Monday, January 4, 2010

Ndoa zetu na vidumbwe ndumbwe vya michango kibaaaoUkitaka kuoa/kuolewa usimwambie mtu yeyote kama vile ndugu na wazazi kuwa unataka kuoa. Tatizo la kuwaambia ni kwamba badala ya kusheherekea ndoa yako wataanza kusheherekea ndoa zao na labda kulipiza visasi vyao kwa wengine.
Ukijiandaa kuoa na kuwaambia wazazi, ndugu jamaa na maadui utasikia wakinza taratibu za kukuksanya michango ya harusi hiyo. Sio kweli kwamba wataandaa michango ili kufanikisha sherehe hiyo ambayo sio muhimu sana bali wataandaa sherehe zao wao wenyewe. Utasikia wanasema jamii itanionaje na kusemaje kwamba kijana wetu anaoa haarafu sijui ndo nini na nini
Utasikia wanakusanya michango tu eti kwa sababu na huwa wanawachangia hao wakusanyao michango kwao na sio ishu ya kufanikisha sherehe hiyo. Kwa hiyo ndani ya sherehe yako kuna wanaokuja kwa lengo la kusheherekea na wengine kula walichokilipia huku wakijiandaa nao kuchangisha. Basi utafanyiwa sherehe ya mamilioni lukuki.
Binafsi sikupenda seherehe yangu igharimu mamilioni na kulazimisha watu kutoa michango na sikutaka taratibu za kujionyesha zitawale sherehe hiyo na hivyo nilitamani kitu cha tofauti na mazoea ya kila siku. Basi sherehe ilibidi isizidi thamani ya shs laki nne na sikutaka suti ya gharama kwani sio mpenzi wa suti na kuvaa suti hapa Dar ni sawa na kujiingiza kwenye jera binafsi kwani joto la hapa na suti utakuwa umejibanika lakini pia sipendelei utamaduni wa kigeni na pia nikivaa nguo za kiafrika natoa soko kwa bidhaa za washonaji wetu wa ndani
Hata hivyo gharama zilizidi mpaka laki sita na sherehe ilikuwa wazi kwa waliochanga na wasiochanga. Nilitoa taarifa kwa ndugu jamaa na maadui wa karibi zikiwemo familia niliiyotokea muda mfupi. Wengi walinigomea kwani sikuwajulisha mapema ili wachangishe kama ilivyo ada. Anyway sikuona soo kwani katika shida za muhimu huwa nabakia peke yangu, iweje harusi ndo yatolewe mamilioni?
Hii yote ni kukamilisha usemi wa prof.Jmbele kwamba tunajenga baa nzuri wakati shule, zahanati, bara bara nk ni mbovu sana kuliko maelezo ikiwa ni ishara ya kkupenda starehe za kula na kuachana namambo muhimu nay a msingi kwa jamii yetu.
Nilichokipenda katika sherehe ile ni kwamba karibia kila mtu alivaa nguo za kiasili naharafu tulifanya mambo ya kitofauti na ikageuka kukwa kama vile ni ndoa ya kifalme. Natamani ningeweza kutundika mkanda mzima wa video hapa!

6 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Kamala: kumbe na wewe ni kafisadi kadogo?...lol yaani laki 6! duh!

Mie ya kwangu haitazidi $ 140 ama Tshs 150,000/= usipokuja utajiju.

Tena nasikia kuwa wazazi wangu wana mpango wa kuzira kuja kwa kuwa nataka kuwowa kwa akina Masangu Matondo....lol

Si unajua wakurya wangependa niwowe mkurya aliyekeketwa?... :-(

Kama walikususa lakini Mungu wako hajakususa hivo mambo mbele kwa mbele, watajiju na vijiba vyao... :-(

Mbele said...

Hongera sana. Nawatakieni kila la heri katika maisha yenu.

Niliona picha za arusi yenu kule kwa Michuzi. Safi sana.

Mawazo yako ya kuhoji mambo yanayofanyika ni murua.

Kila la heri.

Upepo Mwanana said...

Hongera sana mwana blog kwa hatua hii

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

THANKIG U

Mwanasosholojia said...

Hongera Kamala!

Tandasi said...

hongera kamanda mkubwa wa kijiwe nyegerage