Sunday, January 31, 2010

Kuhusu wanawake.

Kijiwe hiki sasa kinnaanza makala maalumu juu ya kiume wa kike kwa upande wa binadamu au watu maarufu kama wanawake. Tutanngalia mambo mbali mbali juu ya wanawake kama vile mwanamke ninani au kiummbe gain. Nafasi ya mwanamke na umuhimu wake katika jamii zetu, kile kinachoitwa ‘haki za wanawake’ kifanyacho kuwepo na vyama vya kupigania haki zaa wanawake, watoto na hata vijana lakini sio ‘wanauume’!
Damija amechagua baadhi ya wanawake na kukwaita wanwake ‘waShoka’ nilishindwa kuwajua na hivyo kuamua kuuliza mwanamke wa shoka ni yupi na ni vigezo gain vya kutenga na kusema huyu ni wa shoka? Akatokea jamaa akasema ni juu ya shoka au chukka kidogo kiwezacho kuulaza mti mkubwa, nikashangg kwa nini wasiwepo wanawake wa kulinganishwa na vifaa vingine vilazavyo au kuutokomeza mti kama vile Panga, kisu, mundu, na hata Moto uugeuzao mti kuwa mkaa kama sio majivu? Jibu ni kujikanyaga.
Kama asemavyo mshahiri maarufu wa kale Shaaban Robert kwamba ulimwegu umechagua watu wa chache na kuwasifia, kuwaita watakatifu nk huku wengi na wanaostahiri wameachwa pembeni, ndivyo ilivyo hata kwa hawa waitwao wanaweke wa shoka, wakati mwingine yawezekana sio wa shoka, panga wala kisu kulinganisha na wale halisi na tutaliona hili.
Vitabu vya dini vinatuonyesha kuwa mwanamke si chochote na hana lolote mbele ya mumwe, inakuwa tamu unapokutana na wanawake wanaharakati kama Koero harafu ni wakristo kwa wanalazimishwa kufuata imani mikumbo hizo. Wewe! Kuibishia dini ni dhambi na heri yao wale walioandika miongozo a.k.a vitabu ya dini / vitakatiifu. Eti Eva a.k.a Mwanamke alitoka Ubavuni mwa dume a.k.a Adam, dhana hii siikubali sana.
Toleo lijalo tutaanza safari hii juu ya kiumbe mwanamke, mchango wako unakaribishwa, ila wakati unachangia, vua jinsia yako, sahau utamu au uchungu akupatiao yule wa jinsia tofauti na yako, harafu uchangie katika uhalisia. But I love the women
OMUKAMA ABABEELE

4 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Kamala: nanukuu 'but I love women'.

kwa nini 'you love' them? Je ni kwa sababu wana matumbo? :-( Maana nasikia kuwa WOMAN ni kifupi cha WOMB-MAN :-(

Nasubiri kumjua huyo mwanamke ni NANI/NINI hasa.

Halafu ukishamwelezea mwanamke nami ntamwlezea mwanamme ;-)

SIMON KITURURU said...

Labda MWANAMKE ni mkusanyiko wa kemikali kama Hormones...nk. + Uke.

Maana si nasikia kuna midume inajisikia iko kwenye wrong body ndio maana kuna Basha na Msenge katika Homosexuality?

Na si inasemekana tu mahomoni fulani yakimzidi dume chuchu lazima ikue na ni fulu kutikisa tako katika mwendo na kikosekanacho huwa ni uke tu katika kufanya tumizi la mbele liingizwe badala ya kuingiza?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@CHACHA, dont yo love them?
@simeoni, DUH

chib said...

:-)