Tuesday, December 15, 2009

nilifukuzwa shule kwa kosa la kusikiliza redio

leo kijana wa Changamoto amenikumbusha kitu cha ajabu ambacho ni kufukuzwa shule kwa muda (suspension) nilipokuwa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Tweyambe kwa makosa mawili moja ni la kumjibu 'hovvyo' mwalimu na jingine ni la kusikiliza redio.

ilikuwa ni siku moja miezi kama miwili tukikaribia kumalizia masomo kwa kufanya mtihani wa mwisho wa taifa maarufu kama neshono (national). akatokea mwalimu wa Bweni aitwaye Lukongwa, akatuzuia kupata chakula cha jioni mpaka tufanye adhabu fulani. nilimsihi atuachie ili tupate chakula tukajisomee ili tuweze shinda mtihani nakuwa na maisha mazuri kama ya kwake.

mwalimu yule akanisema kwa kichwa master (head master) na kumwomba nifukuzwe. nilijitetea kuwa sikutoa tusi bali ni ombi la kusoma ili tumalizie masomo yetu salama. kichwa master alinikatalia kuwa alikuwa siku nyingine akinikuta nasikiliza kiredio changu chamkulima. nikamwambia kuwa huwanasikiliza BBC, VOA ili nijipatie taarifa zaidi. Kichwa master akanikatalia na kusema ni kosa na hivyo nastahiri kufukuzwa kwa Muda.

nikafukuzwa. hivyo basi, upenzi wangu wa VOA uliwahi kuniponza. na sijui kama mpaka sasa ni kosa kusikiliza redio pale shuleni au la na nitafatilia

2 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

bila shaka ukionana na kichwa masta hutokasirika....lol

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kulikuwa na sheria nyingi za ajabu ajabu wakati ule. Kulikuwa na sababu gani kukataza wanafunzi kusikiliza redio wakati redio iliyokuwa inasikika kwa muda wote ni RTD? Hii si ndiyo ilikuwa nafasi nzuri ya kueneza propaganda na fikra sahihi za mwenyekiti wa nani hii?

Pale Kahororo sheria ambayo ilikuwa inazingatiwa sana ni ile ya "SPEAK ENGLISH" Hii nayo nilikuwa naiona kama muujiza kwani tulikuwa hatufahamu Kiingereza na sijui tungewezaje kuongea lugha ambayo hatuifahamu. Basi watu wengi tulikuwa tunaishia kukaa kimya tu ili kuepuka adhabu.