Wednesday, January 27, 2010

maisha ya mikoni na yale ya Dar es salaam

sijui kwa nini kuna sehemu zinazoitwa mikoani na labda Dar haiitwi hivyo wakati pia ni mkoa! kama kuna mwenye ujuzi juu ya hili atujuze basi

nimeishi Dar miaka mitano nikiwa na nia ya kuhama na sasa kuhama hukokumewezekana japo nitalazimika kuwa na safari za mara kwa mara kuelekea Dar. kwa kwelil maisha nje ya Dar ni mazuri, hulazimiki kuamka asubuhi saana kuwahi usafiri au foleni wala jioni huitaji sana kuwa na hofu kwani huchelewi wala hugongani na foleni

hali ya hewa ni nzuri mno hapa. siku moja nikiwa mkoani kagera, nilipanda basi kutoka kyaka kuelekea bukoba mjini, nilidhani basi lile lilikuwa na air condition (AC) kwani vioo vilifunguliwa kidogo na iliingia hewa saafi na upepo mwanana vya kutosha sana.

gharama za maisha ni nzuri na kuna aina mbali mbali za vyakula vya asili, matunda ya kufa mtu nk. maji ya mito au bomba yakichemshwa ni mazuuri sana kunywa kuliko hata ya dukani wakati Dar sio hivyo. hata ukioga, unajisikia fresh kweli kweli.

ila changamoto sio nyingi kwani wengi wanakusikiliza zaidi. hulazimiki kuwa na gari wala kutumia daladala, waweza tembea kwa miguu, au hata baiskeli!

8 comments:

Munale said...

Kwangu Dar ni mkoani pia,ninaichukuli
a sawa tu na mikoa mingine.Kila mkoa
una uzuri wake na faida ya kipekee
katika nchi.
Siku moja nikiwa Dar bwana mmoja
aliniuliza nimetoka mkoa gani?
nikamwambia Mwanza,akaniuliza vipi
Mwanza ukiilinganisha na Dar kwa
ukubwa? nikamwambia Mwanza ni mkoa
mkubwa,una wilaya 8.
Jamaa yule hakutegemea jibu langu hilo maana watu wamezoea
kuisifia Dar hata pasipostahili.
Ukimwambia mtu kuwa Mara ni kubwa
kuliko Dar hatakuelewa wakati ndiyo
ukweli

Mija Shija Sayi said...

Kamala umehamia wapi sasa? Kagera, Musoma au Mwanza? maana siku mbili hizi umekuwa huchezi mbali na mikoa hii.

SIMON KITURURU said...

Ila mazoea yana tabu zake kwa kuwa kuna marafiki zangu kadhaa naowajua ambao huwezi kuwaondoa Dar.

Kama alivyouliza DaMIJA : Uko wapi Mkuu?

Mzee wa Changamoto said...

Nilipokuwa Kishanje hukoooo Bukoba vijijini watu wakisema "naenda Bukoba" basi ujue anaenda katikati ya mji. Nikawa Bukoba Mjini wakazungumza kuhusu kwenda Dar. Nilipohamia Dar nikakaa Mbagala (mie mporipori kwa hiyo msishangazwe na makazi yangu) na Mama tuliyekuwa tunaishi naye (apumzike kwa amani alipolala) akasema "mkinisikia nasema naenda Dar mjue naenda Katikati ya jiji". Nikajua ahaaa. Kumbe hata Dar kuna Dar? Mmhhhh!! Katikati ya mji nilikokuwa nafanyia kazi nikasikia kuna "mamtoni" ambako ni Marekani na Ulaya na kwingine nje ya Tanzania. Nilipasikia pakisifiwa na kufanywa paonekane kama "mbingu-toto" na Mungu si Athumani nikajaaliwa kuingia hapo "mamtoni". Mmmmmhhh!!! Ntamezea yaliyopo. Kisha nikaenda mtembelea Babangu wa Ubatizo Austin Texas yeye na wenzake wakawa wanazungumzia kuhusu Washington DC kama vile ni nchi nyingine. Niliporejea DC Metro nikaamua kujisogeza "mjini" DC kushuhudia kilichopo huko ambacho kinamfanya mtu apaone kama pahala patakatifu. Ajabu ni kuwa baadhi ya sehemu ndani ya "mji mkuu wa nchi babe na tajiri kuliko zote duniani" ukanikumbusha Tandale na Manzese. Baadhi ya maeneo hata askari wanaogopa kwenda. Ni kuchafu kuliko unavyoweza kudhania. Kunanuka, watu wanajishughulisha na madawa ya kulevya na utaahira wa hali ya juu.
Na kwa bandiko hili nimerejea mawazo haya (lakini sasa KWA JICHO LA NDANI) na kuishia kujiuliza "hivi huwa tunasifia tunapopajua ama tunapotamani kuwa?

I looove country life. Kuna uhuru, kuna nafasi, mfumo wa maisha unaendesha dunia na dunia haiuendeshi na pia watu wanajali utu. Hakuna maisha yajaayo mawazo yasonganishwayo na ugumu wa maisha.
HONGERA SAANA KAKA KWA KUAMUA KUJINAFASI.
Swali la Da Mija lafaa kurejewa. Ni kipande ama fasi ipi umehamia?
Baraka kwako na familia yako popote mlipo

mumyhery said...

Mija bora swali limepata muulizaji, maana yake hizi safari!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Munale wale wanajua ukubwa wa mji, eneo au nini!

@mtaka'tifu'mazowea yana tabu kweli na ilikuwa vigumu kuhama, nilianza mchakato tangu 2007 lla lengo nisizidi mika mitano, imezidi miezi minne.

ukiangalia profile yangu vizuri, inasema niko kanda ya ziwa, Kumbuka mikoa ya kanda ya ziwa inahusisha kagera, Mwanza, shinyanga na mara! kwa hiyo nimehamia kanda ya ziwa! worry not
ila mimi sio mpenzi wa samaki.

Yasinta Ngonyani said...

Oh! kumbe umihamia kanda ya ziwa halafu hupendi samaki. Basi ile safari yako ya kuja huku Sweden kwa miezi mitatu utakonda sana maana katika nyumba hii samaki ndo chakula chenyewe. Kila la kheri

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Yasinta, nita cope!