Tuesday, December 15, 2009

nawowa jamani nafunga ndoaz

kuna mijadala miingi kuhusu ndoa, kufunga ndoa na harusi katika jamii yetu. kwakuwa naishi katika jamii, nimejikuta nami nikipaswa kufunga ndoa ya kanisani kwani kumbuka kanisa sio baya na nizuri.

basi weekend hii jpili saa 7 mchana, mimi na my beloved waifu tutavaa nguo mpya na kwenda mbele ya hadhira na pasta ili tuvalishwe pete na kukla viapa kidogo nakiasi katika kanisa la KKKT pale posta.

wanablogu woote mnakaribishwa. kutakuwepo na kijisheree kidogo tu na hakuna mchango wala nini kwa wanaojisikia njooni tu.

tumelazimika kufanya hivyo baada ya wife kupata kazi anayoipenda katika KKKt na hivyo hawezi kuajiriwa nakuzaa bila kufunga ndoa kwani itakuwa muujiza huo.

NB; Chacha Wambura ndiye atakuwa bodyguard wangu siku hiyo

15 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

mbona maryamu alizaa bila kufunga ndoa....lol?

umesema utavaa nguo mpya je mie mwenye nguo kuukuu a.k.a za mtumba naruhusiwa?....lol

nitumie tiketi basi toka musoma nije kwani ningekuwa nimechanga ningekuja nikomelee finyango na ze ugimbi ulotokana na mchango wangu....lol

Anonymous said...

KAKA MIE NAKUTAKIA KILA LA HERI, UMEAMUA VYEMA KWANI TOFAUTI NA HAPO WIFE HANA JOB KWA TARATIBU ZA WA-KKKT.

Yasinta Ngonyani said...

Kamala umefanya uamuzi wa busara sana nakutakieni maisha mema ya ndoa wewe na mtarajiwa mkeo (wifi) yangu. Karibu sana kwenye maisha ya ndoa pia nawatakieni muwe wazazi wema. Ila nasikitika sana sitaweza kuja ungesema mapema kidogo sasa ghfla hivi au ulitaka nisije nini...lol.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

TANGAZO: mmeambiwa kuwa miye ndo ntakuwa bodigadi...hivo mkibugia ze ugimbi na mkaleta fujo hapo patakuwa hapatoshi kwani ntakuwepo kuhakikisha usalama wa Bw/Bi harusi kabla hawajaenda KUJIPUMZISHA....lol

Koero Mkundi said...

Kamala, if you want do do something, just do it, and dont Camouflage with an excuses...LOL

Hivi Adam na Hawa walifungishwa ndoa na nani vileee...naomba kukumbushwa wajameni

Anya way nakutakia ndoa njema japokuwa siamini kama itakuwa ni takatifu maana huenda mmeshaonjana kabla. Si unajua tena mpaka ujue ladha...LOL

Nisalimie mtarajiwa wako aka Wifi yangu mtarajiwa

wavuti-nukta77 said...

Nakutakia heri na furaha na mafanikio tele katika siku hii yakufunga ndoa na katika kuanza maisha ya ndoa!
Salam za heri rafiki mwalimu!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hili ni jambo jema. HONGERENI na kila la heri! Mpaka kifo kitakapowatenga ati!

SIMON KITURURU said...

HONGERA wajameni !

Hili swala labda lingekusumbua HAPO baadaye kupata kura za WANA KKKT wakati ukigombea URAIS .

Si unajua tena KIBANO cha jamii kinabana kama unaihitaji jamii?:-(


Naacha nikiendelea kutafakari maswali ya DADA KOERO.

chib said...

Hongera sana. Upate baraka mpya.

Candy1 said...

Hongera kaka, nakutakia kila la kheri katika "steji" hiyo ya "maisha"...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Nawashukuruni kwa pongezi zenu. Koero Adam na Eva walivua nguo na kuanza kazi bila kifungo na wenyewe wanadai mungu alikuwa shahidi wa kwanza.

kuonjana? si tunaonja kwa mdomo kwa hiyo unamaanisha busu au?

anyway ndoa ya kweli ya Moyoni tuliifunga muda mreefu uliopita ni karibia miaka miwili. ila kuna suala la ajira ya wife hapa harafu kuna suala la kuwa mwanasiasa, therefore ni maandalizi yakukabiliana na jamii tunamoishi au sio?

Chacha ucje na viboko vyako wala mawe, hapa sio musoma wewe

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@KL: mawe na viboko suna mzee kwani huo ubodigadi mpaka mtakapokwenda kujipumzisha unadhani utakuwaje?....lol

Cheers

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Vita ni vita Murrah, ucje ukaanza kurusha mawe kama signal ya ulinzi Imara ehe

Mzee wa Changamoto said...

Labda huu ni wakati muafaka wa kumalizia HABARI yangu kuhusu KAPERA KAMALA kabla hajaoa. Na kwa kuwa unaoa JUMAPILI, basi Ijumaa nitakuwa na KAPERA KAMALA KWA MARA YA MWISHO BLOGUNI.
Na atakuwa pale kama andiko na si mtoa maoni.
Hongera zangu zitafuata huko
Blessings

mumyhery said...

hongera Kamala kilala heri