Thursday, December 24, 2009

neno la ndoa tulilosomewa hili hapa

Wakolosai 3:1-25
Wakolosai 3
Maisha Mapya


1Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa Mungu. 2Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani. 3Kwa maana ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu. 4Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo na ninyi mtakapoonekana pamoja naye katika utu kufu.
5Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu. 6Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. 7Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha yenu ya zamani. 8Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu. 9Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake 10na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake. 11Katika hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru. Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. 12Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13Vumilianeni na kusameheana kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha kuwasamehe. 14Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu.
15Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Wajibu Katika Familia 18Ninyi wake, watiini waume zenu kama inavyopasa katika Bwana. 19Ninyi waume, wapendeni wake zenu wala msiwe wakali juu yao. 20Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii humpendeza Bwana. 21Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa.
22Nanyi watumwa, watiini mabwana wenu wa hapa duniani katika mambo yote; fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu, na wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatazama. 23Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na siyo wanadamu. 24Kwa maana mnafahamu kwamba mtapokea urithi wenu kwa Bwana kama tuzo yenu.

9 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa habati mmbaya hatutaweka picha yoyote hapa kijiweni!!!!

ndoa ilikuwa ni ya kiafrica zaidi tofauti ni kuwepo kanisani na mchungaji wa kisasa badala ya mkuu wa mizimu

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kamala
Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
Baraka kwako

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Kamala, huo ni uchoyo...lol!

umetunyima wengine finyango za nyama na ugimbi....na picha pia? Duh!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"kwa habati mmbaya hatutaweka picha yoyote hapa kijiweni!!!!"

Kwa nini?

Muwe na safari njema pamoja.

Nimelipenda hilo neno japo sina uhakika kama mtu wa utambuzi kama wewe unakubaliana nalo.

Mbarikiwe DAIMA!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Kijana wa C/moto, na kwako pia uaminiye katika hilo. Chacha define uchoyo!##

matondo, nilichogundua juu ya maneno ya biblia ni tafsri. kwa hiyo ukitafsri vyema linakuwa la manufaa kwako ila ukiwa negative na uoga wa sijui nini basi ni soo mkuu

anyway, tunaishi katika jamii na lazima tuenende kijamii wakati mwingine

Masangu Matondo Nzuzullima said...

"...anyway, tunaishi katika jamii na lazima tuenende kijamii wakati mwingine"

Maneno ya busara sana haya. Natamani kweli kama yangewafikia "walokole!"

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo tatizo la walokole wao hujiona sahihi, wajuaji na wenye mamlaka ya kukosoa na hata kukemea. laiti wangelijua ya kuwa ulokole wa kweli ni kuishi vyema ili wengine wavutiwe na wema kuliko kupiga kelele na kuudhalilisha ulokole, maisha yangekuwa mazuri zaidi na walokole wa kweli wangeongezeka nakwambia

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@ Matondo and Kamala: Jinsi unavowaona wasivo sahihi ndivo nao wanavowaona wanautambuzi wasivo sahihi!!!!!!!!!!!!

inakuwa shida saaaana tunapowadhania wenzetu yale wanayotudhania pia, eti eh!!!!

ninaanza kupata wasiwasi kuwa pengine tusipokuwa makini basi msigishano kati ya watambuzi na wasokuwa wanautambuzi patakuwa hapatoshi na kuanza kupeana majina kama bundi a.k.a 'ginhi' kwa kiwetu kule bariadi nk....lol

Tandasi said...

ndoa ndoano lakini kwa wanautambuzi nadhani itakuwa na mashiko tu