Monday, December 28, 2009

utamu wa dafu wakuu

kwanya likatwe, unyweeee harafu lichokonolewe, mkuu utafune mpaka basi. Mambo ya kuchokonoa haya.

7 comments:

Markus Mpangala. said...

kazana ulichokonoe, ili lijichonoke vema. Pozxi BOMBA HILOOOOOOOOO mtu mzima, UNAWAZA WIFE AU?????????

Mzee wa Changamoto said...

Nimependa saana vazi hilo. Nitahitaji kujadili lipatikanapo na lipatikanavyo.
Naona pete kwa mbaali inang'aa. Hivi ni kwanini waivaa? Ina maana yoyote katika kuboresha ndoa? Naamini yangu iko moyoni. Nahisi pete ni kama ilivyo mambo ya Krismasi vileeeeeeeeeee. Yaani wanazivaa wasipojua umuhimu wake na wakienda kusaka kimada wanazinyofoa.
Nadhani tafuta PETE YA MOYONI KAMA YANGU ili uwe nayo milele.
Lol
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Naona umekaa ki-yoga yoga, au niseme kitahajudi tahajudi. Na bonge la pete tena jipyaaaa linameremeta mkononi. Na hilo vazi - maisha yamenoga eeh. Yaonekana kama vile umevuka kwenye kifundo na sasa umeingia ile sehemu laini yenye utamu. Hongera!

Kuna kafununu fulani nilikasikia zamani eti madafu hayo yanachangia sana katika ueneaji wa MABUSHA hiyo kanda ya pwani. Kwa hivyo jihadhari!!! Bila shaka huu ni utani kwani nanukuu "One cup-full of coconut water contains more electrolytes than most sports drinks and more potassium than a banana" Tazama hapa kwa habari zaidi. http://www.living-foods.com/articles/coconutwater.html

Mzee wa Changamoto - hilo la pete nalo ni jambo. Wengi wetu tunajivalia tu hizi pete hata bila kujua hasa maana yake ni nini. Ni fasheni tu. Ukisoma historia yake na kugundua kwamba chanzo chake hasa ni dini za "kipagani" za kale kule Misri, Babiloni na Roma basi mtu unashangaa.

Hivi wenye wake zaidi ya mmoja huwa wanavaa pete ngapi?

Nakubaliana nawe - pete ya moyoni ni muhimu zaidi kuliko hizi tunazovaa hata bila kufahamu hasa zinamaanisha nini!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mpangala, nataka copy za makala zako juu ya freemasons, nitumie kwa email au niambie ziko blogu gani. naona umejaribu. nina kijitabu kinawaongelea hawa labda twaweza shea

Mzee wa Cmoto, vazi hili kwakweli ni la kiafrika zaidi na lilibuniwa na fundi wa kawaida tu wa mtaani, tatizo la wajasiriamali wa bongo ni kujitangaza. ni rahisi kulipata na ukilihitaji labda tuwasiliane kama mimi nihitajivyo the way u see the prob...

nimekuwa na pete ya moyoni kwa muda mrefu sasa ila nimelazimika kuvaa na hii ya mkononi. labda tuone itakaa mpaka lini

kuna kitu kinagundulika hapo kuwa nikama krismassssss yaani sikukuuuuu,

duh, natuone katika hilo

napenda sana kula vitu vya kienyeji /kiasili kuliko vya kiulaya / viwandani

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hilo nalo dongo babu...lol

kwani uliihitaji hiyo pete sana?

huoni kuwa itakuwa ni mzigo kwako ama ndo unajiepusha na 'vishawishi' ama timbwili timbwili za mashosti kama Da Koero alivonitishia wakati mmoja?

:-(

Yasinta Ngonyani said...

Nimependa sana vazi lako je huyo aliyebuni anaweza kubuni na za akina mama kama mimi maana mimi na mavazi ya kiafrika ndo mwenyewe..lol Nahisi hilo lilikuwa ndo vazi la harusi safi sana. Naona mlipendeza kweli. Bahati mbaya hutaki kutuonyesha picha hapa kwako..lol

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta, harusi??????? labda, heri mimi sijasema!

vazi waweza lipata binti, na labda nitajaribu kupata ppicha walizopiga wadada wakiwa na vazi kama hilo