa? kabla sijajibu, akamuuliza yule niliyekuwa naye, unajua dada mimi nataka kukusaidia maana hawa vijana wa siku hizi........

nikamwabia kuwa sisi tuliishafunga ndoa ya moyoni na ile ya kimila sikunyiingi sana na ndio maana natumia salamu ya kihaya kwa waliooa yaani Shumaalamu waitu! jamaa akashangaa! nikampatia nafasi kwamba kama anataka kutufungisaha ndoa, nakwa kuwa yeye ni makatoliki mwajiriwa wa kanisani, hamna shaka, aniite nije na atufungishe ndoa, lakini asianze matangazo maanake mimi ninasafari nyingi kwa hiyo kuniwekea matangazo harafu tarehe ya tarehe sipo au niache dili kisa? ndoa,

basi bwana, jamaa akashangaa kuona na mke wangu ananisapoti. kwao ndoa ni kanisani na ni kwa padri ili watu wote waone na washuhudie, nikamwabia yangu ni ya kimila na ni ya moyoni zaidi. alishangazwa na majibu yangu na kubakia anacheka yeye mwenyewe. yaaani kacheka kwa mshangao mpaka tukatokomea mbali

mjadala utaendelea.... lakiniwewe unasemaje?

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Shumaalamu waitu! Hongera kwa kufunga ndoa ya moyoni. Nadhani hiyo ni nzuri zaidi safi sana Kamala.

Nuru Shabani said...

Nadhani wengi bado tuko kwenye lile tatizo la kutaka jamii itukubali kabla ya sisi wenyewe kujikubali.Ndiyo maana utakuta watu wanahangaika kufanya sherehe kubwa ya mamilioni ya pesa kwa kitu cha siku moja tu.
Safi sana kamala.

fred katawa said...

kamala naanza kuhisi una mapungufu ya kufikiri,hutaki ndoa kwa sababu huna pesa na huna marafiki watakaokuchangia kufanikisha ndoa ya kifahari ndo maana unajifanya kutoipenda sherehe ya ndoa.

Wewe kamala unajifanya kutopenda kuzungushwa na gari mji mzima na bibi Arusi siku ya ndoa?

Hupendi kutumia milion kumi kwa sherehe halafu ukapata raha ya kudaiwa baada ya ndoa?

Sema tu umechoka huna mahela ya kutanulia

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

katawa, mmoja wa marafiki wanaoweza kunichangia kiasi kikubwa cha pesa ni wewe, sasa utasemaje sina marafiki? hata nikidaiwa, wewe si upo?

harafu sikuonage faji wewe!