Thursday, December 10, 2009


unadhani huyu aliyekaa ni nani?, waliosimama ni Andrea wa Ujermani, Adam sijaona wa dar, na mimi nimepiga magoti kitandani. jamaa aliyekaa ni mwenzetu katika uwanja wa blogu na weng

i htamani kumwona. picha ni ya Sant balijit Singh wa santmat meditation katika ku-convey initiation jijini Mwanza. kwa atakaye mjua, zawadi nono yatolewa, Amina

6 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

huyo alokaa anafanana na mwinjilisti fulani vile ambaye nimemsahau jina...lol

hapo mwanza mlikuwa ndani ya nyumba ama nje? lol

halafu ni zawadi nono gani hiyo mbona husemi?

Mzee wa Changamoto said...

Kwa mara ya nne naiangalia hii picha na nimeamua kuKUBALI YAISHE
NIMECHEMKA.
Lol

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Mzee wa Changamoto, pole kwa ku-boil....lol


labda umpe mji...lol

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

halafu uki-zoom hiyo picha ikawa kubwa huyo mjamaa ana macho mekunduuuu kama pilipili...lol

Akifika shinyanga atakuwa kitoweo cha mapanga yanayocharanga wachawi a.k.a wanga wenye macho mekundu...lol

Eti Kamala, jamaa ni mganga wa kienyeji?....lol

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti - ni lazima uturushie madongo Wasukuma namna hiyo? Huyu bado kijana na hivyo mapanga hayatamrarua. Kamala sema basi, huyu jamaa ni nani?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@ Matondo: hilo si dongo bali ndo ukweli...lol

kwani wapi tena uliposikia vibibi vinacharangwa mapanga kwa sababu ya vimacho vyekundu kama siyo ukanda wa ziwa katika KABILA kubwa?...lol

kama unastuka ina maapia kuwa unakubaliana na dhana hiyo ya kuwa vibibi hivo ni vichawi?

ni vijimambo tu baba Zofa....lol