Monday, December 7, 2009

Ndoa, kwanini kuzaa watoto?

katika mijadala tumeoina mengi na baadhi, sasa leo tuone juu ya uzazi wa watoto katika ndoa. kwanza kabisa kuna wazazi wanaowalingia watoto wao juu ya kuwazaa, utasikia mzazi akimwambia mtoto kuwa wewe, nimekuzaa, nimekulea na kukusomesha. wazazi kama hawa wanashindwa kujua kuwa hakuna aliyewahi kuomba kuzaliwa na kuzaa kwao ni matokeo tu ya vitendo vyao na wala hakuna aliyewahi kuomba kuzaliwa.

uzaaji wetu ni matokeo ya matendo yetu na hasa ngono. inashangaza baadhi ya watu wanafanya ngono na kuogopa matokeo (mimba), kwa hiyo kama wewe unafanya ngono basi kuwa tayari kukubaliana na matokeo yaani kuwepo kwa mimba au kutokuwepo pia.

wengi huchukulia watoto kama tunu, heshima na kadhalika na wengine hufikia wakati wa kudai watoto au kuwatafuta kwa nguvu yoyote ile na wanasahau kuwa watoto ni matokeo tu ya matendo yetu. wapo pia wajaribuo kuzuia mimba au hata kuharibu mimba ili wasizae.

ila kwenye ndoa tunapaswa kuzaa watoto kwa sababu tu ya kukamilisha kanuni ya utegemezi. kwamba kama binadamu tunahitaji mama, dada. tunahitaji demu (girl friend). tunahitaji mke nk. kwa hiyo ni lazima tuzae ili na wengine waweze kuwapata kupitia sisi japo kila azaliwaye huja na mikakati yake, malengo na mitizamo yake.

kwa hiyo sisi kazi yetu ni kuwaleta duniani, kuwapa malezi mpaka pale watakaposimama wenyewe na kuishi maisha yao.

ndoa ikikosa watoto sio ishu japo wengine huanza kujiona kama wamelaaniwa na kwenda kuombewa ili wapate watoto. wanasahau kwamba sio lazima hata kidogo wakati mwingize kuzaa watoto. kuna waliozaa watoto na wanajuta kuwazaa na hivyo labda ni bora kutokuzaa wakati mwingine. kwa hiyo wanapokuwepo tuwapokee, tuwalee na kuwaacha wawe wao kwani kanuni ya utagemezi imekamilishwa.

watoto sio wa baba wala mama bali ni wao wenyewe na wanajimiliki wao sio mtu mwingine kuwamiliki. tusijifunganishe nao kupita kiasi, wanamaisha yao, mapenzi yao na uchaguzi wao pia

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala umenikumbusha mbali sana. Hii ya kutopata watoto ukiwa umeolewa/0a, watu au ndugu wanataka mkishafunga ndoa tu basi vifaranga vionekane uwanjani la sivyo wanaanza mwanamke huiyu hafaai au mwanamke huyo kalogwa. nk, nk. Huwa nashangaa sana watu waingiliao maisha ya watu wengine. "watoto sio wa baba wala sio wa mama" umenipa tafakari ambayo naendelea kutafakari...

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

watoto ni lazima kwa mujibu wa WAKURYA...lol

kama huzai...get lost...lol