Thursday, February 11, 2010

changamoto kwa wanawake---kujitafuta nje yao!tunaendelea na mada juu yamwanamke, tumeona mazuri ya mwanamke na mwanamke alivyokuwa kiumbe mzuri aliyekamilika na kiumbe muhimu katika maisha yetu. lakini mwanamke anachangamto kibao zinzzomkabili huku changamoto kubwa ikiwa ni kujitafuta nje yake kamaasemavyo kijana wa changamoto kwamba tunajipoteza katika harakati za kujitafuta

mwanamke anasahau uzuri alionao ndani mwake, na umuhimu, anaanza kufanya vitu vya ajabu nje yake na kujitafuta huko! mwanamke huyu huishia kujiharibu yeye na jamii nzima. angalia nyuso za wanawake wengi, zimeungua ungua na ngozi zao ni mbovu kwa sababu ya kujitafuta nje yake kwa kujipakaa sumu wao wanaita uremboo

nywele za mwanamke zimetiwa sumu ya ajabu na kufinyangwa finyangwa ili apendeze, kumbe ajiharibu yeye na jamii nzima nilidhani hii ni kwa wanawake wa mijini kumbe hata wa vijijini

mwanamke anahangakia kuvaa mavazi ya ajabu ajabu na mengi huishiakumpeleka pabaya. pia huongea kwa njia fulani fulani na kuacha uhalisia wake
anapenda kujibainisha nje yake, anajiharibu yeye, watoto, Mume, wapenzi wake nk na hivyo kuiharibu jamii nzima

yampasa mwanamke kujiamini yaani kuwa yeye, kusimama ktika nafasi yake na kutambua jambo muhimu kwamba uzuri wake umo ndani mwake kwa ajili ya jamii nzima na sio nje yake kama anavyoendelea kujitafuta huko!
bila
uzuri wa mwanamke ambao umo ndani yamwanamke, maisha yanaweza kukosa maana yake,

mwanamke, umekamilika, jiamini na acha kujitafuta huku ukijipoteza


I love HER

7 comments:

chib said...

Nywele zimetiwa sumu ili zipendeze!!
Duh! Nilifikiri utasema zimetiwa nakshi kupendeza, mimi najua sumu ni itu kibaya au vipi?
Mada zako za maisha nimezipenda. Hongera sana Mkuu!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Kamala, Kamala: Unatafuta ugomvi na watu sasa.

Mi simo ukija kuomba msaada wa mawe....lol

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmh!! mada hii ngoja niitafakari nitarusi:-)

Mija Shija Sayi said...

Nimeipenda hiyo I LOVE HER naanza kushawishika kwamba wewe ni mwanamke wa shoka, lakini uendelee hivyo hivyo sio baadaye unabadili mwelekeo.

Kwa Upande wa mada naona siku hizi si wanawake tu wanaohangaika na sumu za kutafuta urembo, wanaume pia wamejiunga. Sasa naongeza swali mheshimiwa Rais Mtarajiwa, wewe kama Rais(ukishaingia madarakani) utafanya nini kurekebisha hali hii?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Mija: kijiwe hiki kinatawaliwa na sheria na kanuni. Je unaweza kuthibitisha kuwa 'naona siku hizi si wanawake tu wanaohangaika na sumu za kutafuta urembo, wanaume pia wamejiunga'?

Kama huna ushahidi uko tayari kula suspension kwa uda wa wiki moja?....lol

Mija Shija Sayi said...

Kwanza samahani Kamala, mkono uliteteleka nimeandika Mwanamke wa shoka badala ya Mwanaume wa shoka.

@Chacha mfano wa chapchap fungua hii link..
http://2.bp.blogspot.com/_JI2CjMwyBpw/STQl0UXSV5I/AAAAAAAAFa0/WiL3Sd1loZc/s400/ben+kinyaiya.JPG

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

KAribu,

Yasin yasinta, utarudi waapiii???
chacha, wanawake wana upendo, wanazaa na kulea, hawarushi mawe, ....usiniulize wale wanao abort.....

damija ukisema mimi ni mwanamume wa shoka maanake ninachanja sana kuni mimi, nadhani shoka liendelee kuwapimia wanawake na sio wanaume, sasa mtu kama chacha anayerusha mawe na anatembea na mawe, utamwitaje mwanaume wa shoka?? niliwahikumshuhudia akiurushia mti mawe mpaka ukafa.

kuhusu kuwa rais?? naomba uendelee kuniandaa