Monday, January 25, 2010

safari ya meli to mwanza kwa meli

The MV Victoria, Bukoba, Tanzania, Kigali, Rwanda via Uganda to Mwanza, Tanzania

kama ilivyaoada, nitapanda mmeli huu usiku wa leo ili nifike jijini mwanza kesho jumanne na kelekea Musoma kwa wakukra akina chacha ili kuendeleza libeneke la utambuzi pamoja na shughuli nyingine za kiofisi.

zamu hii nitakaa kwa wakurya mpaka wanikome na kukoma ubishi wa kutwangana pia

darasa la utambuzi litatwangwa mjini Bunda jumaane mchana na msoma tutapanga na kutoa taaarifa, ahsanteni sana na karibuni sana

ila mkisikia mmeli umekunywa maji mjue ndo hivyooooo nami nakunywa nao11111111

7 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa taarifa zaidi, mmeli huu unaondoka saa tatu usiku jijini bukoba na kuwasili saa kumi na mbili hivi jijini mwanza usu-kuma-ni

Yasinta Ngonyani said...

Usiwe na wasiwasi ukinywa maji basi tutakuhifadhi panapotakiwa.

Mija Shija Sayi said...

Safari njema. Yasinta akili yako si nzuri walahi tena...umeniacha nacheka..

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Naikumbuka sana hiyo MV. Victoria. Hata MV. Bukoba iliyozama. Nimekumbuka hata ile safari yangu ya mwanzo kabisa niliyosindikizwa na Baba Mdogo mpaka hapo Mwanza na kupandishwa hiyo MV. Victoria kwenda kuanza form one Kahororo. We acha tu. Safiri salama na kale "BUKIMA" vizuri kule Ukuryani. Ng'wanambiti anajua nazungumzia nini!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Duh

Mzee wa Changamoto said...

Kumbe huko ulikokutaja ndiko uendako? No wonder unakenua ukikufikiria.
Basi enjoy

mumyhery said...

Safari njema