Friday, February 5, 2010

juu ya re-incarnation au kuzunguka kwetu

blog ya maisha a.k.a ruhuwiko pale kwa mama mrembo amenukuu makala juu ya kuzaliwa kwetutena na tena kwamba sisi tumewahi kuwepo na sio ara ya kwanza kwetu kuishi kwenye miili kwamba tuliwahi kuivaa miili (kuzaliwa) na kuivua (kufa) na kuendelea tena na tena.

huko nyuma niliwahi kuandika juu ya kila kitu kuzunguka lakini sikupenda kuongelea juu ya kuzaliwa na kuivaa miili tena na tena kwani wakati ulikuwa bado na leo nachovya tu kidogo

kama tungelitambua hili upendo ungeongezeka duniani, tatizo ni kudhani sisi ni miili na sis tunaishi maramoja tu jambo ambalo labda sio sawa.

kuna nadhalia nyingi juu ya hili lakini kuna uhakika pia kwamba sisi tunazaliwa tena na tena, kufa na kufufuka pia. maisha yetu ni mzunguko, kwawanoamini katika uumbaji ni kwamba kazi ya uumbaji ilifanyika ara moja tu na hivyo sisi soote tulimbwa siku na yaliyo baki ni kuzungukatu kwenye miili, tuazaliwa tunaishi, tunakufa na kuvaa miili mingine, kwa wanaoamini / au kujua masuala ya evolution jambo hili halina ubishi

tunelelewa kwenye imani lakini kuna changamoto zake pia kama vile Yesu Kristo kupaa mbinguni! na mwilikwambaatarudi duniani! KWa kuangalia tu bila kutumia sayansi ni kwamba miili yetu ni mali ya udongo.

ili tuzae, tunapaswa kufanya ngono, yale mayai yanatokana na protni itakayo kwenye vitu kama maharagwe, yatokayo udongoni! ili tuwe na afya ni lazima tule vyakula vya udongoni na baada ya hapo, na sis hufa ili tukawe chakula cha funza na baadaye kuwa undongoni na ndiyo maana wakristo wazikapo, hudai ulitoka mavumbini na utarudi mavumbini.

kumbuka sisi sio mwili ila sisi ni wakazi tu wa mwilini, sis ni uwepo japo tumetanguliza faida za kimwili zaidi.

tunawezakuishi kama wanyama, mapepo na hata watu na kuzaliwa tena tukiwa vile, ndio maana sisi sote wamoja.lakini mafundisho ya santmat yanatuelezea ni kwa namna gani tukiweza kuishi kwa upendo na uhalisia na kufanya tahajudi ya nuru na sauti basi tukiacha miili hii hatutarudi tena kwenye mzunguko wa kuzaliwa na kufa (reincarnation) na badala yake tutajiunga na chanzo chetu a.k.a Mungu

kuna kitwa kinachoitwa karma (law of action and re-action) kwamba vile tunavyoishi sasa yaani matendo yetu, mawazo na maneno yetu ndivyo vinavyotupangia na kutuamlia maisha yetu ya baadaye au wakristo huita hukumu. hukumu ya Mungu au shetani sio hiyo bali na matendo yetu katika maisha yetu yaani karma
hata maisha tunayoishi sasa yanategemea sana karma za maisha yetu yaliyopita na ndio maana kuna wanaoonekana kama wameadhibiwa nk kwa kutokana na maisha yaliyopita lakini kuna wanaolipa karma zao ndani ya mwili huu huu.

reinacantaon ni fact na ndio maana nilitoamifano ya meditators wa pale faji-kimara. maisha unayoishi hata mke /mume uliyenaye inatokana na karma zako za maisha haya na yaliyopita na hivyo ni lazima tuwe wapole ili tulipe madeni ya karma zetu vizuri sana tu.

MADA YA WANAWAKE ITAENDELEA

4 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

kweli eh! nadhani tutajadili hili bila kusema fulani 'pengine' alizaliwa samaki kwa kuwa anapenda samaki....lol

mamake unaweza kuanza ku-speculate 'oh1 kumbe yawezekana kamala aliishi kama mti hapo zamani' ....lol

Yasinta Ngonyani said...

Nafikiria kama kuna mwingine alikuwa kama mimi au atakuwa kama mimi nifapo.

Shabani Kaluse said...

Salute!!!!!!
Darsa zuri sana hili.......

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Yasinta hacha kujibainisha na mwili huo, wewe sio mwili, wewe ni zaidi ya mwili na kwa hiyo wew hufi na hutakaa ufe ila mwili wako ndo unakaribia kufa, wewe utatoka ndani ya huo mwili na sio vinginevyo