Thursday, December 17, 2009

ndoa ni ndoano, ni kifungo?

kijiwe hiki kilikuwa kikiongelea masuala ya ndoa kwa muda mrefu na imefika hatua ya mwanakijiwe kufunga ndoa. ukweli ni kwamba mwanakijiwe ni mwanandoa wa muda sasa ila ameamua tu kufunga ile ya kanisani na hivyo ana ka-uzoefu katika masuala haya.

basi nilihudhuria mafundisho ya ndoa kanisani. wanafundisha vitu vya ajabu kidogo. mzee mmoja aliniambia kuwa maana halisi ya ile pete ni upendo unaozunguka, hauna kikomo eti.

sasa mafundisho tukaambiwa ya kuwa tunaapa ili tukitaka kuachana turejee (hasa wanaume) kwenye kauli zetu za viapo. katika mafundisho yale linaongelewa zaid suala la kuachana, kugombana na 'negatives' nyingine badala ya positives.

kwa utafiti wa kiutambuzi usio rasimi ni kwamba, ndoa nyingi zinashindwda kuendelea kwa sababu ya baadhi ya maneno wakati wa kufunga ndoa hizo. kwa mfano MC anasema, 'usiende ukampiga' au wazazi wanasema 'mwangalie binti yetu hana hata kovu' au usilewe pombe na kurudi usiku ukamtwanga au usiende nje ya ndoa eti kazeeka au sio mtamu tena!!!

maneno haya na mengine mengi yanasemwa tukidhani twatenda vyema. kumbuka ....as you think, so you become! wanandoa wakiangalia mkanda wa video wa harusi na kusikiliza maneno hayo, huwajaa akilini na baadaye kuwa vitendo na ndio maana ndoa nyingi huishia kubaya.

tuwe positive na kufuta negatives katika ndoa zetu jamani au sio?

suala lingine tumeambiwa ya kuwa Mungu ndiye wa kwanza kufungisha ndnoa kuwa eti alimpatia Adam Eva /Hawa na eti hawa alitoka ubavuni mwa mwanamke!! labda iko hivyo kwa sababu bible iliandikwa na wanaume. mimi daima nashuhudia wanawake wakitubeba tumboni na kutuzaa tena kwa kupitia ukeni. wanatubeba na kutunyonyesha harafu wanatupatia mapenzi na mara nyingi wanaume hulala kwa juu. sasa nani anatoka katika mwingine?

anyway, welcum 4 wedding

4 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Ati nani anatoka kwa mwingine ama nini kinatoka kwa mwingine....lol

labda na wanaume wanazaa kimawazo...lol

na mawazo ndio muumbaji...lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chacha, kama mwanamke ni shamba basi mwanaume ni mkulima / mpanda mbegu. si tunapanda?

Markus Mpangala said...

ni ajira kuu kuliko zote ulizowahi kuzifanya

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@markus ????????? unapanda na kupanda na kupanda au?