Thursday, January 7, 2010

msaidieni Nestory Enericko asome!

nimeamua kutundika mtundiko huu baada ya maoni yangu katika blogu ya mwenzetu matondo ambao umemgusa mtanzania mwema mmoja. unaweza kuona maoni yangu hayo hapa. niliongelea juu ya kijana ninayetamani kumwona akisomea katika mazingira mazuri lakini najitafuta sana kiuchumi,

kwa kifupi habari hiyo iko hivi; kijana Nestory Eneriko Kashekya alikulia kwenye familia yetu kule kijijini na alikaa pale kwa sababu tu kaka yake alikuwa houseboy wetu. baadaye kakayake alifukuzwa kazi ila yule kijana akakaa kwa muda. baadaye naye akafukuzwa. binafsi niliguswa na utulivu wake na uwezo wake wa akili za kuzaliwa na alivyofanya vyema shuleni.baada ya kuondoka nyumbani alienda kijijini kwao na kumalizia darasa la sana akashinda na kujiunga na shule za kata kijijini kwao ni Bugorora njia ya kuelekea kyaka-mutukula-uganda.

sikuwasiliana naye kwa kipindi kirefu na kuna wakati nilienda kumsaka ili nimpe anagalau pesa ya kununulia madaftari nk lakini sikumpata. nilipata taarifa kuwa baada ya kusomea shule ya kata ya bugorora na kukaribia kidoto cha tatu, shule ile haikuwa na walimu kwa hiyo alihamia shule ya kata ya kyaka na nikaambiwa anatumia baiskeli kwenda na kurudi, ni kama km50 hivi na risk kwani barabara kubwa ile. juhudi zake hizi na uwezo wake wa kiakili vilinikuna najisikia nisipofanya jambo ntakuwa sijatenda wema.

basi kuna shule ya private imeanzishwa pale bukoba mjini karibu na nyakato nanishule ya kanisa la KKKT, nia yangu ni angalau ahamie pale na kumaliziakidato cha nne akiwaboarding na akializa tutafute jinsi na ninaamini anaweza kufanya vizuri kwa kwelikwa hiyo inahitajika karo ya mwaka mzima shs laki saba na vitu vingine kama sare, vitabu nk.

baada ya maoni yangu hayo katika blogu ya prof Matondo, kuna mtanzania mwema aliyejitokeza na kuahidi kutoa mchango wa lakimbili ili nestory aende shule, sikuamini na kuamua kuzungusha kibakkuli hapa kijiweni ili kama kuna wengine wenye nia basi watoe kadri ya uwezo ili kijana Nestori akamalizie kidato cha nne katika mazingira mazuri ya Boarding ili aweze kuendelea vizuri kielimu natanguliza shukrani wakuu.
NB: sikuwahi kusema jambo kama hili kwani siamini kwa watz kuchangia elimu lakini mabadiliko yaweza kuanzia kwangu na wewe.

Asantesana
kamala JL kny UONGOZI WA KIJIWENI BLOG

7 comments:

chib said...

watu watasingizia mwezi huu ni wa kupeleka watoto shule, na sikukuu zimewapukutisha mifuko!

Kutoa ni moyo, lakini kama zipo!
Nakusaidia kupigia debe!!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kama tunaweza kuchangishana mamilioni kwa ajili ya harusi, mbona tushindwe kwa jambo jema kama hili???

Mija Shija Sayi said...

Mimi nachukua jukumu la viatu, soksi na kalamu hadi amalize kidato chake cha nne. Naomba namba ya mguu wake na anuani yako kamala.

Bless you.

Anonymous said...

Even the bloggers who complain a lot about issuez now they are quiety. Suggestion. Sema kwamba you need money for your wedding or kitchen party hapo utapata shs. Lakini school, who cares about school? We are Tanzanians Bwana ala!

Bloggers tazameni you will be hypocrities.

I am not a blogger but I wanna help this guy. So kamala, I will send you (Tsh. 25,000). This is what I can afford now but I may be able to offoer more later! Bye

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nawashukuru sana nyote mliojitolea. Damija nadhani kama uko nje pea moja au mbili za viatu kama ni vya darasani na vya michezo basi vinaweza mtosha kwa mwaka mzima uliobahakia na kama ukitoa kijibox cha kalamu zote mbili peni na pencil basi mambo ni mazuri zaidi

kwa watakaojisikia kutuma pesa walioko bongo mwazeza weka kwenye akaunti yangu benk ya CRDB no 01J39437801 na acc name ni James Luta kamala.

ukiweka pesa yoyote nijulishe kwa njia ya simu email au bloguni hapa.

nitakuwa bk next wee kwa hiyo the week after next weeek kijana atahamia bukoba mjin na kuanza masomo. michango inakaribishwa lakini kwa njia yoyote lazima asome hata ikibidi nipunguze milo yangu, nitafanya hivyo

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

bila shaka wengine hawataandika hap lakini wataachangia!

stay blessed!

SIMON KITURURU said...

Tutajitahidi mkuu! Utanisikia kwa hili pembeni mkuu!