Monday, January 18, 2010

nimemtembelea kijana Nestory

bahati mbaya kamera yangu sio kamera, nilitumia muda wa mwishoni mwa wiki kumtafuta kijana nestory, nilimtafuta kwao na kuambiwa ameenda kwa babaye mdogo ambaye ni mratibu elimu kata.

niliaambiwa hayupo kaenda kutafuta majani ya ng'ombe. mvua ilikuwa inanyesha. nilimkuta akiwa na mzigowa majani kwenye baiskeli na umande wa kufa mtu, alichuruzika maji mwili mzima lakini alionekana mwenye furaha.meno yake ya mbele yaliisha toka kwa kile alichonielezea ni ajali ya baiskeli katika juhudi za kuisaka elimu!

babaye mdogo hakuwepo na nilishindwa kuondoka naye. lakini Jtatu ya leo tulikutana Bukoba mjini. kumbe yuko form threee na sio four kama ilivyodhania. shue niliyotarajia kuwaathamia, kumbe karo yao iko juu kuliko nilivyodhania. inagharimu mpaka shs mil 1.5 kwa mwaka na sio laki saba kama nilivyodhania. basi ikawa changamoto ya kufa mtu

kwakuwa mpaka sasa nimepokea mchango wa tsh laki mbili na thelathini na tano elfu tu na msaada wa hali na mali unaopaswa kutoka kwangu na wife wangu, nimeona ni vyema tumie pesa kidogo nimnunulie mahitaji muhimu kama vile vitabu, madaftari, begi la shule, uniform na pocket money wakati nikiendelea kujikusanya ili ipatikane pesa ya kumhamishia bweni (boarding)

kuna shule nyingine za gharama nafuu lakini sitaki kumpeleka mradi tu shule ya bweni ila iwe shule yenye tija na ya kusoma kiukweli ukweli.

kwa dada damija, kijana Nestory anavaa viatu size 40/41. jitahidi ninia viatu imara kwani kuna umande wa kutosha hapa. kuna waliohahidi michango kuwa tutawasiliana pembeni lakini mpaka sasa baaado!

lengo ni angalau mwezi juni kijana wetu awe boarding ili aweze kufanya vyema.

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

Haya nitakutafuta kipembeni unipe anuani yako.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

vuta subira baba, bijampola :-(

Yasinta Ngonyani said...

Kazi nzuri kamala!!Endelea vivyohivyo.

nyahbingi worrior. said...

heri wale wenye moyo kama wako kamala wakusaidia sio tu kutumiana happybirthday.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Wanablogu jamani tuko wengi. Vipi tukitoa laki moja moja au elfu hamsini hamsini tu? Au cho chote mtu anachoweza? Tumelalamika sana katika blogu zetu kuhusu watu kutopenda kuchangia na kujitolea katika mambo ya msingi kama elimu. Mkazo uko kwenye mambo ya harusi na kitchen party. Basi tuonyesheni mfano jamani isije nasi tukaingizwa katika kundi la wanafiki, kundi la maneno mengi lakini vitendo hakuna. Sisi ni nuru ya jamii. TUONYESHENI NJIA!!!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Dkt, umenena. Na tutende sasa

Mzee wa Changamoto said...

Naaaam. Nimekuwa MZITO kwenye kutembea na hata kusoma na sasa katika KUSHIRIKI.
Kama umesema June naamini ni wakati mwema. Tujikusanye na TUTAFANIKISHA.
Asante kwa kuwa na juhudi na Nestory.