Tuesday, January 5, 2010

hivi ni kwa nini watu hubusiana?


12 comments:

Baraka Mfunguo said...

Hongera sana mkuu na karibu katika klabu. Ninakutakia maisha mema na yenye fanaka ya ndoa. Kubwa zaidi ninaloweza kukuambia wewe na mwenzako, ni kwamba kila mmoja ana jukumu kwa mwenzake maisha yote hivyo basi msichoke kukumbushana juu ya maisha yenu huku mkiimbiana zaburi na kumtukuza Mungu. TO GOD BE THE GLORY.

Anonymous said...

Kwa mdomo...!!! Nafikiri wanachukiana ndio maana wanabusiana ha ha haaa

Yasinta Ngonyani said...

kwa sababu ya kupenda:-)

chib said...

Mkuu, nafikiri jibu unalo mwenyewe au vipi?

mumyhery said...

mimi labda nimuunge mkono Chib kwani anona unatuonyesha kabisa jinsi ya kubusu, sasa labda ungeweza kutuelmisha

SIMON KITURURU said...

Ni kwasababu ya U-temporary wa PENZI ndio maana binadamu akagundua mpaka busu kama nyenzo moja yakumkumbushia mpenzi BILA SABABU MAALUMU kuwa bado unampenda ingawa nyenzo hii hutumiwa sana na BABA watoto akitoka kwa KIMADA pia..

Mzee wa Changamoto said...

Labda kwa kuwa huwa unaangalia yale maigizo ya usiku sana ya ITV kina Acapulco Bay na mengine.
Yaani ni kuiga tuuuuuu wala hakuna jingine.

John Mwaipopo said...

kwa sababu ya upendo na mahaba, au?

Mija Shija Sayi said...

Naungana na Kitururu ktk jibu lake.

Candy1 said...

si upendo au??...halafu nasikia eti sijui kina nani wanasema kwamba eti unatakiwa uhisi "magic"...mi sijui ndio nasema eti...lol

You guys look absolutely LOVELY! God Bless you

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@ Mt. Simon: labda

lakini si hata bwana mkubwa jizazi alisalitiwa kwa kupigwa BUSU? :-(

kupenda na kutopendwa yote "saresare maua asiyejua kuchagua kabila lake mzigua!" :-))

nyahbingi worrior. said...

Kaka kamala mimi naamini yakwamba BUSU ni KUSALITI kutokana na Judas Iskariot alivomsaliti Bwana Yesu Kristo.

Katika maisha na imani yangu, naamini busu ni tendo la Judas Iskariot.

N.B.Mtazamo wangu na imani yangu.
Selassi I .